Prof. Tibaijuka atoa onyo kwa wanaopotosha kauli yake ya 'Unavyopanua zaidi watu wanazidi kutamani'

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,942
19,130
Mbunge wa Muleba Anna Tibaijuka ametoa onyo kwa watu wanaopotosha kauli yake na kukata vipande vifupi vya video na kuharibu maana ya aliyokuwa anamaanisha kwa mchango wake bungeni

Amesema kufanya hivyo ni kosa kisheria na watu wanafanya hivyo makusudi ili ujumbe aliokuwa amedhamiria kuufikisha usifike na kuwatupia lawama wapinzani ndio walifanya hivyo na kuwataka watu watafute hotuba yake yote

Amerudia tena anataka umeme upanuliwe na kama neno panua halitumiki tena basi msamiati mwingine utafutwe
 
Kwani uongo? ukipanua zaidi ndivyo watu wengi wanatamani. Baada ya Tanesco kupanua zaidi huduma zao watu wanaotamani kuwa na umeme wanaongezeka.
 
Yaani profesa mzima anatokwa povu kwa kutaniwa kidogo? Kuna hoja gani ya kutolea ufafanuzi hapo? Kikwete aliposema "ukitaka kula lazima uliwe kidogo" watu wakatafsiri kinyume mbona alikaa kimya. Huyu naye akiwa spika tutaona makubwa!.
 
Haya wenye umeme wamwmsikia...
Watapanua ili wengine watamani zaidi nao wawe na umeme!!!
 
Mbunge wa Muleba Anna Tibaijuka ametoa onyo kwa watu wanaopotosha kauli yake na kukata vipande vifupi vya video na kuharibu maana ya aliyokuwa anamaanisha kwa mchango wake bungeni
Amesema kufanya hivyo ni kosa kisheria na watu wanafanya hivyo makusudi ili ujumbe aliokuwa amedhamiria kuufikisha usifike na kuwatupia lawama wapinzani ndio walifanya hivyo na kuwataka watu watafute hotuba yake yote

Amerudia tena anataka umeme upanuliwe na kama neno panua halitumiki tena basi msamiati mwingine utafutwe

Great thinker mom weldone
 
Eeeeeeeee Rwegoshora! N'shomire mpaka Mbwa'ngu ashomire,n'shomire mpaka form six but no course.Wanigambira stupid infront of my wife wewe...hyo ni zalau kwa kweli.
 
Back
Top Bottom