Profesa Amechelewa.. !

Profesa Amechelewa.. !

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,

Profesa Mwesiga Baregu amenukuliwa na gazeti Mwananchi akisema;
"Bila kuweka utashi wa kujenga taifa moja, Bunge lijalo linaweza kutawaliwa na vituko. Iwapo wajumbe watakwenda kwenye Bunge la Katiba huku wakiwa na ushabiki wa vyama vyao mimi naona kutakuwa na vituko vikubwa.Tunapaswa kutambua kwamba tunakwenda kutengeneza Katiba ya Taifa na siyo kwa kuegemea masilahi ya kundi fulani” - Profesa Baregu ( Mwananchi, Februari 7, 2014)

Na kabla sijaichambua kauli ya Profesa, ngoja hapa nimkumbushe Profesa juu ya mwanafalsafa wa Kiyunani, Ptolemy, huyu alipata kuandika: ”Ex Africa simper aliquid novi". Maana yake: "Kila kukicha kitazuka kioja kingine Afrika."

Mimi nadhani Profesa amechelewa katika kauli yake hii, maana, anachofikiri Profesa kuwa kitatokea, tayari ishara zilishaonekana, na sasa tumeanza kukiona. Na Rais Kikwete kule Mbeya majuzi ndiye aliyeweka bayana kabisa, kuwa tatizo naye ameliona, kuwa kwenye Bunge la Katiba yumkini malumbano hayatakuwa ya hoja bali hata kupimana ubavu na kwa sura za rangi za vyama.

Profesa wangu Baregu, hivyo vitakavyotokea si vituko tu, ni vioja kama anavyosema Mwanafalsafa Ptolemy. Na tujiandae na burudani za aibu kwa taifa.

Maana, nilishapata kuandika, kuwa safari nyingi za Mwafrika ni za bure tu. Tusipotanguliza busara na hekima, tutambue, kuwa kazi yote hii ya akina Jaji Warioba na wenzake nayo itakuwa ni ya bure tu. Tutakuwa tumechoma mabilioni ya fedha kwa jambo litakalohitimishwa na kutugawa zaidi kuliko kutujenga kama taifa. Maana, sisi ni wabinafsi kuliko. Hatutangulizi maslahi ya nchi bali yetu binafsi, ya makundi yetu na vyama vyetu.

Na zaidi ya miaka 15 iliyopita niliandika, kuwa Tanzania ina vyote kasoro Watanzania. Tusipowafanya wajumbe wengi ndani ya Bunge la Katiba wafikiri kama Watanzania, basi, tutaishia kuipata Katiba ya Vyama Vya Siasa na si ya Watanzania.

Maana, wanachotaka Watanzania walio wengi tayari kinafahamika kupitia rasimu ya pili ya Mabadiliko ya Katiba. Lakini, hofu iliyopo ni kutokea kwa baadhi ya Watanzania wenzetu, kupitia Bunge la Katiba, kuyateka matakwa ya umma na kupandikiza matakwa ya vyama na makundi.

Maana, kupitia Tume ya Warioba Wananchi walishausonga ugali wao na ukaiva. Lakini, kuna waliojipanga kwa kuanika kimea cha mtama, tayari kuwakorogea Wananchi togwa ili wanywe, walewe na kuendelea kulala usingizi. Wakiamka watayakuta yale yale. Na yawe ni mapambano, ya uwepo wa Katiba ya Kusongwa na Wananchi, kama ugali, na kuipinga kwa hoja, Katiba ya kukorogwa na wanasiasa, kama togwa.

Itakumbukwa, mwanzoni kabisa mwa mchakato wa Katiba, Profesa Kabudi alipata kusema, ” What we are doing is Constutional building and not Constutional making”. Kwamba tunachokifanya ni Ujenzi wa Katiba na si Kutengeneza Katiba.

Na katika alichokisema Profesa Kabudi swali lilikuja,je; “ Ni kina nani wanaostahili kushirikishwa kwenye maandalizi ya ujenzi huo? Swali lingine, ni maoni yepi yanayotakiwa kupewa kipaumbele, ya wananchi au wanasiasa?

Nahofia, kuwa hatufikiri kuhusu nchi yetu tuliyozaliwa na hatma yake. Tunajifikiria sisi , makundi na vyama vyetu. Vyote vya kupita, wakati nchi itabaki.

Maana, kutengeneza Katiba ya nchi ni sawa na kulima shamba la pamoja. Na kwanini basi wenye kulima shamba moja wagombanie majembe? Hakika, huo utakuwa ni uwendawazimu, ni kwa vile, watakachopanda na kuvuna ni cha faida yao wote.

Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
Iringa.
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
 
wanaotaka kuharibu katiba ni magamba,wananchi wametoa maoni wanataka serikali tatu,maccm yanapinga..
 
maggid acha unafiq
Wewe ulikuwa wapi kutoa uchambuI wako hadi umsikie Proff Baregu na wewe ndo uje on top.
Mimi nasema wewe ndo umechelewa zaidi au pengine bado uko usingizini...
Kalaghabao..
 
Last edited by a moderator:
...ilikuwa haitoshi JK kuwaambia watu wake wajiandae kisaikolojia,alichotakiwa kufanya ni kuwatafutia daktari ama kuwapeleka India wakapatiwe matibabu ya akili ili waingie kwenye bunge la katiba wakiwa ni watu wenyeakili timamu...
 
Ndugu zangu,

Profesa Mwesiga Baregu amenukuliwa na gazeti Mwananchi akisema;
"Bila kuweka utashi wa kujenga taifa moja, Bunge lijalo linaweza kutawaliwa na vituko. Iwapo wajumbe watakwenda kwenye Bunge la Katiba huku wakiwa na ushabiki wa vyama vyao mimi naona kutakuwa na vituko vikubwa.Tunapaswa kutambua kwamba tunakwenda kutengeneza Katiba ya Taifa na siyo kwa kuegemea masilahi ya kundi fulani” - Profesa Baregu ( Mwananchi, Februari 7, 2014)

Na kabla sijaichambua kauli ya Profesa, ngoja hapa nimkumbushe Profesa juu ya mwanafalsafa wa Kiyunani, Ptolemy, huyu alipata kuandika: ”Ex Africa simper aliquid novi". Maana yake: "Kila kukicha kitazuka kioja kingine Afrika."

Mimi nadhani Profesa amechelewa katika kauli yake hii, maana, anachofikiri Profesa kuwa kitatokea, tayari ishara zilishaonekana, na sasa tumeanza kukiona. Na Rais Kikwete kule Mbeya majuzi ndiye aliyeweka bayana kabisa, kuwa tatizo naye ameliona, kuwa kwenye Bunge la Katiba yumkini malumbano hayatakuwa ya hoja bali hata kupimana ubavu na kwa sura za rangi za vyama.

Profesa wangu Baregu, hivyo vitakavyotokea si vituko tu, ni vioja kama anavyosema Mwanafalsafa Ptolemy. Na tujiandae na burudani za aibu kwa taifa.

Maana, nilishapata kuandika, kuwa safari nyingi za Mwafrika ni za bure tu. Tusipotanguliza busara na hekima, tutambue, kuwa kazi yote hii ya akina Jaji Warioba na wenzake nayo itakuwa ni ya bure tu. Tutakuwa tumechoma mabilioni ya fedha kwa jambo litakalohitimishwa na kutugawa zaidi kuliko kutujenga kama taifa. Maana, sisi ni wabinafsi kuliko. Hatutangulizi maslahi ya nchi bali yetu binafsi, ya makundi yetu na vyama vyetu.

Na zaidi ya miaka 15 iliyopita niliandika, kuwa Tanzania ina vyote kasoro Watanzania. Tusipowafanya wajumbe wengi ndani ya Bunge la Katiba wafikiri kama Watanzania, basi, tutaishia kuipata Katiba ya Vyama Vya Siasa na si ya Watanzania.

Maana, wanachotaka Watanzania walio wengi tayari kinafahamika kupitia rasimu ya pili ya Mabadiliko ya Katiba. Lakini, hofu iliyopo ni kutokea kwa baadhi ya Watanzania wenzetu, kupitia Bunge la Katiba, kuyateka matakwa ya umma na kupandikiza matakwa ya vyama na makundi.

Maana, kupitia Tume ya Warioba Wananchi walishausonga ugali wao na ukaiva. Lakini, kuna waliojipanga kwa kuanika kimea cha mtama, tayari kuwakorogea Wananchi togwa ili wanywe, walewe na kuendelea kulala usingizi. Wakiamka watayakuta yale yale. Na yawe ni mapambano, ya uwepo wa Katiba ya Kusongwa na Wananchi, kama ugali, na kuipinga kwa hoja, Katiba ya kukorogwa na wanasiasa, kama togwa.

Itakumbukwa, mwanzoni kabisa mwa mchakato wa Katiba, Profesa Kabudi alipata kusema, ” What we are doing is Constutional building and not Constutional making”. Kwamba tunachokifanya ni Ujenzi wa Katiba na si Kutengeneza Katiba.

Na katika alichokisema Profesa Kabudi swali lilikuja,je; “ Ni kina nani wanaostahili kushirikishwa kwenye maandalizi ya ujenzi huo? Swali lingine, ni maoni yepi yanayotakiwa kupewa kipaumbele, ya wananchi au wanasiasa?

Nahofia, kuwa hatufikiri kuhusu nchi yetu tuliyozaliwa na hatma yake. Tunajifikiria sisi , makundi na vyama vyetu. Vyote vya kupita, wakati nchi itabaki.

Maana, kutengeneza Katiba ya nchi ni sawa na kulima shamba la pamoja. Na kwanini basi wenye kulima shamba moja wagombanie majembe? Hakika, huo utakuwa ni uwendawazimu, ni kwa vile, watakachopanda na kuvuna ni cha faida yao wote.

Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
0754 678 252
Iringa.
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio

Ombwe la uongozi wa juu (rais & co) tulilonalo ndio linasababisha yote. U Na zaidi ukiniuliza mimi kama kweli Kikwete anataka katiba mpya iwe tayari kutumika 2015 nitakuambia HAPANA! Anafanya tu usanii yeye na swahiba yake ...Lowassa
 
Hata kwenye hotuba ya Rais jana, aliweka wazi kuwa "msingi wa ujenzi wa KATIBA mpya usilenge kunufaisha itikadi/kundi fulani". KATIBA lazima iwe na sura ya KITAIFA. Ninaimani hata kama alikuwa akimaanisha haya, bado hawa wawakilishi wetu wanaweza kusimamia kwenye manufaa ya makundi na kutoridhia mijadala yenye kuleta muafaka. Kama itafikia vipengele fulani kuamuliwa kwa KURA, basi ni wazi hiyo KATIBA haitakuwa na manufaa halisi kwa TAIFA. Ni vizuri wajumbe wabadilike mitazamo yao, waende kwenye BUNGE LA KATIBA kuwasilisha hoja na kusikilizana wote kwa kauli moja mpaka kufikia muafaka.

Kitu kingine ninachokiona kitawafanya hawa wanasiasa wetu kuwa na shingo ngumu, ni kuona kama tutaruhusu serikali mbili basi CCM watakuwa wameshinda, ama kama tutakubali serikali tatu, basi CDM itakuwa imeshinda. Hii ndiyo mitazamo inayobidi kuondolewa, tuwasilishe hoja na kuzipembua kwa makini na uhalisi. Tunaomba BUNGE hili liwe wazi/ lirushwe hewani kupitia vyombo vingi vya habari na wananchi tutapata wasaa mzuri pia wa kujielimisha ama kutuma maoni yetu kupitia vyombo vya habari.
 
umesema vema kamanda, shida kubwa ni hii majangiri maccm yawaza jinsi ya kuchakachua katibu kwa maslai ya matumbo yao yenye mimba za ndama na kondoo
 
Leo Maggid umeongea kwa kujenga na maneno yako haya yaweza kuwa kumbukumbu kubwa huko siku za mbeleni
 
ieleweke kwamba hatutakubali maoni ya wananchi kupuuzwa .
 
Katiba ni mali ya watanzania lazima itapatikana kwa neema za mungu siku si nyingi.
 
Ungesema Kikwete ndio kachelewa ningekubali lakini kwa kumtaja Baregu umeharibu kabisa maana nzima ya hoja yako, nasema hivyo kwasababu hii; JK ndie mwenye dhamana kuu ukilinganisha na Baregu, Baregu anabaki kuwa mwananchi kama mwananchi mwingine lakini Kamwe JK hawezi kuwa kama Baregu na hivyo hotuba ya jana ya KIkwete ambayo aligusia the same thing haina mantiki yoyote na kwamba yeye ndio kachelewa.

Kitu kingine, JK haeleweki maana leo hii kasema hivi lakini anaujua ukweli uliomo ndani ya chama chake, anafahamu kabisa mipango yote ya hujuma inayoendeshwa na chama chake yeye kama Mwenyekiti (sio kama Rais), leo akiongea hivi akifika kwenye vikao vyake atauliza ule mkakakti umefikia wapi? kwanini Yeye mwenyewe hatekelezi kile anachokisema? Kwanini akina Asha rose Migiro walisambaza waraka ule kwa email kuhusu mabaraza ya Katiba kipindi kile? ni kweli Mwenyekiti hakuwa- aware au informed juu ya mpango ule hatarishi? Sasa je leo tutaamini vipi maneno yake yale?

naamini swala la kuangalia kuwahi au kuchelewa litazamwe kwa mtazamo wa Raisi/Mwenyekiti wa CCM na sio kwa Baregu ambaye ni Mjumbe tu wa Kamati kuu ya Chadema.......unless otherwise mseme mmeamua kuikubali CHADEMA kuwa matamko yao yako strong na yana uwezo wa ku-influence decision kwenye jamii na kwenye Taifa. hahahahaaaa kumbe nimelewa, jamani pombe hizi, sorry maggid
 
Wewe eli ni wewe ndio unaipenda cdm mimi namimi kama rais asingelikua na nia basi katiba isinge patikana wala mchakato usingelikuwepo na wshauri waliobatika kwenda kwenye bunge la katiba wangalie mustakabali wa nchi yetu na tanganyika yetu maslai ya vyama vyenu sio ya taifa taifa kwanza nyambafu
 
Katiba ni mali ya watanzania lazima itapatikana kwa neema za mungu siku si nyingi.

Wakilazimisha kupitisha matakwa yao kwenye bunge la katiba kwa kutumia wingi wao na sisi tuje tutumie wingi wetu kukataa waliyoyapitisha na hatimaye tuje kuwakataa 2015 kwa kutumia huo huo wingi wetu.
 
Mimi ni mmojawapo wa watu walioona kwamba mchakato wa kupata katiba mpya ulikosewa toka mwazo. Na hii imesababishwa na mchakato wote kuwa chini ya Rais. Ukiiangalia sana mchakato huu ni mihimu lakini ulikuja wakati ambao si muafaka, kwani waliokuwa wakitaka katiba mpya hawakuwa wengi bungeni na wale ambao wako wengi bungeni katiba mpya haikuwa wala hata kwenye ilani yao. Kilichotokea walio wengi maana katiba haikuwa kwenye utashi wao wakaiteka kwani Rais wa nchi alishakubali kutuletea katiba mpya, ikabidi waanze hila kwenye huo mchakato. Tulisikia mengi toka kwa kina Kombani, mwanasheria mkuu, sijui mara wananchi hawataki katiba mpya wanataka maji, umeme nk.

Ngoma sasa iko kwenye makada wa CCM, wao wakipanda majukwaani wanasema wanaotaka serekali tatu ni walafi wa madaraka!! Sasa unajiuliza haya ni maoni ya wananchi lakini makada wa CCM hawakubaliani nayo wanataka maoni ya CCM. Hali hii imepelekea mpaka Jaji Warioba kutoa ufafanuzi wa serekali 3 na gharama zake. Kwa ccm hili ikawa ni tatizo. Ninachokiona ni kwamba JK amejikuta kwenye wakati mgumu haswa kutoka kwenye chama chake kwani huko ndio watu hawakubaliani na mawazo ya wananchi, na yeye anashindwa kuwaambia kwani wao wanamuambia kwanza yeye ndio aliyewaletea balaa la katiba mpya wakati hata kwenye ilani yao haipo. Imebidi sasa JK aitishe baraza la vyama vyote kupata muafaka mapema kabla ya bunge ili kuwaambia wanaccm wenzake kwa kutumuia mgongo wa baraza la vyama ili waelewe alama za nyakati. Lakini haya yote yasingetokea leo iwapo toka mwanzo mchakato ungetoa nafasi sawa kwa watanzania wote na sio wanasiasa kujazwa kwenye bunge la katiba mpya. Ubovu huu ulichangiwa na kulazimisha katiba kuwa chini ya rais wakati rais alitakiwa awe tunda la katiba na si katiba ya rais. Tusipoangalia bado kwenye katiba hii rais anaweza kuwa juu ya sheria matokeo yake ni mfumo huu mbovu wa watu kutojali sheria bali kujali rais anataka nini.
 
Ombwe la uongozi wa juu (rais & co) tulilonalo ndio linasababisha yote. U Na zaidi ukiniuliza mimi kama kweli Kikwete anataka katiba mpya iwe tayari kutumika 2015 nitakuambia HAPANA! Anafanya tu usanii yeye na swahiba yake ...Lowassa

Kwahiyo unataka tuamini kwamba ''Raisi'' Slaa na Chadema wangetupa katiba mpya ndani ya siku 100------kama alivyoahidi kwenye kampeni!
 
Back
Top Bottom