Mapya kuhusu ESCROW, Shule ya Prof Tibaijuka yathibitisha kupokea pesa' in good faith'

Makaura

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
894
195
TAARIFA YA BODI YA WADHAMINI WA JOHA TRUST KWA WAZAZI NA UMMA KUHUSU MCHANGO WA SHS BILIONI 1.617 KUTOKA KWA BW. JAMES RUGEMALIRA WA TAREHE 12 FEBRUARI, 2014

1. Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Barbro Johansson Girls’ Education Trust (JOHA TRUST au BARBRO) inatoa taarifa hii kutokana na utata uliojitokeza kuhusu mchango wa Shs bilioni moja milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,0000/- ) tulioupokea kutoka kwa Bw James Rugemalira wa VIP Engineering and Marketing Limited.

2. Mwanzilishi wa Shirika na Malengo yake: Bodi ya Wadhamini BARBRO inachukua nafasi hii kufafanua kwamba kiongozi wa Waanzilishi wa asasi yetu ni Mhe Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Malengo na madhumuni ya taasisi ya JOHA TRUST ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike kwa kuwafadhili wasichana wenye vipaji lakini watokao katika familia za kipato kidogo kusoma katika shule bora inazoziendesha.

3. Jina la taasisi ya JOHA TRUST linatokana na uamuzi wa wanawake waanzilishi kumpa heshima Hayati Dr. Mama Barbro Johansson (1912-1999) aliyewasili kutoka Sweden mwaka 1946 kama mmisionari na kuanzisha shule ya wasichana ya kati hapo Kashasha Bukoba. Mwaka 1954 alijiunga na Mwalimu Nyerere kupigania uhuru na baadaye kuwa raia wa Tanzania na Mbunge. Mwaka 1964 aliombwa na Mwalimu Nyerere kujitolea kuwa Mwalimu Mkuu wa sekondari ya juu (High School) pekee ya wasichana ya Tabora Girls iliyokuwa imekumbwa na utovu wa nidhamu na kutaka kufungwa. Mama Barbro akafanikiwa sana kuigeuza shule hiyo kiasi kwamba ilipata nishani ya UNESCO mwaka 1967. Mama Barbro ndiye alianzisha elimu ya watu wazima nchini na pia ndiye alimuunganisha Mwalimu Nyerere na wahisani kutoka nchi za Nordic ambazo zilianza ufadhili wake katika Kituo cha Elimu Kibaha na Kituo cha Kilimo, Uyole, Mbeya.

4. Shule za JOHA TRUST na Sura yake: Shirika linamiliki na kuendesha Sekondari mbili nchini. Kwanza ni Sekondari Bingwa ya Barbro iliyopo jijini Dar es Salaam. Ilianzishwa mwaka 2000 ikiwa na wasichana 40 na hivi sasa wapo 632 wote wa bweni katika kidato cha 1 hadi 6. Pili ni Kajumulo Girls’ High School iliyopo Manispaa ya Bukoba. Ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wasichana 31 na hivi sasa wapo 151 katika kidato cha 1, 5 na 6. Jumla shule hizi zina wanafunzi 783 na waliomaliza ni 1,512. Wote isipokuwa 5 walifaulu mitihani na kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Kwa kulingana na uwezo wa mfuko wa ufadhili, wasichana 453 sawa na asilimia 30% ya wanafunzi wamesaidiwa karo. Shule ya Barbro imekuwa miongoni mwa shule kumi bora Tanzania (2010) na kwa wastani inakuwa kati ya shule 50 bora katika mitihani ya taifa. Itambulike kwamba mafanikio haya yanapatikana pamoja na shule kuwa na sera ya kutowafukuza wanafunzi kwa misingi ya ufaulu wa mitihani ili mradi wawe na nidhamu. Falsafa yetu ni kuwahimiza wanafunzi kuweka bidii kadri ya uwezo wao, kujithamini na kujiamini katika maeneo wanayofanya vizuri. Kipa umbele chetu ni maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja kwanza na sifa kwa shule baadaye. Katika hali hii walimu hawana budi kufanya kazi ya ziada.

5. Gharama za Uendeshaji na vyanzo vyake: Tangu ianzishwe JOHA TRUST imetumia gharama ya Shs bilioni thelathini na mbili (Shs 32,267,000,000/-) ambazo zimetokana na karo na michango ya wazazi asilimia 37%; wafadhili wa nje asilimia 35%, wafadhili wa ndani asilimia 7% na mikopo asilimia 21%. Kama taasisi nyingi zinazotoa elimu, JOHA TRUST inakabiliwa na uhaba wa fedha na ujenzi bado kukamilika. Shule inatoa huduma ya elimu bora na haifanyi biashara kama wengi wasioelewa wanavyofikiri. Bila ruzuku na misaada viwango vyake vya juu haviwezekani. Shirika la misaada la Sweden (SIDA ) ambalo limekuwa mfadhili mkubwa limekamilisha ahadi yake ya ufadhili wa miaka 10 (2002-2012) lililopanga kwamba ingelitosha kusimika taasisi ya JOHA TRUST na kuitaka ijitegemee. Hata hivyo SIDA imeacha utekelezaji wa Master Plan ya BARBRO ya mwaka 2004 bado kukamilika. Jambo hili limekuwa changamoto kubwa kwa Bodi kwa sababu katika Master Plan SIDA ilipandisha viwango vya majengo kuwa juu kulingana na sifa na hadhi ya Mama Barbro. Ikihitimisha ufadhili huo, SIDA ilihimiza Bodi kuhamasisha michango ya ndani ili kujenga uendelevu na kukamilisha ujenzi wa Master Plan hiyo.

6. Maombi ya Ufadhili: Kwa kuzingatia ushauri huo wa SIDA, mwaka 2012 Bodi ilimtaka Mwanzilishi (ProfesaTibaijuka) ambaye pia ni Mtafuta Fedha (Fund Raiser) wa JOHA TRUST kuwaomba baadhi ya wafanyabiashara mashuhuri nchini kuunga mkono shughuli za asasi yetu kwa michango. Bwana na Bibi James Rugemalira ni miongoni mwa wafanyabiashara walioombwa mchango huo kwa barua ya tarehe 4 Aprili 2012 kupitia kampuni yao ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited. Hatimaye mapema Februari 2014, bila kutaja ni kiasi gani, Bw. Rugemalira alimjulisha Mwanzilishi kwamba yuko tayari kufanya mchango ulioombwa na kumwagiza kwamba sharti ni yeye Mwanzilishi kufungua account hapo Mkombozi Benki kuupokea mchango huo na kuchukua jukumu la kuufikisha shuleni na kuhakikisha unatumika kama ilivyokusudiwa. Bw Rugemalira alieleza hakutaka kuhangaika kuhamisha fedha kwenda benki nyingine ambapo tayari kulikuwa na akaunti za shule.

7. Mchango wa VIP ulivyopokelewa: Kama alivyotakiwa, Mwanzilishi alifungua account hiyo hapo Benki ya Mkombozi tarehe 3 Februari, 2014 na kuupokea mchango huo wa jumla ya bilioni moja, milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,000/=) kwa niaba ya shule tarehe 12 Februari, 2014 kutoka kwa kampuni ya VIP Engineering and Marketing.

8. Maamuzi ya Bodi: Bodi ya Wadhamini BARBRO ilikaa katika kikao maalum tarehe 13 Februari, 2014 kupokea taarifa ya mchango huo mkubwa kutoka kwa Bw. Rugemalira kupitia kampuni yake ya VIP Engineering. Bodi iliukubali na kuamua mchango huo utumike kulipa sehemu ya deni la shule hapo Bank M ambalo lilikuwa changamoto kubwa. Kwa hiyo Mwanzilishi aliagizwa na Bodi kuhamisha fedha hizo kutoka akaunti yake ya Mkombozi kwenda akaunti ya Bank M kulipia mkopo huo. Hii inafafanua kwa nini fedha zilihama kwa haraka kutoka Benki ya Mkombozi kwenda Bank M kwa wale wanaohoji suala hili.

9. Ulipaji wa Deni na Madai yaliyobakia: Ili kutekeleza Master Plan, Julai 2011 JOHA TRUST ilikuwa imechukua mkopo wa Shs bilioni mbili (Shs 2,000,000,000/-) hapo Bank M kwa ajili ya ujenzi wa bweni kubwa lenye uwezo wa vitanda 163. Hadi kufikia tarehe 19/04/2014 mkopo huo ulipolipwa wote, deni hilo lilikuwa limezaa riba na gharama nyingine na kuongezeka hadi kufikia takriban jumla ya Shs bilioni mbili, milioni mia saba arobaini na moja, lhaki tatu sabini na nne elfu, mia nne arobaini na nne (Shs 2,741,374,444/-). Kwa hiyo, pamoja na ukubwa wa mchango wa Bw Rugemalira bado umelipia sehemu ya deni hilo tu. Sehemu nyingine iliyobaki (Shs 1,124,274,444/-) imelipwa kutoka vyanzo vingine vya mapato ikiwemo mkopo wa milioni mia mbili tisini na moja, lhaki tatu sabini na nne, mia nne arobaini na nne (Shs 291,374,444/-) zilizotolewa na Mwanzilishi kulipa riba ya kila mwezi wakati wa uhai wa mkopo huo. Ilikuwa maamuzi ya Bodi kupunguza madai hayo ya Mwanzilishi kutoka takriban Shs milioni 291 na kubakia takriban Shs milioni 174 . Kwa hiyo fedha zote alizozitoa Bw Rugemalira za Shs 1.617,100,000/- zilitumika kulipa mkopo na wala hazikutosha. Katika hali hiyo, hisia na madai yanayotolewa kwamba Mwanzilishi alijinufaisha na fedha hizo SI KWELI. Isingewezekana.

10. Ufadhili Endelevu wa Shule: Itambulike kwamba hata kwa nafasi yake Mwanzilishi ni mfadhili na mdhamini mkubwa wa JOHA TRUST kwa fedha zake binafsi. Bodi ilimwomba awe analikopesha shirika letu na wafadhili wakipatikana tunamrejeshea fedha zake polepole. Kwa mfano SIDA iliwahi kuridhia kwamba sehemu ya msaada wake utumike kurejesha mkopo uliotolewa na Mwanzilishi wakati wa kuanzisha shule kati ya mwaka 2000 hadi 2003.

11. Mchango wa VIP ulipokelewa kwa nia Njema. Shirika halina utaratibu kuwahoji wafadhili wetu wa ndani au nje kwanza kuthibitisha chanzo cha fedha zao wanazotuchangia. Misaada na michango, iwe mikubwa au midogo, yote imekuwa ikipokelewa kwa nia njema tukiamini pia inatolewa kwa nia njema. Tunaamini hivi pia ndivyo ilivyo kwa asasi nyingine nchini na jamii kwa ujumla kwa mfano michango ya maendeleo na hata harusi na shughuli nyingine kama hizo. Kwa kuwa tulihakikishiwa na Benki ya Mkombozi kwamba fedha za Bw Rugemalira zilikuwa zimelipiwa kodi, tulipokea mchango wake kwa furaha bila wasi wasi wowote.

12. Michango ya kuendeleza shule siyo zawadi binafsi kwa viongozi wake: Tunatambua kuwa sheria ya Maadili ya viongozi huwataka kuwasilisha zawadi zote zinazozidi Shs elfu hamsini (Shs50,000/-) kwa mwajiri wao. Kuna wanaodai Mwanzilishi amekiuka maadili kwa kutouwasilisha mchango huo Serikalini. Pia kuna wanaohoji kwa nini mchango mkubwa huo haukwenda kwenye jimbo lake la uchaguzi (Muleba Kusini) ili kuendeleza shule za Kata. Wote wanakosea. Mchango ulitolewa kwa shule ya JOHA TRUST na Mwanzilishi alipoufikisha kwetu tuliupokea na kuutumia kama ilivyokusudiwa kwa shughuli za maendeleo ya shule na kumwendeleza mtoto wa kike. Kufanya vinginevyo ndiko kungelikuwa kukiuka maadili.

13. Umuhimu wa Uchunguzi: Kupitia luninga tulifuatilia mjadala Bungeni Dodoma jioni ya Ijumaa tarehe 28, Novemba, 2014 kabla ya kikao hicho kuvurugika. Tulishuhudia jinsi Bunge zima lilivyoazimia kwamba vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake kuhusu waliopata ͞mgao͟ ili kuondoa mashaka na taarifa kamili zipatikane ili pale penye makosa hatua stahiki kuchukuliwa. Kwa hiyo, katika kikao cha Bodi cha tarehe 2 Desemba, 2014, kilichoitishwa rasmi kujadili jambo hili, kwa kauli moja tunatamka kwamba hatuamini kabisa na tunashindwa kuelewa kwa nini Mwanzilishi wetu atakiwe kuwajibishwa nafasi yake Serikalini kwa kuwa tu alipokea mchango wa shule kwa niaba yetu. Jambo hili litatuchanganya na kutukatisha tama sisi wananchi wa kawaida tunaojitolea kutekeleza shughuli mbali mbali za maendeleo hususan elimu. Tunaamini hatua hiyo pia itafifisha juhudi za viongozi wengine wengi wanaohangaika kuhamasisha michango ya shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, maji, vijana, walemavu, watoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, wazee, wajane, n.k. katika taifa letu changa. Tunaomba Mhe Rais alione jambo hili. Ikiwa michango ya maendeleo inayopokelewa na viongozi kwa niaba ya wadau wao itatafsiriwa kama zawadi zao binafsi kuna hatari kuzorotesha ͞harambee͟ za maendeleo. Tunaamini ufafanuzi huu utatosha kuondoa utata katika suala hili ili umma na viongozi wa ngazi za juu wapate ukweli juu ya jambo hili na ushiriki wetu. Bodi yetu iko tayari kujibu maswali yoyote yanayoweza kuulizwa ili kuondoa utata huu kabisa.

14. Shukrani kwa Wafadhili: Katika miaka 15 ya uwepo wa taasisi yetu (2000 -2014) , JOHA TRUST imepokea michango jumla ya Shs bilioni 13.59 kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Wafadhili wakubwa wa nje ni SIDA ambayo imetoa jumla ya Shs bilioni 8. 15 sawa na asilimia 60% na JOHA TRUST Sweden Shs bilioni 1.79 sawa na asilimia 13.11%. Mwaka 2000 Serikali ya Tanzania chini ya Mhe Rais mstaafu Benjamin Mkapa ilitoa ardhi ekari 50 kujenga shule ya Barbro jijini Dar es Salaam. Mwaka 2005 kabla ya kuondoka madarakani Rais Mkapa alikuja kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne kukagua maendeleo yetu, akaridhika na kuchangia Shs milioni tano (Shs 5,000,000/-). Kwa wahisani wa ndani ya nchi Dr. Reginald Mengi Mwenyekiti wa IPP amechangia jumla ya Shs milioni 278 mwaka 2013 alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne. Kwa hiyo alichofanya Bw James Rugemalira ni sawa sawa na wahisani wengine waliotuunga mkono. Tunawashukuru wafadhili wetu wote wa ndani na nje ya nchi kwa michango yao na tunawaahidi kuongeza juhudi zetu za kumwelimisha mtoto wa kike na kwa kufanya hivyo jamii nzima ya Watanzania.

15. Ujumbe kwa Wazazi: Kama ilivyofafanuliwa tarehe 25 Septemba, 2014 katika mahafali ya kidato cha nne, ni muhimu kwa wazazi na walezi kuyaelewa vizuri yaliyojiri katika suala hili kuepuka upotoshwaji unaotokana na sababu za kisiasa dhidi ya Mwanzilishi wetu. Pamoja na matatizo yaliyojitokeza hatujakata tamaa katika juhudi zetu kumjengea uwezo mtoto wa kike. Tunawaahidi wazazi ambao wamekuwa na wasiwasi kuhusu ufadhili wa watoto wao kwamba kazi inaendelea kama kawaida. Hivi sasa wasichana 83 katika shule ya BARBRO na wasichana 20 katika shule ya KAJUMULO wanasoma kwa ufadhili. Tunawahakikishia wasichana wote hawa 103 ambao ni asilimia 13% ya wanafunzi wote 783 tulionao wasiwe na wasiwasi bali kuendelea kusoma kwa bidii. Hakuna binti mwenye ufadhili tayari atakayepoteza nafasi yake katika shule zetu kwa sababu ya tukio hili. Tunachukua nafasi hii kuhimiza michango kutoka kwa wafadhili wengine watakaoguswa na juhudi zetu ili tuweze kuongeza uwezo wa kuwafadhili wahitaji wafikie asilimia 30% tuliyokusudia. Pamoja tuendelee kushirikiana katika kuendeleza elimu na ulezi bora kwa mtoto wa kike. Kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ͞Hasa wakati wa shida kukata tamaa ni dhambi

 

Attachments

 • File size
  134.7 KB
  Views
  8,456

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,607
2,000
Kawaida sana.

Bodi inalipwa na shule ya Tibaijuka. Ni jambo lisilo la kushangaza kusema chchote ili kufunika uovu na kujaribu kumsafisha mtuhumiwa kwa maslhi ya pande zote mbili. Tibaijuka na bodi.

Nyaraka kama hizi ni ujenzi wa mazingira ya kuonyesha innocence ya mtuhumiwa kwa kujaribu kumjustify kwenye public.

Mama Tiba kapiga yowe, lazima watu wa kariu naye wajaribu kumsaidia. Ni kawaida sana.

Lete habari nyingine! But at the moment we need back our money!.
 

win8

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
926
250
Saivi tena kila kitu kitawezekana, kwanini kama mlipata msaada huo wote kutoka Rugemalila hakuna hata gazeti moja nchini lilioandika kupokewa kwa fedha hizo nyingi kama tunavyoijuwa nchi yetu? taarifa hii inatoka leo iweje. Tibaijuka hana jinsi atakwenda na maji tu
 

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,300
2,000
Taarifa ya bodi ya wadhamini wa joha trust
kwa wazazi na umma kuhusumchango wa shs bilioni1.617 kutoka kwa bw. James rugemalira wa tarehe 12 februari, 2014
 

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,737
2,000
Haha wafa.maji hao...walikuwa wapi siku zote je kuna hata habari yupokea hilo gawio kama msaada japo kuandikwa ktk magazeti au tv zetu hapa.
 

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
4,696
2,000
Kila mara nakushauri achana na siasa haya mambo ya shule ndio mazuri jiuzulu in good faith uwasaidie watanzania katika elimu usisubiri raisi akutoe mana hawezi kukuacha wewe ni prof wasikudanganye utaachwa linda heshima ita waandishi waambie hivi "Nimeona mshika mawili yote humponyoka nimmeamua in good faith kuacha nyadhifa ya uwaziri na baadae sitogombea tena ubunge ili nisimamie kwa karibu elimu ya watoto wa kike. Unapongangana ndo watu wanahoji kwanini na uprofesa wako unahojiwa. Mi ni mtetezi wako ila kwa njia hiyo .
 

ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,761
2,000
Sawa hapo tumemwelewa, ila kuondoka Wizarani kuko palepale..Akae pembeni kupisha uchunguzi
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,529
2,000
Mama Tibaijuka mla rushwa tuu hasafishiki!kwa nini pesa haikuingia account ya shule?weka statement ya shule kuonyesha pesa imeingia na wakalipa deni
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Wamesoma,wamefanya kazi wameshiba na sasa wanataka kutuvurugia nchi!!!
Sio wa kuchekewa watu wa namna hii!!

She shud pack and go!!!
 

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
4,696
2,000
Sasa hao wazazi na alumni Serena hoteli kwanini isiwe shuleni-Serena hoteli jamani watu watakuwa na fikra huru hapo?watafika wangapi?Wa status ipi?.Ninachokijadili hapa ni ugumu wa mtu huyohuyo kuwa waziri au kiongozi wa juu serekalini na hapohapo fund raiser wa taasisi yake mana rushwa ni influence on decision making .Kwa mfano watu hutoa kiwango kikubwa cha michango ya harusikwa mabosi wao kuliko wafanyakazi wa kawaida sasa kiwango kikubwa mno kinataka ku-influence decisions flani au ku attract some favours .ndo mana nasema achana nao unasumbukia nini?piga chini wasikutajetaje natamani wakupe hii meseji ilikwenye hicho kikao udeclee resignation.Jielezee vizur jitakase kisha jiuzulu simple like that.
 

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,014
2,000
BARBRO JOHANSSON GIRLS’ EDUCATION TRUST
JOHA- TRUST

P.O. Box 14556, Dar es Salaam, Tanzania. Tel: 255 2129883 (0) 744 596649;
Fax 255 22 2129882; e-mail: johatrust@hotmail.com
TAARIFA YA BODI YA WADHAMINI WA JOHA TRUST KWA WAZAZI NA UMMA KUHUSU MCHANGO WA SHS BILIONI 1.617 KUTOKA KWA BW. JAMES RUGEMALIRA WA TAREHE 12 FEBRUARI, 2014 1. Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Barbro Johansson Girls’ Education Trust (JOHA TRUST au BARBRO) inatoa taarifa hii kutokana na utata uliojitokeza kuhusu mchango wa Shs bilioni moja milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,0000/- ) tulioupokea kutoka kwa Bw James Rugemalira wa VIP Engineering and Marketing Limited.


 1. Mwanzilishi wa Shirika na Malengo yake: Bodi ya Wadhamini BARBRO inachukua nafasi hii kufafanua kwamba kiongozi wa Waanzilishi wa asasi yetu ni Mhe Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Malengo na madhumuni ya taasisi ya JOHA TRUST ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike kwa kuwafadhili wasichana wenye vipaji lakini watokao katika familia za kipato kidogo kusoma katika shule bora inazoziendesha.


 1. Jina la taasisi ya JOHA TRUST linatokana na uamuzi wa wanawake waanzilishi kumpa heshima Hayati Dr. Mama Barbro Johansson (1912-1999) aliyewasili kutoka Sweden mwaka 1946 kama mmisionari na kuanzisha shule ya wasichana ya kati hapo Kashasha Bukoba. Mwaka 1954 alijiunga na Mwalimu Nyerere kupigania uhuru na baadaye kuwa raia wa Tanzania na Mbunge. Mwaka 1964 aliombwa na Mwalimu Nyerere kujitolea kuwa Mwalimu Mkuu wa sekondari ya juu (High School) pekee ya wasichana ya Tabora Girls iliyokuwa imekumbwa na utovu wa nidhamu na kutaka kufungwa. Mama Barbro akafanikiwa sana kuigeuza shule hiyo kiasi kwamba ilipata nishani ya UNESCO mwaka 1967. Mama Barbro ndiye alianzisha elimu ya watu wazima nchini na pia ndiye alimuunganisha Mwalimu Nyerere na wahisani kutoka nchi za Nordic ambazo zilianza ufadhili wake katika Kituo cha Elimu Kibaha na Kituo cha Kilimo, Uyole, Mbeya.


 1. Shule za JOHA TRUST na Sura yake: Shirika linamiliki na kuendesha Sekondari mbili nchini. Kwanza ni Sekondari Bingwa ya Barbro iliyopo jijini Dar es Salaam. Ilianzishwa mwaka 2000 ikiwa na wasichana 40 na hivi sasa wapo 632 wote wa bweni katika kidato cha 1 hadi 6. Pili ni Kajumulo Girls’ High School iliyopo Manispaa ya Bukoba. Ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wasichana 31 na hivi sasa wapo 151 katika kidato cha 1, 5 na 6. Jumla shule hizi zina wanafunzi 783 na waliomaliza ni 1,512. Wote isipokuwa 5 walifaulu mitihani na kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Kwa kulingana na uwezo wa mfuko wa ufadhili, wasichana 453 sawa na asilimia 30% ya wanafunzi wamesaidiwa karo. Shule ya Barbro imekuwa miongoni mwa shule kumi bora Tanzania (2010) na kwa wastani inakuwa kati ya shule 50 bora katika mitihani ya taifa. Itambulike kwamba mafanikio haya yanapatikana pamoja na shule kuwa na sera ya kutowafukuza wanafunzi kwa misingi ya ufaulu wa mitihani ili mradi wawe na nidhamu. Falsafa yetu ni kuwahimiza wanafunzi kuweka bidii kadri ya uwezo wao, kujithamini na kujiamini katika maeneo wanayofanya vizuri. Kipa umbele chetu ni maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja kwanza na sifa kwa shule baadaye. Katika hali hii walimu hawana budi kufanya kazi ya ziada.


 1. Gharama za Uendeshaji na vyanzo vyake: Tangu ianzishwe JOHA TRUST imetumia gharama ya Shs bilioni thelathini na mbili (Shs 32,267,000,000/-) ambazo zimetokana na karo na michango ya wazazi asilimia 37%; wafadhili wa nje asilimia 35%, wafadhili wa ndani asilimia 7% na mikopo asilimia 21%. Kama taasisi nyingi zinazotoa elimu, JOHA TRUST inakabiliwa na uhaba wa fedha na ujenzi bado kukamilika. Shule inatoa huduma ya elimu bora na haifanyi biashara kama wengi wasioelewa wanavyofikiri. Bila ruzuku na misaada viwango vyake vya juu haviwezekani. Shirika la misaada la Sweden (SIDA ) ambalo limekuwa mfadhili mkubwa limekamilisha ahadi yake ya ufadhili wa miaka 10 (2002-2012) lililopanga kwamba ingelitosha kusimika taasisi ya JOHA TRUST na kuitaka ijitegemee. Hata hivyo SIDA imeacha utekelezaji wa Master Plan ya BARBRO ya mwaka 2004 bado kukamilika. Jambo hili limekuwa changamoto kubwa kwa Bodi kwa sababu katika Master Plan SIDA ilipandisha viwango vya majengo kuwa juu kulingana na sifa na hadhi ya Mama Barbro. Ikihitimisha ufadhili huo, SIDA ilihimiza Bodi kuhamasisha michango ya ndani ili kujenga uendelevu na kukamilisha ujenzi wa Master Plan hiyo.


 1. Maombi ya Ufadhili: Kwa kuzingatia ushauri huo wa SIDA, mwaka 2012 Bodi ilimtaka Mwanzilishi (ProfesaTibaijuka) ambaye pia ni Mtafuta Fedha (Fund Raiser) wa JOHA TRUST kuwaomba baadhi ya wafanyabiashara mashuhuri nchini kuunga mkono shughuli za asasi yetu kwa michango. Bwana na Bibi James Rugemalira ni miongoni mwa wafanyabiashara walioombwa mchango huo kwa barua ya tarehe 4 Aprili 2012 kupitia kampuni yao ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited. Hatimaye mapema Februari 2014, bila kutaja ni kiasi gani, Bw. Rugemalira alimjulisha Mwanzilishi kwamba yuko tayari kufanya mchango ulioombwa na kumwagiza kwamba sharti ni yeye Mwanzilishi kufungua account hapo Mkombozi Benki kuupokea mchango huo na kuchukua jukumu la kuufikisha shuleni na kuhakikisha unatumika kama ilivyokusudiwa. Bw Rugemalira alieleza hakutaka kuhangaika kuhamisha fedha kwenda benki nyingine ambapo tayari kulikuwa na akaunti za shule.


 1. Mchango wa VIP ulivyopokelewa: Kama alivyotakiwa, Mwanzilishi alifungua account hiyo hapo Benki ya Mkombozi tarehe 3 Februari, 2014 na kuupokea mchango huo wa jumla ya bilioni moja, milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,000/=) kwa niaba ya shule tarehe 12 Februari, 2014 kutoka kwa kampuni ya VIP Engineering and Marketing.


 1. Maamuzi ya Bodi: Bodi ya Wadhamini BARBRO ilikaa katika kikao maalum tarehe 13 Februari, 2014 kupokea taarifa ya mchango huo mkubwa kutoka kwa Bw. Rugemalira kupitia kampuni yake ya VIP Engineering. Bodi iliukubali na kuamua mchango huo utumike kulipa sehemu ya deni la shule hapo Bank M ambalo lilikuwa changamoto kubwa. Kwa hiyo Mwanzilishi aliagizwa na Bodi kuhamisha fedha hizo kutoka akaunti yake ya Mkombozi kwenda akaunti ya Bank M kulipia mkopo huo. Hii inafafanua kwa nini fedha zilihama kwa haraka kutoka Benki ya Mkombozi kwenda Bank M kwa wale wanaohoji suala hili.


 1. Ulipaji wa Deni na Madai yaliyobakia: Ili kutekeleza Master Plan, Julai 2011 JOHA TRUST ilikuwa imechukua mkopo wa Shs bilioni mbili (Shs 2,000,000,000/-) hapo Bank M kwa ajili ya ujenzi wa bweni kubwa lenye uwezo wa vitanda 163. Hadi kufikia tarehe 19/04/2014 mkopo huo ulipolipwa wote, deni hilo lilikuwa limezaa riba na gharama nyingine na kuongezeka hadi kufikia takriban jumla ya Shs bilioni mbili, milioni mia saba arobaini na moja, lhaki tatu sabini na nne elfu, mia nne arobaini na nne (Shs 2,741,374,444/-). Kwa hiyo, pamoja na ukubwa wa mchango wa Bw Rugemalira bado umelipia sehemu ya deni hilo tu. Sehemu nyingine iliyobaki (Shs 1,124,274,444/-) imelipwa kutoka vyanzo vingine vya mapato ikiwemo mkopo wa milioni mia mbili tisini na moja, lhaki tatu sabini na nne, mia nne arobaini na nne (Shs 291,374,444/-) zilizotolewa na Mwanzilishi kulipa riba ya kila mwezi wakati wa uhai wa mkopo huo. Ilikuwa maamuzi ya Bodi kupunguza madai hayo ya Mwanzilishi kutoka takriban Shs milioni 291 na kubakia takriban Shs milioni 174 . Kwa hiyo fedha zote alizozitoa Bw Rugemalira za Shs 1.617,100,000/- zilitumika kulipa mkopo na wala hazikutosha. Katika hali hiyo, hisia na madai yanayotolewa kwamba Mwanzilishi alijinufaisha na fedha hizo SI KWELI. Isingewezekana.


 1. Ufadhili Endelevu wa Shule: Itambulike kwamba hata kwa nafasi yake Mwanzilishi ni mfadhili na mdhamini mkubwa wa JOHA TRUST kwa fedha zake binafsi. Bodi ilimwomba awe analikopesha shirika letu na wafadhili wakipatikana tunamrejeshea fedha zake polepole. Kwa mfano SIDA iliwahi kuridhia kwamba sehemu ya msaada wake utumike kurejesha mkopo uliotolewa na Mwanzilishi wakati wa kuanzisha shule kati ya mwaka 2000 hadi 2003.


 1. Mchango wa VIP ulipokelewa kwa nia Njema. Shirika halina utaratibu kuwahoji wafadhili wetu wa ndani au nje kwanza kuthibitisha chanzo cha fedha zao wanazotuchangia. Misaada na michango, iwe mikubwa au midogo, yote imekuwa ikipokelewa kwa nia njema tukiamini pia inatolewa kwa nia njema. Tunaamini hivi pia ndivyo ilivyo kwa asasi nyingine nchini na jamii kwa ujumla kwa mfano michango ya maendeleo na hata harusi na shughuli nyingine kama hizo. Kwa kuwa tulihakikishiwa na Benki ya Mkombozi kwamba fedha za Bw Rugemalira zilikuwa zimelipiwa kodi, tulipokea mchango wake kwa furaha bila wasi wasi wowote.


 1. Michango ya kuendeleza shule siyo zawadi binafsi kwa viongozi wake: Tunatambua kuwa sheria ya Maadili ya viongozi huwataka kuwasilisha zawadi zote zinazozidi Shs elfu hamsini (Shs50,000/-) kwa mwajiri wao. Kuna wanaodai Mwanzilishi amekiuka maadili kwa kutouwasilisha mchango huo Serikalini. Pia kuna wanaohoji kwa nini mchango mkubwa huo haukwenda kwenye jimbo lake la uchaguzi (Muleba Kusini) ili kuendeleza shule za Kata. Wote wanakosea. Mchango ulitolewa kwa shule ya JOHA TRUST na Mwanzilishi alipoufikisha kwetu tuliupokea na kuutumia kama ilivyokusudiwa kwa shughuli za maendeleo ya shule na kumwendeleza mtoto wa kike. Kufanya vinginevyo ndiko kungelikuwa kukiuka maadili.


 1. Umuhimu wa Uchunguzi: Kupitia luninga tulifuatilia mjadala Bungeni Dodoma jioni ya Ijumaa tarehe 28, Novemba, 2014 kabla ya kikao hicho kuvurugika. Tulishuhudia jinsi Bunge zima lilivyoazimia kwamba vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake kuhusu waliopata “mgao” ili kuondoa mashaka na taarifa kamili zipatikane ili pale penye makosa hatua stahiki kuchukuliwa. Kwa hiyo, katika kikao cha Bodi cha tarehe 2 Desemba, 2014, kilichoitishwa rasmi kujadili jambo hili, kwa kauli moja tunatamka kwamba hatuamini kabisa na tunashindwa kuelewa kwa nini Mwanzilishi wetu atakiwe kuwajibishwa nafasi yake Serikalini kwa kuwa tu alipokea mchango wa shule kwa niaba yetu. Jambo hili litatuchanganya na kutukatisha tama sisi wananchi wa kawaida tunaojitolea kutekeleza shughuli mbali mbali za maendeleo hususan elimu. Tunaamini hatua hiyo pia itafifisha juhudi za viongozi wengine wengi wanaohangaika kuhamasisha michango ya shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, maji, vijana, walemavu, watoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, wazee, wajane, n.k. katika taifa letu changa. Tunaomba Mhe Rais alione jambo hili. Ikiwa michango ya maendeleo inayopokelewa na viongozi kwa niaba ya wadau wao itatafsiriwa kama zawadi zao binafsi kuna hatari kuzorotesha “harambee” za maendeleo. Tunaamini ufafanuzi huu utatosha kuondoa utata katika suala hili ili umma na viongozi wa ngazi za juu wapate ukweli juu ya jambo hili na ushiriki wetu. Bodi yetu iko tayari kujibu maswali yoyote yanayoweza kuulizwa ili kuondoa utata huu kabisa.


 1. Shukrani kwa Wafadhili: Katika miaka 15 ya uwepo wa taasisi yetu (2000 -2014) , JOHA TRUST imepokea michango jumla ya Shs bilioni 13.59 kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Wafadhili wakubwa wa nje ni SIDA ambayo imetoa jumla ya Shs bilioni 8. 15 sawa na asilimia 60% na JOHA TRUST Sweden Shs bilioni 1.79 sawa na asilimia 13.11%. Mwaka 2000 Serikali ya Tanzania chini ya Mhe Rais mstaafu Benjamin Mkapa ilitoa ardhi ekari 50 kujenga shule ya Barbro jijini Dar es Salaam. Mwaka 2005 kabla ya kuondoka madarakani Rais Mkapa alikuja kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne kukagua maendeleo yetu, akaridhika na kuchangia Shs milioni tano (Shs 5,000,000/-). Kwa wahisani wa ndani ya nchi Dr. Reginald Mengi Mwenyekiti wa IPP amechangia jumla ya Shs milioni 278 mwaka 2013 alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne. Kwa hiyo alichofanya Bw James Rugemalira ni sawa sawa na wahisani wengine waliotuunga mkono. Tunawashukuru wafadhili wetu wote wa ndani na nje ya nchi kwa michango yao na tunawaahidi kuongeza juhudi zetu za kumwelimisha mtoto wa kike na kwa kufanya hivyo jamii nzima ya Watanzania.


 1. Ujumbe kwa Wazazi: Kama ilivyofafanuliwa tarehe 25 Septemba, 2014 katika mahafali ya kidato cha nne, ni muhimu kwa wazazi na walezi kuyaelewa vizuri yaliyojiri katika suala hili kuepuka upotoshwaji unaotokana na sababu za kisiasa dhidi ya Mwanzilishi wetu. Pamoja na matatizo yaliyojitokeza hatujakata tamaa katika juhudi zetu kumjengea uwezo mtoto wa kike. Tunawaahidi wazazi ambao wamekuwa na wasiwasi kuhusu ufadhili wa watoto wao kwamba kazi inaendelea kama kawaida. Hivi sasa wasichana 83 katika shule ya BARBRO na wasichana 20 katika shule ya KAJUMULO wanasoma kwa ufadhili. Tunawahakikishia wasichana wote hawa 103 ambao ni asilimia 13% ya wanafunzi wote 783 tulionao wasiwe na wasiwasi bali kuendelea kusoma kwa bidii. Hakuna binti mwenye ufadhili tayari atakayepoteza nafasi yake katika shule zetu kwa sababu ya tukio hili. Tunachukua nafasi hii kuhimiza michango kutoka kwa wafadhili wengine watakaoguswa na juhudi zetu ili tuweze kuongeza uwezo wa kuwafadhili wahitaji wafikie asilimia 30% tuliyokusudia. Pamoja tuendelee kushirikiana katika kuendeleza elimu na ulezi bora kwa mtoto wa kike. Kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere “Hasa wakati wa shida kukata tamaa ni dhambi”.


IMETOLEWA NA BODI YA WADHAMINI WA SHIRIKA LA JOHA TRUST TAREHE 2 DESEMBA, 2014 JIJINI DAR ES SALAAM
Imesainiwa na Imesainiwa na
Bw SALMON ODUNGA Mhe BALOZI PAUL RUPIA
MWENYEKITI MLEZITAARIFA: KUTAKUWEPO NA KIKAO MAALUM CHA BODI YA WADHAMINI, BODI YA SHULE YA BARBRO, WAZAZI , WAALIMU NA WAHITIMU (ALLUMNAE) KUHUSU JAMBO HILI JUMATANO TAREHE 10 DESEMBA, 2014 KATIKA UKUMBI WA MKUTANO WA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM KUANZIA SAA TANO NA NUSU HADI SAA TISA MCHANA. MNAKARIBISHWA.
KWA TAARIFA ZAIDI PIGA SIMU KWA MWALIMU MKUU
BI HALIMA KAMOTE +255744596649
SOURCE: ISSA MICHUZI
 

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,194
1,250
Mbona kama document yote mnazungumzia JOHA TRUST? Eti wenye kipato kidogo kusoma shule nzuri..niambieni ADA ya kusoma shule hii kwanza.
 

Mantombazane

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
491
250
Huo ni ujanja tu wa kuchukua pesa. Eti lazima mpewaji afungue account Mkombozi? Kwakuwa ana shule ana tafuta pa kutokea. Hata bodi itafanya nini kwa mwenye shule zaidi ya kumlinda? Bil 1.6 mchango? Mtoaji labda awe mume, mchepuko au share holder
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom