Profesa Mbarawa awashangaza TanRoads kukosa Resident Engineer wa Miradi na kutegemea Waethiopia. Aangiza Watanzania kupikwa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,863
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa amewashangaa TanRoads Kukosa Resident Engineers ambao husimamia miradi Mikubwa ya ujenzi badala yake TanRoads wamekuwa wakitegemea Kuajiri Waethiopia kwenye Kazi hiyo..

Resident Engineers huliowa Dola 10,000 Kwa mwezi (zaidi ya mil.22) ambazo zingeenda Kwa Watanzania ila Kwa kuwa hakuna Mainjinia wenye sifa Wageni hulazimika kuajiriwa..

Waziri Mbarawa ameiagiza TanRoads kuanza Mchakato wa kuandaa wahandisi hao wa Kitanzania Ili Waanze kusimamia miradi..

My Take
Kama Ma Engineers wa Miradi ya Barabara hawapo,Ni Haki Bandari wapewe Waarabu maana Hii Nchi Kila kitu tumeshindwa..
 
Hili jambo hata mimi nashangaa sanaaaa tatizo tuwe na masomo ya ujenzi nchi.

Tenda apewe mzawa kwanza huu ndio uzalendo halisi.
Tatizo sio uzawa,uwezo mbao? Babu yenu hajutaka kuwasomeaha akawa anasaidia Nchi zingine 😂😂😂
 
Mbarawa mbona kama kuna ujumbe ana jaribu kuutuma, anataka kujustify wazo lake la Kukodisha bandari kwa kisingizo kuwa Tanzania hatuna wataalam wala Technology ya Kuendesha bandari Kisasa?
 
Mbona kwenye bandari hataki wa TZ wapikwe waendeshe bandari yao kwa ufanisi??
Anashangaza sana afu issue ya bandari mi naona Watalawala wenyewe wamekuwa wakiingilia sana kisiasa kupelekea mpaka compliance Kuwa hafifu kama kipindi kile cha mwenda zake kuna mstaafu alitaka kupitisha Vitu vyake Bure kwa vile tu aliwahi ku hold higher position uko serikalini, Autonomy kwenye mashirika yetu italeta sana ufanisi ila kuyatumia kwa ajili ya Political gain haitatufikisha popote, Leo ngoja DP world aje uone hata mambo fulani ya ovyo yataondoka bandarini nidhamu itakuwepo ila akiwekwa mzawa kila mtu atataka kuvuna mtaji wa kisiasa apo
 
Wapo madogo wengi tu wana uwezo.Hawajataka..hizo si 10%+ 10%+10%
Asione watu wajinga..ndio U professa wa makaratasi huo.

Nje ya karatasi hawawezi kufikiri.
 
Mbarawa mbona kama kuna ujumbe ana jaribu kuutuma, anataka kujustify wazo lake la Kukodisha bandari kwa kisingizo kuwa Tanzania hatuna wataalam wala Technology ya Kuendesha bandari Kisasa?
Sasa kama mnakodisha hadi Wahandisi wa Barabara bandarini mnaweza kipi?
 
Sasa kama mnakodisha hadi Wahandisi wa Barabara bandarini mnaweza kipi?
Mkuu sina data sana za Tanroad ila pia nachelea Kumuanini Mbarawa katika hili
Kuna mtu aliwahi kushauri vyema sana umu akisema Pamoja na mtu kuwa PhD holder anaweza kukosa exposure za mambo mengi tu
 
Anashangaza sana afu issue ya bandari mi naona Watalawala wenyewe wamekuwa wakiingilia sana kisiasa kupelekea mpaka compliance Kuwa hafifu kama kipindi kile cha mwenda zake kuna mstaafu alitaka kupitisha Vitu vyake Bure kwa vile tu aliwahi ku hold higher position uko serikalini, Autonomy kwenye mashirika yetu italeta sana ufanisi ila kuyatumia kwa ajili ya Political gain haitatufikisha popote, Leo ngoja DP world aje uone hata mambo fulani ya ovyo yataondoka bandarini nidhamu itakuwepo ila akiwekwa mzawa kila mtu atataka kuvuna mtaji wa kisiasa apo
Nasema hivi huo ujinga unafanyika Kwa sababu ni Mali ya Umma,ikiwa privately operated hakuna huo ujinga na ndio maana kelele ziko nyingi maana waliozoea vya bule wanaona kitumbua kinaenda kuingia mchanga.
 
Wapo madogo wengi tu wana uwezo.Hawajataka..hizo si 10%+ 10%+10%
Asione watu wajinga..ndio U professa wa makaratasi huo.

Nje ya karatasi hawawezi kufikiri.
Acha uongo wewe,Kwa hiyo Watzn wote hawawezi kutoa 10%? Harafu TanRoads wafanye hivyo Nchi nzima kwani hawaogopi?
 
Mbarawa huyu huyu au mwingine?
Yeye anayeleta waarabu wasimamie bandari wakati kila mwaka vyuo vyetu vinazalisha wasomi?
 
Tukumbuke yale wakati nchi Ina heshima na adabu,CEO wa THA alikua A Janguo ,elimu yake ilikuwa ya kawaida ILA bandari yetu ilisimama vema, because kulikua na nidhamu kutoka juu hadi chini,....samaki anaanza kuoza kichwa
 
www.facebook.com/watch/?v=1474260993389820
Hivi hawa wenzetu Rwanda, barabara zao huwa zinajengwa na wataalamu wa sayari gani? kati ya nchi barani Afrika zenye miundombinu ya barabara za viwango Rwanda ni mojawapo. Barabara zina kingo imara na zote zina alama zote za barabarani na kutunza vizuri.....Hivi sisi na TANROAD/TARURA tunakwama wapi?
Kama hatuna uwezo wa kujenga wenyewe barabara bora, kwa nini mkandarasi tunayemchagua wenyewe anakuja kutujengea barabara za hovyo na bado tunazipokea tena kwa shangwe na vigeregere?... 🤔
 
Back
Top Bottom