Kwanza naona kama vile unachanganya vitu viwili hapo, income tax (kodi ya mapato) na property tax (kodi ya majengo) ni kodi mbili tofauti na zinaongozwa na sheria mbili tofauti. Property tax inakusanywa na local govts (kwa sasa wamewapa hiyo kazi TRA kwa DSM) na Income tax inakusanywa na TRA kwa ajili ya central govt. Either way, wastaafu hawapo exempted (chukulia kwa mfano mstaafu ana nyumba arobaini za kupangisha....kweli asamehewe kodi kwa sababu tu ni mstaafu!?).