Kiukweli kuangalia tutorial youtube ili ujifunze programming kuna ukakasi , issue inakuja hivi wafundishaji wengi wanapokuwa wakielezea kitu huwa wanafuta vitu vya mwanzo halafu wanaendelea na vi part vingine, hii inakuwa ngumu kwa unayejifunza kujenga mtiririko mzuri.
Kingine ni kwamba usitegemee kuelewa leicture ya masaa matatu kwa kuangalia tutorial kwani kuna muda unakuwa bored unajikuta una next next.
Mimi njia ninayokushauri tafuta kitabu cha programming chochote labda cha web designing kisome kwa masaa mawili (sio chote ila sehemu ambayo utakuwa umeweza kuielewa ndani ya hayo masaa mawili), baada ya kumaliza fanya zile assignment ambazo zinakuwa in terms of projects ndani ya saa 1½ halafu nusu saa iliyobaki rekebisha code zako ,kwa kuangalia mahitaji ya project na kinachokuwa displayed kwenye web browser yako.