Proffesor Jay amtembelea Diamond ofisini kwake, amfagilia kwa uwekezaji alioufanya na mawazo mapana

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
xDiamond-akiwa-na-rais-wa-WCB-Diamond-Platnumz.jpg.pagespeed.ic.dYCliu6zuf.jpg



Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi za WCB na kujionea uwekezaji uliofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platunmz.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amemsifia Diamond kwa uwekezaji aliyoufanya.

“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu,” alisema Professor.

Aliongeza, “Kwa mfano pale kwa Daimond jana nimeenda nimekuta kuna studio hapo hapo, pamoja na kurecord lakini pia anachumba ambacho amekitengeneza cha kutengeneza photoshoot. Lakini pia ana sehemu ya kufanya editing ya kazi zake na ana watu special ambao amewaajiri kwa ajili ya kazi hizo, hii ni hatua kubwa sana kwa msanii,”.

xBabu-Tale-akiwa-na-Professor-Jay.jpg.pagespeed.ic.MRVQ_ltyIO.jpg
 
Nasikia baada ya ujio chid benz wasafi..pale studio walitoa lile sanamu la kichwa cha mtu wameweka bangi
 
Safi sana, bila shaka angependa kumtembelea mzee wa Ndovu lakini tatizo atamkuta wapi maana jamaa hana ofisi.

Si vema mbunge kwenda Saigoni kwa ajili ya mazungumzo na babu K.
 
Akina Proff haya ma aidia hawakuwa nayo nadhani dogo amepata exposure ya kutosha ndio maana anazidi kutanuka kibiashara...
 
Back
Top Bottom