Profesa Shivji ashauri walimu walipwe zaidi ya mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Shivji ashauri walimu walipwe zaidi ya mawaziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwanazuoni maarufu nchini, Profesa Issa Shivji.  Mwanazuoni maarufu nchini, Profesa Issa Shivji, ameishauri serikali iwalipe walimu mishahara mizuri zaidi ya mawaziri kwa kuwa kazi wanayofanya ni ngumu.
  Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa Jukwaa la Wazi la Uchumi wa Afrika lililofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
  Jukwaa hilo liliandaliwa kwa pamoja na mashirika ya ActionAid Tanzania, Oxfam, Forum CC, FemAct, Yuna na Kepa.
  Profesa Shivji alisema elimu inazidi kuporomoka kwa kuwa hakuna jitihada zinazochukuliwa na serikali kuondoa hali hiyo.
  Alisema serikali inaangalia zaidi ongezeko la majengo na idadi ya wanafunzi mashuleni jambo ambalo alisema haliwezi kuinua kiwango cha elimu.
  “Mwalimu akiwa bora na akiwa katika mazingira mazuri ya kufundisha hata akifundishia chini ya mti, wanafunzi watafanya vizuri sana, lakini ukiwa na majengo mazuri mwalimu akawa mbovu ina maana elimu itakayopatikana hapo ni ya kiwango cha chini," alisema.
  Alisema walimu wengi kutokana na hali ngumu wameamua kuachana na hali hiyo na sasa wanafanya shughuli zao za kuwaingizia vipato.
  "Mimi sioni sababu kwanini mwalimu ambaye ni muhimu zaidi ya waziri kwenye jamii, alipwe mshahara kidogo na waziri alipwe mshahara mnono na marupurupu mengi kumzidi mwalimu," alisema.
  Vile vile, Profesa Shivji alisema ingawa Tanzania ni ya pili kwa kuwa na mifugo mingi Afrika, wafugaji wamekuwa hawanufaiki na mifugo yao.
  Alisema wafugaji wamekuwa wakihangaishwa kama vile si raia wa Tanzania kwa maeneo yao kuchukuliwa kiholela akitolea mfano wa Ngorongoro.
  Awali, akifungua mkutano wa jukwaa hilo, Mkurugenzi wa ActionAid Tanzania, Aida Kiangi, alisema inaonekana mkazo mkubwa wa ustawi na ukuaji wa uchumi katika jukwaa hilo la kiuchumi umeelekezwa zaidi kulenga maslahi ya makampuni makubwa dhidi ya Waafrika walio wengi hususani wanawake, wakulima wadogo na wafupaji pamoja na maskini wanaozidi kuongezeka hasa maeneo ya mijini.
  Kiangi alisema kumekuwa na ukuaji wa uchumi kwa nchi za Afrika lakini wanaonufaika na ukuaji wa uchumi huo ni wachache.
  “Tunaweza kujiuliza ni nani anayenufaika zaidi na ukuaji wa uchumi huu," alihoji.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...