PROPAGANDA MFU: Tushike lipi RICHMOND au ESCROW?

PROPAGANDA MFU: Tushike lipi RICHMOND au ESCROW?

munirah

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2015
Posts
551
Reaction score
224
Wapenda mabadiliko!

Tunashuhudia milolongo ya propaganda zenye ubunifu dhaifu zinazoenezwa na watawala dhidi ya upinzani nchini! Taifa linapitia hatua ngumu na hata kuelekea kukosa dira kabisa!

Richmond ni kashfa ya ufisadi iliyopelekea Mh. ENL kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008! Hii ni kashfa ambayo haitafutika mioyoni mwetu kwa urahisi hata punje!

Kumekuwepo na sintofahamu (conspiracy) kuhusu sakata hili japo waliojiwajibisha walifanya hivyo na kukaa pembeni!

Kwa miaka takribani minane Taifa linaingia hasara ya mabilioni ya pesa kuilipa dada wa kampuni ya RICHMOND aitwaye DOWANS!

Tuliyeaminishwa ndio muhusika mkuu (ENL) akatoa ufafanuzi kwa ufupi kuwa hakuhusika moja kwa moja ila alipokea amri kutoka kinachoitwa MAMLAKA ZA JUU ambazo mpaka sasa mamlaka hizo hazijakanusha kuhusika kwake na hakuna aliyechukuliwa hatua za kinidhamu ya utumishi wa umma hadi leo hii!

WATANZANIA TUNASAHAUM APEMA MNO!

Hayo yalitokea mnamo mwaka 2008! Lakini bado haikukuisha KASHFA katika unyeti wa serikali! Tumeshuhudia kashfa nyingi sana kama EPA, TOKOMEZA, UUZWAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI, UTOROSHAJI WA VIUMBE PORI (TWIGA na KOBE) na nyingine ambazo kuzitaja hapa utakuwa mlolongo mrefu!

Katika zote tajwa hapo juu babalao ni ESCROW ACCOUNT!

Kwanini ESCROW ni babalao?

Anyway lazima tujue ukweli na hasa kwa kupima kwa ubichi wa kashfa hizi mbili kubwa!

ESCROW ilitolewa maamuzi na hata kufikia kusafishwa kwa baadhi ya makada wa chama tawala kuwa muamala ule ulikuwa safi ilhali kuna wachafu wengi

Tunashuhudia baadhi ya watu waliochota pesa kina (Chenge......Tibaijuka.....nk) wakipeta tena katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu oktoba 2015 licha ya kwamba hata baadhi ya makada wa chama tawala kutamka bungeni kuwa pesa zile ni za umma na ikafikia pahala Mwanasheria mkuu wa SJM, Waziri wa nishati na madini na Waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi kujiuzulu kwa aibu kubwa! Ingawa kulikuwa na shinikizo la Waziri mkuu PINDA kujiuzulu lakini haikuwa hivyo hatimaye akaendelea kuwa WM ilhali tayari mawaziri 3 walijiuzulu!

HALI ILIVYO SASA

Propaganda mfu zinasambazwa kumlaumu ENL kuwa ni fisadi papa ( Nashindwa kuelewa) nafasi alokuwa nayo serikali ya WM ilishindwa nini kumshughulikia akiwa mwana CCM badala yake mnapiga kalele majukwaani wakati fisadi huyo akiwajibu pelekeni ushahidi mahakamani!

MY TAKE

Kama kweli tumekosa sera za kuwaeleza wananchi tukakomalia siasa za USWAZI majungu Umbe Fitna uzandiki na Ukapuku....ni kwanini basi tunaongelea RICHMOND pekee ilhali ni ya zamani kuliko ESCROW ambayo hatujui hatma ya waliokomba pesa STANBIC BANK?

Kama tumeamua siasa za mitaani basi tuongelee ufisadi wote uliotokea hata enzi za ukoloni ili kujiaminisha kuwa tutapewa kura!

CCM ina timu ya watu 30 na zaidi ambao wote wakipanda jukwaani wanaelezea RICHMOND ambayo hata wanaomuita muhusika kawaambia hakuhusika bali mamlaka za juu....wote wamesahau agenda ya ufisadi mbichi kabisa uliowafanya mawaziri watatu kujiuzulu na wanang'ang'ana na RICHMOND ambayo amejiuzulu mmoja tu!

3 in 1 kweli wacha tuitwe malofa na wapumbavu tukiendelea kuwanyamazia hata kwa haya ambayo hata Mpanju anaona ukweli!

#TukutaneOktoba #UsinizibeMdomo #September1
 
...Lowasa ndio sera ya ccm katika uchaguzi huu...

LOWASA! LOWASA! LOWASA!!!
i) Post nyingi za wanaccm Facebook
zinamzungumzia Lowasa!
ii) Post nyingi za wanaUKAWA Facebook
zinamzungumzia Lowasa!
iii) Post nyingi za wanaACT Facebook
zinamzungumzia Lowasa
iv) Magroup mengi ya siasa whatsaap
yanamzungumzia Lowasa muda mwingi!
v) Twitter tweets nyingi zinamzungumzia
Lowasa
vi) Viongozi wa kubwa wa vyama mbalimbali
vya siasa wameacha kunadi Sera zao
wamekalia Lowasa!
vii) Viongozi wa serikali wameacha ofisi zao
wapo Ngurudoto kuzungumza juu ya Lowasa
viii) Thread nyingi za Jamii forum
zinamzungumzia Lowasa!
ix) Magazeti Mengi habari zenye uzito ni
Lowasa!
x) Redio na tv ni Lowasa
xi) Ukirudi mitaani kila mtu haongei maneno
matatu bila kumtaja Lowasa!
xii) Mtanzania wa leo hapati usingizi mpaka
ataje Lowasa!
xiii) Watu kabla hata ya kupiga mswaki
asubuhi wanaamkia Lowasa!
HITIMISHO!!!
TUKUBALIANE TU KUWA LOWASA NI HABARI
YA MJINI!!!!
 
Back
Top Bottom