Professional Consultants Are Required | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Professional Consultants Are Required

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Sanctus Mtsimbe, Feb 28, 2012.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Dear Friends;

  An experienced Local Consulting Company with National and Regional Consulting assignments is looking for Consultants who are experienced to work on different assignments on part-time or contractual basis subject to mutual agreement.

  Currently the Company is looking for Consultants in the following categories:

  1. Consultants in any of the Ten Pillars of "Kilimo Kwanza"
  2. Livestock & Fisheries issues
  3. General Development issues
  4. Environmental issues
  5. Organizational Change
  6. Training (Capacity Building)
  7. Investments & Finance
  8. Project Management
  9. Other General and Specific Consultants (Please seek clarification)

  In case you believe you are a good Consultant in any of the above areas, please PM me for details.

  Kind regards

  Sanctus Mtsimbe

   
 2. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwa taarifa zaidi ni kuwa kuna azimio la Kilimo Kwanza:


  AZIMIO LA KILIMO KWANZA
  *********************************


  KWA KUWA Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilifanya mkutano tarehe 2 na 3 mwezi Juni 2009 jijini Dar es Salaam, kujadili sera na mikakati ya kuleta mapinduzi ya kilimo cha Tanzania pamoja na utekelezaji wake chini ya kaulimbiu ya “KILIMO KWANZA”;


  NA KWA KUWA
  asilimia themanini ya Watanzania hutegemea kilimo kwa ajili ya kuendeleza maisha yao;


  KWA KUTAMBUA KUWA
  changamoto kubwa kwa Tanzania ni kupambana na umaskini na kwamba hili litawezekana hasa kwa kuongeza tija katika kilimo;


  KWA KUZINGATIA KUWA
  Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali za kutosha kwa ajili mazao, mifugo na uvuvi, ambazo kwa sasa matumizi yake yapo chini;


  KWA KUFAHAMU KUWA
  Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kuwa na kiasi kikubwa cha maji kinachoweza kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji pamoja na ufugaji;


  NA KWA KUTAMBUA KUWA
  jitihada za makusudi zimekuwa zikichukuliwa ili kuboresha kilimo bila mafanikio yakuridhisha;
  HIVYO IMEAZIMIWA KWAMBA:

  1. KILIMO KWANZA iwe ndiyo dhana ya kuleta mapinduzi ya kijani kwa lengo la kukifanya kilimo cha Tanzania kuwa cha kisasa na cha kibiashara;
  2. Dhana ya KILIMO KWANZA ijumuishwe kwenye mipango mbalimbali ya Serikali ili kuhakikisha mafanikio ya utekelezaji wake;
  3. Jitihada zifanyike katika kuongeza rasilimali mbalimbali ili kufanikisha utekelezaji wa KILIMO KWANZA;
  4. Sekta binafsi ihamasishwe ili iongeze uwekezaji kulingana na wajibu wake katika utekelezaji wa KILIMO KWANZA; na
  5. Utekelezaji wa KILIMO KWANZA utaongozwa na nguzo kumi zifuatazo:


  I. Utashi wa kisiasa kutoa msukumo wa mapinduzi ya Kilimo.

  II. Kugharamia mapinduzi ya Kilimo

  III. Uboreshaji wa mfumo wa utawala wa kilimo.

  IV. Mabadiliko ya mfumo mkakati katika kilimo.

  V. Upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo.

  VI. Vivutio vya kuchochea uwekezaji katika kilimo.

  VII. Uendelezaji wa viwanda katika kuleta mapinduzi ya kilimo.

  VIII. Sayansi, Teknolojia na Rasilimali Watu katika kuwezesha
  mapinduzi ya kilimo.

  IX. Uendelezaji wa Miundombinu ili kuwezesha mapinduzi ya kilimo.

  X. Uhamasishaji na ushirikishwaji wa Watanzania kuunga mkono na
  kutekeleza
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wote walio ni-PM nitawajibu bila ya shaka.
   
 4. UKWELIWANGU

  UKWELIWANGU Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu
   
 5. j

  jjjjjuma New Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba contacts zako ili nijuwe jinsi ya kuomba.
   
 6. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wote waliotuma PM wameshajibiwa. Plz check your PM.
   
 7. naike

  naike Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Iam a new member here, i can't PM yet. Kindly PM your contacts so i can give you a buzz.
   
Loading...