Profesa Lipumba ataka serikali ikimbiwe kwa unajimu


Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,579
Likes
39,004
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,579 39,004 280
CHAMA cha CUF kimewataka Watanzania kuiogopa serikali inayoendesha kazi zake kwa kuwatumia wanajimu wanaotishia kufa watu.

Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kiwalani Jijini Dar es Salaam ambapo alisisitiza kwamba serikali ikifikia kiwango cha mambo yake kuendeshwa kwa unajimu ni dalili za wazi kwamba maji yameifika shingoni.

Profesa Lipumba alisema hayo kufuatia Sheikh Yahya Hussein kutangaza utabiri wake hivi karibuni kwamba mwana CCM atakayechukua fomu kuwania urais atafariki dunia ghafla.

Alisema Sheikh Yahya aliwatisha wana CCM ili wasichukue fomu za kuwania Urais uchaguzi wa mwaka huu kupingana na Rais Kikwete kwa kuwapandikiza hofu kuwa watakaompinga Kikwete watakufa kifo cha ghafla.

"Niliposikia kauli ya Sheikh wangu huyu, nilidhani uzee unamjia vibaya, lakini niliposikia tena msisitizo kutoka kwa msemaji wa Ikulu akisisitiza jambo hili, ndio nikajua kuwa kumbe Sheikh Yahya alitumwa na CCM. Ukiona Ikulu imeanza kuendeshwa na wanajimu tambua kuwa maji yamefika shingoni," alisema Profesa Lipumba.

Alisema ni fedheha kwa serikali kuwashirikisha wanajimu wanaotishia kufa watu na kwamba yeye anaamini kwamba kiongozi yeyote anawekwa na Mwenyezi Mungu kama akiwa na njema kwa binadamu na nchi yake.

Akizungumzia sualam la vita vya ufisadi vinavyodaiwa kuendeshwa na baadhi ya wana CCM , Lipumba alikinanga Chama hicho akifafanua kwamba ndani ya chama hicho , hakuna wapambanaji wa ufisadi bali kuna mapapa na manyangumi wa ufisadi pekee.

Alitoa mfano wa jinsi jinsi Bunge lilivyomaliza sakata la kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development (LLC), na jinsi serikali ya CCM inavyoichukulia kashfa ya ubadhilifu wa fedha katika manunuzi ya rada.

"Kwa namna suala la Richimond lilivyomalizwa bungeni, limeonyesha wazi kuwa katika serikali ya CCM, hakuna makamanda wa ufisadi bali kuna mapapa na manyangumi wa ufisadi, wanaojifanya makamanda wa ufisadi. Wote wanagombea maslahi binafsi tu," alisema Lipumba.

Kuhusu suala la rada alisema "Hivi wewe kama umetapeliwa na mtu akakuambia amempata tapeli wako, utasema unasubiri taarifa rasmi?, Serikali haitaki kulichukulia suala hili kwa uzito kwa sababu, haitaki tujue kila mmoja alipata shilingi ngapi katika mgao wa fedha hizo,".
Profesa Lipumba pia aligusia safari za Rais Kikwete kwa kusema"Kiongozi wa nchi masikini kama Tanzania kama hajatulia hawezi hata siku moja kuiletea nchi maendeleo, kiongozi wa nchi kama hii lazima uwe mtu wa kujisomea, mtu uliyetulia na unayeshaurika," alisema Lipumba.
 

Forum statistics

Threads 1,251,904
Members 481,940
Posts 29,789,806