PDPF au PSPF?
mkuu c walisema riba ni 1%Naomba kupata ufafanuzi wa hili kwa wahusika wa mikopo ya elimu PSPF.
Ninahitaji mkopo kwa maelezo yao wanakulipia moja kwa moja chuoni ni jambo zuri, wanasema riba ni 7. 5 %kwa mwaka ambayo ni tofauti na mabenki mengine yenye kuanzia 18% tunashukuru.
Ndgu zangu nimeenda nataka mkopo wa 4. 6mil kwa ada. Wakaangalia salary slip na calculations zao wakanambia ntakatwa 119000 hivi kwa mwezi kwa miaka5. Kuzidisha hiyo ni km million 7. 1 narudisha.JE HII NI SAWA NA 7. 5 Kwa mwaka? Crdb ukitaka hela hiyo hiyo wanakata 117000 kwa miaka5 na riba ni 18%. PSPF mnatukomboa au mnatuibia wafanyakazi?
Vilevile mtu ni mfanyakazi kwa miaka 7 kwann asipewe hela ya mkopo kupitia makato yake mnatupa form za Post Bank tupitishe kwa waajiri kama tunavoomba mikopo binafsi usumbufu mara mbili hii inakuwaje?
PSPF tafadhali majibu.
Hakuna riba ya 7.5. Riba yao ni 14. Mimi nilifatilia wakanijazia makato elfu 75 kwa miaka 3. Kiwango hicho hicho backlays wanakata 77 kwa mwez kwa miaka 3. Bado pspf wasumbufu wana sehem ya kusaini mwajiri, wanataka barua ya ruhusa, wanataka invoice kutoka chuo, salary slip certified,fomu yenyewe inapitia mahakani tena bado watumishi wao wanajib kwa nyodo utadhan wanakusaidia. Mimi niliwachana palepale ofcn kwao na fomu zao nilizichana.Nikawaambia ukija utaratibu wa kuhama mfuko ntawahama