Profesa Baregu azidi kumshukia Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Baregu azidi kumshukia Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Asha Bani

  MHADHIRI mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine, Profesa Mwesiga Baregu, na wanaharakati wengine wamemjia juu Rais Jakaya Kikwete wakimtaka kujiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia utendaji wa serikali yake.
  Kauli ya wanaharakati hao imekuja siku moja baada ya Kikwete kuwashukia Mawaziri, Makatibu wakuu wa wizara na watendaji wa serikali kutotumia nafasi zao vibaya kwa kujishirikisha katika vitendo vya rushwa na ubabe wakati wa semina elekezi ya siku nne inayofanyika mkoani Dodoma.
  Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima Jumatano jana, Profesa Baregu alisemakauli ya rais Kikwete, inashangaza kwa sababu watendaji anaowashutumu aliwachagua mwenyewe hivyo badala ya kuwataka kuachia ngazi aanze kujiondoa yeye ili ufanyike uchaguzi mkuu mwingine.
  Profesa Baregu ambaye ni Mjumbe Kamati Kuu Taifa ya Chama cha Demekorasia na Maendeleo (CHADEMA) alisema maneno hayo ni dalili ya kushindwa kuongoza nchi kutokana na kuwa na watendaji wabovu hivyo kujitokeza kwake kwenye vyombo vya habari na kuwashukia ni kutaka aonewe huruma na wananchi.
  "Kutokana na hili sitomuunga mkono hata kidogo na namshauri kuvunja baraza la mawaziri kama halifanyi vyema au mwenyewe kujiuzulu kwa kuwa ana kila dalili ya kushindwa kuwaongoza watendaji wake," alisema Profesa Baregu.
  Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro, alisema ikiwa Kikwete anaona watendaji wake hawafanyi kazi awaengue na kuwachagua wengine atakaoona ni wachapakazi. Alisema maneno ya rais Kikwete yanaonyesha kutaka kujikosha kwa wananchi kwa kuwa tayari ana ombwe la uongozi kwa kuwa wananchi wana matatizo mengi ikiwemo ukosefu wa huduma ya afya, maji na mengine. Naye mwananchi Sylivester Nyamuhanga alisema kuwa kwa sasa Rais hakutakiwa kufanya semina hiyo elekezi kwa kuwa alishakagua wizara na kilichobakia ni mawaziri kufanya utekelezaji.
   
 2. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  kulikuwa na sababu gani kwa presida kutembelea wizara mbalimbali na kutoa maelekezo kama alikuwa na mpango wa kuwakutanisha mawazir na makatibu kuwaeleza jambo lile lile? jk hakuwa na haja yoyote ya kuchoma fedha za walipakodi kwani hata ile semina elekezi ya ngurudoto haikuzaa matunda yoyote . hali kadhalika kwa hili pia itakuwa kama kutwnaga maji kwenye kinu.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mtu yeyote mwenye akili anajua huyo Presidaa hamnazo!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kikwete baada ya kufungua hiyo semina elekezi mara mmoja wa mawaziri wake anatoka na kuanza kuchochea wananchi kuzomea upinzani badala ya kujipanga kutekeleza aliyoelekezwa na mkuu wake. Labda yaho ndiyo aliyoelekezwa. Nakubaliana nawe huku ni kutwanga maji kwenye kinu.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huyu rais kila siku ananishangaza na mambo anayofanya, sijui ana tatizo gani!
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Prezidaa ni kichaa..hashauriki!!
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Raisi anatakiwa kupata ripoti kila siku ya mambo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Mfano Obama. Sasa nilitarajia raisi ayajue matatizo yote na kuwaeleze mawaziri na makatibu wakuu jinsi ya kuyatatua. Lakini nashangaa eti kuna semina elekezi ya kujadili matatizo mbalimbali tena kwa mawaziri. Duh. Kazi ipo.
   
 8. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili ni janga baya kuliko yote..janga la uongozi ambalo ni man made.. ni la kujitakia, tofauti na majanga ya asili kama yaliyotokea Japan au yanayoendelea America!
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii semina elekezi na zile ziara za kila wizara zina malengo tofauti? Hapa sijui kama tutafika?
   
 10. O

  Oldarasu Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Niaminivyo mimi Profesa Baregu hajamshukia Mheshimiwa Rais. Alichofanya Baregu ni kuonyesha hisia zake za kweli jinsi Rais anavyoonyesha udhaifu mkubwa katika uongozi. Haiwezekani Mkuu wa nchi kulalamika kama alivyofanya Mheshimiwa Kikwete. Kwangu mimi kuitishwa kwa Semina Elekezi ni matumizi mabaya ya fedha za umma, kwani semina haitawasaidia mawaziri chochote maana kama hawawezi kazi ukweli ni kwamba semina hiyo haitawasaidia chochote. Pili, Mheshimiwa Rais kutumia muda wote huo kuwasema mawaziri aliowachagua yeye mwenyewe ni kuanika udhaifu wake binafsi. Kwangu alionekana kama mtoto ambaye amepigwa na kwa sababu hana cha kufanya anabaki analia na kunung'unika tu! Mheshimiwa Kikwete amejua wazi hana watu wanaomsaidia sasa amewashitaki wateule wake kwa wananchi yaani ni kama kuwaambia wananchi "jamani tatizo siyo mimi ni hawa." Anasahau kwamba tatizo ni yeye kwa sababu ndiye aliyewachagua na wengi wao ni maswahiba wake! Kwa hiyo, asilalamike aingie kazini. Awaondoe mawaziri wabovu aweke watu wanaoweza kuchapa kazi. Mbona wapo tu!!! Ama hawaoni kwa kuwa watu hao wazuri siyo maswahiba wake? Asante Profesa Baregu endelea kusema wala usichoke. Mabadiliko hayako mbali
   
 11. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sipendi kutoa tusi kwa Rais wangu kwakuwa ni rais wa nchi kwa sasa aliyetangazwa. Ila kwa mshangao mkubwa kabisa nashindwa kuelewa hii semina elekezi ni yanini ? Kwa kumbukumbu zangu yeye alishapita katika wizara mbali mbali na kutoa mwongozo huko hii ni semina ya kupeana fedha za walipa kodi tu. Naomba watawala sasa muamke kwani tanzania ya sasa sio ya miaka 47 iliyopita. ni ya watanzania wanao pambanua mambo sio kwa kupitia chadema la, wanaona na wanawasoma jamani na tunajua tunakokwenda sasa siko tumepotezwa
   
Loading...