Public Opinion: Je, Rais Magufuli amfute kazi Mkurugenzi wa EWURA?

Hii inachanganya watu. wote hao ni serikali. watu watatu: kwanza Tanesko na takwa la kuongeza bei na sababu walitoa. Pili ni EWURA kwa kukubali ombi la Tanesco lakini kwa kupunguza kiasi ni lazima walijiridhisha. Tatu ni waziri na katazo lake nadhani siasa imeingia hapo ili serikali isionekane haijali raia.
Kwa hiyo mambo yanachanganya! yaani hali halisi dhidi ya siasa
 
Poll yako iko wapi hapo?? Huoni kuwa huyo mkurugenzi alitumiwa na mtu fulani kujipatia umaarufu?? Ati, kapiga stop. Nnani kakuambia?? Yote danganya totooo. Watu wanatafta kik
 
Kabda hakuomba approval nk kwa mamlaka husika,ukipandisha umeme bei unaua viwanda kidogo kidogo
 
Nafikiri hao ndio wale wanaomkwamisha Rais katika kauli mbiu ya hapa kazi tu na Tanzania ya Viwanda basi amtengue tu huyo ni kikwazo sana
 
Kabda hakuomba approval nk kwa mamlaka husika,ukipandisha umeme bei unaua viwanda kidogo kidogo

someni repoti ya ewura juu ya procedures nzima zilizotumika kufikia maamuzi. itakuwa ni uonevu wa ovyo sana kumuonea mkurugenzi wa Ewura kwa kufuata utaratibu wa kisheria. Kama serikali haikubali basi ilipie hizo Gharama kwa Tanesco.Tunajua Serikali kwanza hailipi madeni harafu unataka kumdhalilisha EWURa..Ujinga wa ajabu. Hii thread inafanya watendaji waache kuisadia serikali na mwishowe nchi itayumba.
 
Agency zote za serikali kabla ya kufanya chochote zinapaswa kureport kwa katibu mkuu wa wizara agency hiyo ilipo. Je hili halifikufikiwa?
 
Kujiuzulu ni njia nzuri pia.

Ajabu sijaona kiongozi ambaye alitangaza kujiuzulu kwenye utawala huu wote wanasubiria kutumbuliwa
 
Wadau naweka hapa kura ya maoni kama Raisi Magufuli amfukuze kazi Mkurugenzi wa EWURA ama abaki baada ya tangazo lake la kuongeza gharama za umeme kugonga mwamba na kuzuiwa na Waziri Prof. MUHONGO... Je kuna uhalali wa mkurugenzi kubaki kwenye nafasi hiyo?

Ni kweli maana km yule mama/mkrgnz Wa NEMC alichapa basi huyu naye achapwe tu vilevile
 
Kwanini wakati Tanesco wakiomba kwa Ewura kupandisha bei Waziri Muhongo hakuzuia kwani Tanesco iko chini ya Wizara yake.
Hii ni aibu kubwa kwa serikali kwa kushindwa kujua uwajibikaji wa viongozi wake waandamizi kwani Waziri Muhongo alijua kilichokuwa kinaendelea na alikuwa na uwezo wa kuzuia kabla EWURA haijatangaza ongezeko hilo.
 
Wadau naweka hapa kura ya maoni kama Raisi Magufuli amfukuze kazi Mkurugenzi wa EWURA ama abaki baada ya tangazo lake la kuongeza gharama za umeme kugonga mwamba na kuzuiwa na Waziri Prof. MUHONGO... Je kuna uhalali wa mkurugenzi kubaki kwenye nafasi hiyo?
Mi nimekuja mbio nikajua kuna ile polling station nitwange kura yangu
 
Wadau naweka hapa kura ya maoni kama Raisi Magufuli amfukuze kazi Mkurugenzi wa EWURA ama abaki baada ya tangazo lake la kuongeza gharama za umeme kugonga mwamba na kuzuiwa na Waziri Prof. MUHONGO... Je kuna uhalali wa mkurugenzi kubaki kwenye nafasi hiyo?
Hivi unajua Dg wa Ewura anavyopatikana?
 
Back
Top Bottom