Prof.Tibaijuka atajwa tena na mtandao wa kimataifa wa EQUALITY FOR HER

jembe2015

Senior Member
Sep 21, 2014
118
71
Mtandao wa Equality For Her umemtaja Prof.Tibaijuka miongoni mwa wanawake majasiri,hodari shujaa ktk kupigania haki za wanawake na maendeleo kwa ujumla Duniani.

Mtandao huu wenye makao yake makuu New York nchini Marekani,ni mtandao ambao umekua ukitambua na kuenzi juhudi na mchango wa wanawake hodari na jasiri duniani kote katika kupigania haki na maendeleo.Kwa mara ya kwanza Mtanzania pekee amepata bahati ya kutajwa katika mtandao huo kwa kutambua mchango wake katika nyanja tofauti za kimaendeleo Duniani na katika kuendesha harakati za wanawake.

Itakumbukwa kuwa Tibaijuka mbali na kushika nyadhifa mbali mbali duniani,lakini pia ni mwanaharakati wa kutetea haki na maendeleo ya wanawake,anatambuliwa kwa kuanzisha BALAZA LA WANAWAKE TANZANIA (BAWATA),ambapo yeye ndiye mwenyekiti wake, ni mwanzirishi wa taasisi ya JOHA TRUST ambayo inasimamia na kuendesha shule bora za mfano kwa wasichana hapa nchini,Akiwa umoja wa mataifa alianzisha taasisi mbalimbali za kutetea haki na usawa wa wanawake kumiliki ardhi hasa kwa bara la Afrika,badhi yake ni UGWLAT-UGANDA,KEWLAT-KENYA,TAWLAT-TANZANIA,ZIWLAT-ZIMBABWE.... na sehem zingine nyingi Afrika.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanasababisha mwanamke huyu kuendelea kutambuliwa sehemu mbalimbali duniani katika kuchangia maendeleo.

Miongoni mwa wanawake wengine walio tajwa na mtandao huo ni walio wahi kushika nyadhifa za uraisi na kuleta mapinduzi katika nchi zao,wanaharakati mbali mbali Duniani kama Kamala Harris,mmarekani mweusi wa kwanza kuwa mwanasheria mkuu Calfornia,Ursula Burns CEO na mwenyekiti wakwanza mwanamke kuongoza zaidi ya kampuni 500 za Fortune.Wengine ni Shirley Chisholm,Tasneem Zehra Husain,Yu Su-May na wengine wengi.
Heko kwa Prof.Tibaijuka
 

Attachments

  • Tiba 2.PNG
    Tiba 2.PNG
    106.2 KB · Views: 19
  • Tiba 5.PNG
    Tiba 5.PNG
    7.7 KB · Views: 18
  • Tiba.PNG
    Tiba.PNG
    24.5 KB · Views: 20
  • Tiba3.PNG
    Tiba3.PNG
    97.3 KB · Views: 20
  • Tiba4.PNG
    Tiba4.PNG
    56.2 KB · Views: 18
Back
Top Bottom