TANZIA Professor Frank Chiteji afariki

Shwari

JF-Expert Member
Jan 12, 2008
568
330
Professor Frank Chiteji amefariki dunia. Tumetoka mbali pamoja.

Nilifahamiana naye kwa miaka mingi sana tangu mwishoni mwa miaka ya sabini alipokuwa mwanafunzi Michigan State University pamoja na Issa Kaboko Musoke, mwandishi wa habari Daily News na baadaye professor UDSM.

Chiteji na Musoke walikuwa roommates walipokuwa wanafunzi Michigan State nilipokwenda kuwatembelea miaka ile, na baadaye kumtembelea Haidari Amani (later also a professor, UDSM) ambaye pia alikuwa mwanafunzi pale.

Kabla ya kwenda kusoma USSR na USA, Chiteji aliwahi kufanya kazi ofisi ya FRELIMO (Leveraging Alternatives: Early FRELIMO, the Soviet Union, and the Infrastructure of African Political Exile) ambako alikuwa karibu na viongozi wa chama hicho pamoja na makamu wa raisi wa FRELIMO Uria Simango chini ya uongozi wa Dr. Eduardo Mondlane.

Chiteji alianza kufanya kazi pale muda mfupi baada ya FRELIMO kuanzishwa Dar 1962. Mwaka 1963, alikuwa katika jitihada ya kujaribu kupata scholarship kwenda kusoma USA. Mwanzoni, aliwaambia Ubalozi wa Amerika kwamba hataki kwenda kusoma USSR ingawa baadaye alikwenda kule.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Prof.Frank Mathew Chiteji afariki



Leveraging Alternatives: Early FRELIMO, the Soviet Union, and the Infrastructure of African Political Exile

https://www.gettysburgtimes.com/obituaries/article_5a2f89b4-9bc9-11e0-b4ba-001cc4c03286.html
 
Picha tafadhali

Frank Chiteji image.jpg


 
Back
Top Bottom