Prof Tibaijuka awaambia wakuu wa shule za sekondari TZ mpango division 5 Utaangamiza Taifa.

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Akifunga mkutano wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania bara uliofanyika kwa muda wa siku 3 mjini Dodoma. Pofesa Anna Tibaijuka alisema serikali ikiendelea na mpango wake wa Division 5 itatoa wataalamu watakao teketeza taifa letu. Aidha amewashauri wakuu wa shule ili vijana wetu waweze kufanya vizuri ni lazima kwanza walimu wenyewe wafundishe wakiwa na matarajio ya kufaulisha kwa kiwango cha daraja la kwanza. Rais wa Umoja huo wa wakuu wa shule za sekondari [TAHOSSA] Ndg. Ndimbo alichaguliwa kumalizia awamu ya pili ya uongozi wake. Tibaijuka aliagiza wakuu wa shule zote za sekondari ambazo mipaka yake hiaijapimwa bila kuomba wawatake maafisa ardhi wa wilaya wakambie shule zao bila kughalamia chochote na Halmashauri itakayokaidi apigiwe simu.

Awali akiongea katika mkutano huo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mtihani wa Taifa Dr. Msome alisema hali ya elimu nchini ni mbaya sana, ukisoma wanayoandika kwenye mitihani ya Taifa kuanzia ile ya darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne, sita na hata chuo kikuu ni uchafu mtupu. Aliwaomba wakuu wa shule kuwasaidia hata walimu wanaoajiriwa wakiwa na shahada elimu namna bora ya kufundisha wanafunzi.
 
Back
Top Bottom