Ule ni mgomo wa wafanyakazi wote serikalini, walimu wakiwa wamoja wao. Cha kushangaza rais wao na serikali kwa ujumla toka mgomo huo uanze yapata mwezi na nusu sasa hataki kukutana nao kusikiliza kilio chao cha kuongezewa mishahara. Rais wao anaonekana kutojali kabisa, anaendelea na mambo yake ya kawaida kama vile hakuna tatizo nchini kwake. Ilitakiwa awasikilize wafanyakazi hao na kuchukua hatua za kurekebisha malalamiko ya wafanyakazi wake, leo ni mgomo kesho wanaweza kuandamana kwenda ikulu hali ikawa mbaya. Yeye amekuwa wa kwanza kuvunja ubalozi na libya kwamba gadafi anaua raia wake halafu yeye anashindwa kuwasikiliza wafanyakazi wake, wakiandamana sijui atafanyaje.