singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
KATIKA siku za karibuni vyombo kadhaa vya habari vimeandika habari kuhusu wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kuhusishwa na matukio ya ubakaji katika maeneo ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako wanalinda amani chini ya Umoja wa Mataifa -UN.
Kabla ya tukio la kubaka, kuna habari nyingine iliwahi kusambazwa kuhusu wanajeshi wetu kurushiana risasi na watu wengine baada ya kutokuelewana.
Mambo yote mawili sasa hivi yanafanyiwa uchunguzi hata hivyo kashfa hii haiwezi kupita hivi hivi bila kutolewa maoni na wadau wengine.
Tukumbuke wanajeshi na polisi wa Tanzania hawako Mashariki ya Kongo pekee, bali wengine wako katika Jimbo la Darfur huko Sudani, na Lebanon. Aidha JWTZ wamewahi kwenda nchi nyingi kwa ajili ya kulinda amani, kutoa mafunzo na misaada mengine chini ya UN.
Pia, jeshi hilo lina historia ndefu ya harakati za uhuru na ukombozi kwa nchi za Afrika, kuanzia Angola, Namibia , Botswana, Afrika Kusini na Msumbiji. JWTZ limewahi kufanya Operesheni katika visiwa vya Comoro kwa mafanikio makubwa na kuinusuru hali ya usalama ya visiwa hivyo.
Katika matukio yote ya toka enzi za ukoloni na kupigania uhuru mpaka kwenda kukomboa nchi kama Uganda na Comoro hapajawahi kuwa na kashfa wala vitendo vyovyote vya uvunjaji wa haki za binadamu , ngono na mengine ya kudhalilisha sasa kwanini leo?
Kwanza tunajua mafanikio ya wanajeshi wa Tanzania huko Kongo, wamefanikiwa kuzima mashabulizi na kusambaratisha makundi mengi ya waasi na kihalifu moja ya kundi hilo ni M23 na sasa hivi ADF ambapo kiongozi wake ameshakamatwa na kurudishwa Uganda ili hatua zichukuliwe hatua za kisheria dhidi yake.
Operesheni hii ya Mashariki ya Congo ilifanya kikosi chetu kupanda mpaka kuwa kwenye namba 27 ya vikosi bora duniani na cha kwanza kwa afrika, haya ni mafanikio makubwa ya JWTZ.
Kumaliza mtandao wa M23 na ADF ina maana kumaliza mtandao wa ulanguzi na wezi wa mali za Congo waliokuwepo katika eneo hilo la mashariki, kwahiyo hawauzi tena silaha, hawapati tena madini kwa bei chee , wanalazimika kulipa kodi na kufanya shuhguli nyingine kwa njia halali. Pia usalama wa ukanda wa mazima umezidi kuimarika marudufu kuliko awali.
Tujue kwamba wanajeshi wa umoja wa mataifa wakiwemo wa Tanzania wanaolinda amani Congo ndio wanaotumia hela nyingi zaidi kwa shughuli hiyo kuliko maeneo mengi duniani, hawa wanatumia dola bilioni 1 kwa mwaka.
Madalali wangetamani wanajeshi wetu watoke Congo ili waletwe wengine wanaoweza kushirikiana nao kuchota fedha hizo na kuendeleza hujuma nyingine dhidi ya Congo, maziwa makuu na Afrika kwa ujumla.
Suala la Wanajeshi wetu kulinda amani Congo, limewafunua, kuwafunza mbinu, matumizi ya silaha , vifaa na kujenga mahusiano mazuri na nchi jirani. Hili pia linaweza kuwa pigo kwa baadhi ya nchi maadui haswa wanaohusika na ulanguzi wa mali za Mashariki mwa Congo .
Hakuna jeshi lolote duniani lenye historia ya kutukuka kama Jeshi la Wananchi wa Tanzania hata kwa kipindi cha miaka 50 tu iliyopita pamoja changamoto zilizopo bado limeendelea kuwa na nidhamu , uadilifu, la kisasa na kujiboresha zaidi katika kila idara.
Pia suala la Rais John Magufuli na Paul Kagame (Rwanda) kukutana na kufanya mazungumzo pamoja na kufungua miundombinu kadhaa naamini litaenda mbali zaidi mpaka kwenye suala la Mashariki ya Congo ambako Rwanda ni mdau mkubwa kama ilivyo Tanzania ili kuendeleza kile ambacho kimefanywa na jeshi letu kwa ushiriano na wadau wengine.
Naomba nimalize kwa kusisitiza kwamba tuliunge mkono jeshi letu tena kwa dhati na kuwapa moyo kwa shuguli hiyo wanayoifanya congo na maeneo mengine duniani . tusife moyo wala kukatishwa tamaa kwa propaganda hizi za wadalali wenye lengo la kulichafua jeshi letu ambalo limejizolea heshima na sifa za kutukuka.
Mwandishi wa makala haya ni msomaji wa Rai, na hayo ni maoni yake binafsi kama raia mwema. 0786 806028.
Chanzo Rai