Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Pengine mchango wa Professa Kabudi kama rafiki wa mahakama ya rufaa kwenye kesi ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila ya mgombea binafsi ndipo nilimjua huyu msomi ni mpinga mabadiliko.
Mbele ya waheshimiwa 7 wakiongozwa na Jaji Mkuu Augustine Ramadhan (Kama alivyokuwa kwenye enzi zake), Kabudi aliwadobosha na hukumu ya India na kuishia kudai katiba yetu haina msingi na bunge linaweza kuinyambulisha litakavyo.
Lengo lake ni Mahakama ya Rufani ihalalishe hoja batili ya kuwa bunge lilikuwa na mamlaka ya kutengua ibara za mgombea binafsi.
Mahakama ilikubaliana naye na kutengua uamuzi wa Mahakama kuu uliompa Mchungaji Mtikila ushindi wa kurudishwa kwa mgombea binafsi.
Msingi mkuu wa katiba yetu ni ujenzi wa taifa la kijamaa na kujitegemea. Sasa zile purukshani zilikuwa za nini hadi kitabu cha Professa Shivji kilibezwa bila sababu za msingi.
Taifa la ujamaa na kujitegemea miguu yake ya kutembelea ni haki za binadamu ambazo mgombea binafsi ni sehemu yake tena nyeti kabisa
Hivi unahitaji kuwa mwanasheria kujua haki za binadamu ndiyo msingi wa katiba yetu?
Kwa lugha nyingine, hivi haki ya kuishi, haki ya kula na kunywa, haki ya kulala n.k kweli Bunge linaweza kuzifuta kwa vile katiba haina misingi ambayo Bunge haina uwezo nao?
Huyu sasa ndiye Waziri wa sheria ambayo historia yake ni kupinga mabadiliko na kutetea dhuluma.
Hata ile katiba ya Warioba ni mfano mwingine wa kukwaza mabadiliko. Ilikuwa kimantiki bandika bandua katiba iliyopo.
Tusitegemee jipya hapo ila blah, blah tupu.
Tusitishwe na makabrasha tupime wahusika michango yao kwenye jamii.