PSPF wakaidi agizo la N/Waziri wa Fedha kulipa wastaafu

FORCE NAMBA

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
937
327
Naibu waziri wa fedha alitoa siku saba tangu ijumaa wiki jana wawe wameshalipa wastaafu viinua mgongo lakini mpaka ijumaa wiki hii hakuna dalili za malipo hayo. Tatizo ni nini hapa au mifuko hiyo kuna majipu hapo?
 
Naibu waziri wa fedha alitoa siku saba tangu ijumaa wiki jana wawe wameshalipa wastaafu viinua mgongo lakini mpaka ijumaa wiki hii hakuna dalili za malipo hayo. Tatizo ni nini hapa au mifuko hiyo kuna majipu hapo?

Hii Mifuko ni tatizo Mhe. Rais teua watu watakaoendana na kasi yako haya majipu yatumbue haraka yatakuharibia kasi yako
 
Kwa kweli PSPF hawa jamaa hawaogopi kabisa ila wachunguzwe kuna kitu hapo!
 
Hawawezi kujichunguza,wasubiri mwakani kupoteza wateja,hasa walimu weng wataenda mifuko mingne,imekuwa dharau sasa
 
Mhe. Rais apitie upya teuzi zao wengi wao waliingiza kwa kubebwa ndo maana wanakuwa na viburi na hii isiwe kwa pspsf tu atengue teuzi zote za watendaji wa hii mifuko
 
Tangu mwez wa 4 watu hawajalipwa,wawatengenezee na riba,maana hakuna namna tena,wanahtaj viboko
 
Pspf ni janga wamerelax tu maofisini hawafuatilii na kuwachukulia hatua waajir wasiowasilisha michango matokeo yake wanakaa kuwazungusha wastaafu tu
 
kuna sehem zingine ukifanya kazi unapata laana tu za wazee!!!
wafanyakaz wengi wa mifuko ya pension wanalaana tiari, mambo ya kuwashindisha wazee njaa tangu mwezi wa nne na bado mnajenga mighorofa posta ni dharau za wazi
 
Wastaau wanaishi maisha ya tabu sana Mhe. Rais tumbua haya majipu haya matatizo hayakuanza leo hawa watendaji kila leo walikuwa hawakai maofisini walikuwa busy na safari za nje bila kujali kwamba wanacham ndo wamewafanya wawepo pale na pia wamegeuza hii mifuko kama kampuni zao binafsi wanapeana ajira kwa kulipana fadhila.
 
Mods,tafadhari sticky huu uzi,ili wengi wapite hapa,maana ni tatzo kubwa la jamii,tafadhari usiondoe hii habari
 
Hii mifuko ina hali mbaya kifedha kwani kwa muda mrefu serikali haijapeleka michango kwao, hivyo hata serikali inajua nini tatizo.
 
Inatia haibu sana watu wanakatwa toka waanze kazi miaka 50 hadi 55 tena serikalini pesa yao waliolimbikiza wenyewe inakuwa shida kuwapa au kuna nini kati yao na serikali !!!!???? Inatia shaka kidogo
 
Hivi unapotoa agizo wiki moja fedha fulani iwe imeshalipwa, una uhakika kuwa hiyo pesa ipo tatizo ni uzembe wa wahusika au ili mradi kutoa matamko tu? Tatizo kubwa la mifuko mingi ya jamii ni serikali yenyewe kuwa mkopaji mkubwa na kutokulipa utadhani fedha zinawekwa kwa ajili ya serikali ikiishiwa. Kama kweli mtoa order alikuwa na uhakika kuwa fedha zipo basi achukue hatua vinginevyo matamko yatakayofuata yatakuwa hayana maana.
 
serikali imekopa sana pspf, pesa ya mafao inapatikana kwa kudunduliza, pole mkuu force namba, ulikuwa idara gani
 
Wastaafu kwa kweli wanateseka sana....ujinga mwingne upo pale hazina kuna watumishi wanapenda rushwa...yani kumsaidia mstaafu kupata haki yake ni mpaka hapewe chochote bila hivyo atazungushwa kila siku ataambiwa file halionekani.
 
Huu ni mwezi wa 3 sasa mzee wangu wanamzungusha kumlipa pension yake...ukiwahuliza eti file halionekani.
 
Serikali yenyewe ijiulize tena hiyo hiyo Wizara ya Fedha mara ya mwisho kupeleka makato ya pension ya wafanyakazi wa Serikali PSPF ilikuwa lini, je Serikali inalipa madeni makubwa iliyokopa likiwemo la kujenga UDOM, vipi lile deni kubwa sana la Serikali PSPF inadai maarufu kama pre..1999. Mama Waziri usikurupuke anzia Wizarani kwako.
 
Yani PSPF sio mfuko rafiki hata kdogo,utadhan ndo imeingia kwnye ushndan,ovyo kbs,PSPF full kujifia,tunalaan sana
 
Wadau sijui hapa tutumie mbinu ipi ili ujumbe ufike kwa walengwa. Naona kwa kiasi kikubwa serikali nayo inachangia kukwamisha malipo ya wastaafu
 
Back
Top Bottom