Propaganda za 'Lowassa vs Sumaye...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Propaganda za 'Lowassa vs Sumaye...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KYALOSANGI, Oct 9, 2012.

 1. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Watanzania ni wepesi sana kutekwa na mijadala ambayo huandaliwa kimkakati na wajanja ili kufikia malengo yao!

  Ni ja
  mbo la kusikitisha kuona huwa tunaingizwa kujadili mambo ambayo yana tija ndogo sana katika jamii yetu !Hebu kumbuka propaganda ya BABU wa Loliondo! napropaganda iliyofanyika kwa ustadi ya kumnadi Kikwete kuwa ni tumaini lilorejea na wajinga wengi wakiwemo wasomi wakalewa na propaganda hiyo na matokeo yake tumeyaona!

  Kuna uwezekano mkubwa kwa mara nyingine tumeanza kuingizwa kwenye mtego tunapoelekea uchaguzi mkuu 2015! Na mara hii yaelekea wamejipanga ipasavyo.

  Ukichunguza kwa makini utaona kuwa kila kukicha vyombo vya habari vimeanza kama kuwaaminisha Watanzania kuwa Wagombea wanaofaa kuwania urais mwaka 2015 ni Lowasa,Sumaye au Membe na Sitta ....Jmbo hili halifanyiki bahati mbaya ni mkakati wa makusudi!

  Hivi katika hali ya kawaida Sumaye na Lowasa katika mazingira ya sasa wanataka wawe viongozi kwa mara nyingine tena; haya ni matusi kwa Watanzania kuwa tumekosa kabisa watu wa kutuongoza!

  Baada ya kuwa Waziri Mkuu kwa kipindi chote kile bada anataka ajaribu tena. LAKINI haya yote yanafanyika baada ya watawala kugundua kuwa wengi wetu uwezo wetu wa kufikiri ni chini ya kiwango ndio maana wanafanya wanavyotaka!

  Hata tulipoambiwa kuwa kuna watu waliiba BOTna wakarudisha hizo fedha lakini hawakukamwatwa badala ya kulia na kuomboleza tukashangila ......ujinga ulioje!?

  Ili kutekeleza propaganda hizi mawakala wa dhambi ya kuwafanya Wa TZ wajinga wakudumu ni vyombo vya habari hususani magazeti .....ndio maana agenda kubwa sasa ya magazeti (baadhi) ni urais kwa LOWASSA na SUMAYE ,,, AU SITTA NA MEMBE!

  Watanzania ni lazima tuamke viongozi na uongozi unaathari kubwa sana katika maisha yetu tulimwamini Nyerere imetosha ...hawa manyang'au wasasa hawaaminiki tena ni lazima tuamke na kujua umuhimu wa kuchagua viongozi.

  Hebu angalia viwaango vya chini kabisa vya kuwaangalia viongozi wetu kwa uafanisi ........eti tunamsifia Magufuli kwa bomoa bomoa katika nchi ambayo haina sera nzuri ya nyumba na makazi ndio maana wananchi maskini tumeamua kujitengenezea sera zetu kwa kuuzina viwanja na kujenga tunataka kwa miakahamsini ....leo anayetubomolea eti naye ni kiongozi bora
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ndiyo siasa yenyewe hiyo......
   
Loading...