" Haitoshi kabisa kulifahamu jambo. Kuambiwa ni habari tu, unaambiwa na unafahamu, unajua kwamba tukio Fulani limetokea. Gumu zaidi ni kuelewa mantiki ya hilo jambo, na hata baada ya kufikiria na kulifahamu, ugumu mwingine huja pale ambapo inabidi ulieleze lieleweke na maelezo yakajitosheleza yenyewe na kumfanya kila asikilizaye kuridhika kwamba jambo linaeleweka. Haitoshi wewe kulielewa, bali na wewe kulielezea na mtu mwingine akaelewa. Hapa umuhimu wa kufikiria unachukua nafasi ya pekee. Hii ndio maana ya mawasilino." – Profesa Chachage Seithy Chachage ( Makuadi Wa Soko Hurua, ukurasa 117)
Naam, ndugu yetu Chachage anatutaka pia tufikiri kwa bidii. Na kimsingi anachosema Chachage inahusu pia dhana nzima ya maarifa. Maana, ukiweza kuelewa ulichojifunza na ukaweza kumwelezea mtu mwingine akakuelewa, basi, kwako hayo uliyoyaelezea yakaeleweka ni maarifa uliyoyapata.
Maggid Mjengwa
Iringa,
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio