Profesa J : Kila la Kheri Yanga..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa J : Kila la Kheri Yanga..!

Discussion in 'Sports' started by KIM KARDASH, Feb 18, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  MSANII wa muziki wa bongo fleva nchini Joseph Haule 'Prof J', amewataka Watanzania kuweka utaifa mbele kwa kuishangilia Yanga katika mchezo wake na Zamelek utakaopigwa Februari leo jioni.
  J alisema siku hiyo Watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi huku wakiungana kwa pamoja kutoa sapoti kwa wachezaji wa Yanga kwa kuwa wanaiwakilisha Taifa.
  "Mimi ni mmoja wa mashabiki wa Simba lakini siku hiyo nitatoa sapoti kwa timu ya nyumbani Yanga kwani utaifa ni muhimu kuliko kitu kingine"alisema Prof J
  Prof. J alisema kwa kufanya hivyo itakuwa ni hatua moja mbele katika kufanya mapinduzi ya maendeleo ya mchezo huo unaopendwa na wengi hapa nchini.
  Alisema ushabiki wa kuzizomea timu za hapa nyumbani zinapocheza na wageni hausaidii kuinua kiwango cha soka na kuliletea Taifa mafanikio bali unazindi kurudisha nyuma mafanikio yanayotarajiwa.
  Prof J alisema Watanzania ni muhimu wakaweka utaifa mbele kwa kuzishangilia timu zao kwa kuwa kila timu inaposhinda ni taifa ndilo linalopata heshima na kutambulika katika mchezo huo duniani.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  poleni yanga leo mtafungwa goli chache tu kama 3 tu sababu ni kwenu..
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hapa hakuna haja ya utaifa sababu hivi ni vilabu na sio timu za taifa zinacheza..
   
Loading...