PreGE2025 Profesa Muhongo Ang'ara Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 Jimbo la Musoma Vijijini

PreGE2025 Profesa Muhongo Ang'ara Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 Jimbo la Musoma Vijijini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428
WhatsApp Image 2025-05-29 at 16.00.30.jpeg


Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospester Muhongo ametajwa kutekeleza vema aliyoyaahidi jimboni kwake.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanataaluma bobezi ameng'ara kwa namna alivyowatumikia wapiga Kura wake katika kipindi cha miaka mitano inayomalizika.

Utekelezwaji wa ilani ya CCM jimboni Musoma Vijijini umetajwa kuwa wa kitaalamu unaokipa haiba njema Chama cha Mapinduzi kwa Wananchi wa jimbo hilo.

Miradi ya Maji, shule zikijumuisha maabara za masomo ya sayansi, zimempa Mbunge huyo upendo mkubwa miongoni mwa wananchi

Muhongo ambaye Awamu ya Nne mwishoni na Awamu ya tano mwanzoni alikuwa Waziri wa nishati na madini aliyefanya mabadiliko makubwa katika sekta hizo ametajwa kuwa Mbunge aliyetumia wakati mwingine jimboni kwake akishiriki, kusimamia miradi pamoja na kusaidia wananchi wa jimbo hilo katika masuala ya kijamii.

Ili kuweka kumbukumbu, ofisi ya Mbunge huyo, imechapisha vitabu vyenye kuonesha utekelezaji wa ilani ya CCM jimboni humo kwa kipindi cha 20/25.

"Profesa Muhongo ametisha" , ameandika Mwananchi mmoja kwenye ujumbe mfupi akionesha kufurahia kwake kazi nzuri iliyofanywa na Mbunge huyo wa Musoma Vijijini.

Profesa Muhongo aliingia Bungeni mwaka 2015, akachaguliwa kwa kura za kishindo mwaka 2020, utekelezaji wake wa ilani jimboni Musoma Vijijini, umeliweka jimbo hilo kuwa moja ya ngome imara ya Chama hicho katika chaguzi zote.
 
Huyo professa alisema umeme wa maji umepitwa na wakati. Bwawa lisijengwe, huku nchi zilizoendelea kama Canada na china zipo site zinajenga mabwawa mapya.

Alikuwa hataki bwawa lijengwe sababu ya rushwa za makampuni ya gesi.

Professa kama huyu china wananyonga
 
Huyo professa alisema umeme wa maji umepitwa na wakati. Bwawa lisijengwe, huku nchi zilizoendelea kama Canada na china zipo site zinajenga mabwawa mapya.

Alikuwa hataki bwawa lijengwe sababu ya rushwa za makampuni ya gesi.

Professa kama huyu china wananyonga
Prof Muhongo was very right. We didnt need to invest over 7trilion for 2400 Megawatt, already we had invested chunk of money on gas pipe from Mtwara to Dar es salaam, which as we speak we have not utilized even 30% of its capacity.

Best way was to invest more on gas pipe, from Dar es salaam to Tanga via Bagamoyo, then drop it in Horohoro boarder.
Then another pipeline from Dar es salaam to Mwanza and Kigoma along side SGR railway. This way we could have invested on gas powered electrical stations in every region where the pipeline touches, big industries like cement industries in Tanga could have cheaper power options, hence cement prices would go down, it could make more sense for trucking industry to start using more gas compared to Petrol/Diesel, as it is common now for Bajaj and Tax drivers in Dar es salaam, gas is the cheaper option they have.

One of the generational blunder that we had under Magufuli term was to abandon gas plans. It will take years to pay those depts while we had other cheaper options.
 
Back
Top Bottom