Prof. Safari: Magufuli shujaa wa Afrika

Prof. Safari: Magufuli shujaa wa Afrika

Prof safari ni msaliti aondoke

😀 🙂
Kwahiyo na Edward Lowasa naye ni msaliti na aondoke ?
Maana hata yeye amesifu jitihada za Magufuri.
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu atakataa juhudi za mheshimiwa Raisi juu ya kudhibiti raslimali za taifa.
Upinzani ni ushindani wenye maslahi kwa taifa.
Namfahamu mheshimiwa Prof, Safari.
Ni msomi makini na mzalendo halisi.
Yapo mengi mema yanafanywa na vyama vya upinzani na CCM pia.
Sera yenye maslahi kwa taifa ni lazima iungwe mkono bila kujali kama imetolewa na Tundu Lisu au Rais Magufuli.
 
Tatizo liko kwenye tabia.

Sheria gani amekiuka? Iweke hapa precisely siyo kkupiga ramli za kipumbavue kwa sababu tu umekaririshwa.

Hawa manyang'au wamefuata sheria? Sheria ipi inayowapa mamlaka ya kuharibu mali? Jibu bila hadhithi za kipumbavue!
Mwambieni Mbowe aende mahakamani kamaa anaona kaonewa!

Period!
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari amemfananisha Rais John Magufuli na Rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Congo (DRC), Patrice Lumumba kutokana na juhudi binafsi anazofanya kutetea rasilimali za nchi.

Wakati Profesa Safari akisema hayo, Mbunge wa Chambani, Yusuf Salim Hussein (CUF) amesema anamuunga mkono Rais Magufuli, kwani amejitoa mhanga kwa maslahi ya taifa. Aliwaambia wabunge vita hiyo ni ngumu na wanapaswa kumshukuru Rais bila ya kujali kama ni wa CCM, Chadema au CUF.

“Sisi si maadui, tuungane tuwe pamoja kwa maslahi ya taifa, tujiulize tunataka kwenda wapi, tusameheane na twende mbele kwani tukipasuka hatutafika,” alisema. Kwa upande wake, Profesa Safari alisema hayo ofisini kwake Dar es Salaam jana, alipotoa maoni yake juu ya agizo la Rais kutaka iundwe timu ya wataalamu kupitia upya sheria za madini nchini na kupelekwa bungeni ili zifanyiwe marekebisho.

“Ninampongeza Rais John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kutetea rasilimali za nchi. Anafanya kazi kama walivyokuwa wanafanya baadhi ya viongozi wazalendo barani Afrika ya kupigania haki za wananchi wao kufaidika na rasilimali za nchi,” alisema Profesa.

Alitoa mfano wa Patrice Lumumba, Kwame Nkrumah na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama viongozi waliojitolea kwa ajili ya wananchi wao. Alisema maamuzi anayoyafanya Rais yanasimama katika Kifungu cha Tisa (Kifungu Kidogo C) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho ya mwaka 2000, ambacho kinasisitiza kwamba utajiri wa Taifa uendelezwe, uhifadhiwe na kutumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine.

Profesa Safari aliwaomba Watanzania na wataalamu wa sheria za mikataba, kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais katika kutetea maslahi ya Taifa. “Nchi hii ina wanasheria wengi wazuri katika masuala ya madini na mikataba. Ninashauri watafutwe wataalamu hawa watakaokuwa sio wala rushwa ili wamsaidie Rais katika vita hii ya rasilimali,” aliongeza Profesa Safari.

Akizungumza kwa niaba ya wazee waliofika Ikulu kusikiliza ripoti ya Kamati ya pili ya kuchunguza mchanga wenye madini, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alielezea ujasiri unaofanywa na Rais Magufuli kuwa ni mfano wa kuigwa na Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais kutetea rasilimali.

Juzi Rais Magufuli alipokea ripoti ya Kamati ya Pili ya Madini ya kuangalia masuala ya kisheria na kiuchumi, ambapo ilionesha Serikali imekuwa ikipoteza mapato ya Sh trilioni 108.46 kutokana na udanganyifu, unaofanywa katika usafirishaji wa mchanga wa dhahabu ‘makinikia’ nje ya nchi katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi mwezi Machi 2017.

Wakati huo huo, Bunge linatarajiwa kutoa Azimio la kumuunga mkono Rais Magufuli kutokana na kazi nzuri, zilizofanywa na kamati mbili alizoziteua kuchunguza mchanga wa dhahabu (makinikia) zilizobaini wizi mkubwa, anaripoti Mgaya Kingoba kutoka Dodoma.

Wabunge wengi wakiwamo wa Kambi ya Upinzani, walisema jana kuwa wameikubali kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli katika suala la madini, ingawa wao walinyoosha kidole kwa Serikali ya CCM kuwa ilishindwa kuzuia wizi huo.

Wabunge wote waliochangia jana walitoa pongezi kwa Rais Magufuli kutokana na kazi nzuri ya kamati zake mbili; ya kwanza ya wataalamu wa jiolojia na kemia na ya pili ya wachumi na wanasheria, ambazo zimeibua wizi mkubwa uliofanywa na kampuni za uchimbaji madini.

Hata kabla ya kuanza kwa mjadala huo asubuhi, Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM), aliomba mwongozo wa Spika, kwa nini Bunge lisitoe Azimio la kumpongeza Dk Magufuli kwa kazi nzuri kuhusu makinikia.

Akijibu mwongozo huo, Spika Job Ndugai aliagiza Kamati ya Uongozi ikutane mara moja na baadaye kabla ya kusitisha shughuli za Bunge mchana, angetoa majibu ya kikao hicho alichoagiza kiongozwe na Mwenyekiti wa Bunge, Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM).

Kabla ya kusitisha kikao hicho saa saba mchana, Spika Ndugai alitangaza kuwa kikao kimeamua kuwa ni busara kutoa Azimio ili kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kulinda rasilimali za Taifa.

Alisema kwa maana hiyo azimio hilo litaandaliwa kwa kufuata Taratibu na Kanuni za Bunge na kuwasilishwa bungeni, lakini akaagiza, “Kwa mamlaka yangu ya Spika, liwasilishwe kesho (leo) bila kuchelewa.”

Katika mjadala wa bajeti, Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajab (CCM) alisema Bunge lichukue hatua kuhakikisha kiwanda cha kuchenjua dhahabu kinaanzishwa nchini ili kumuunga mkono Rais Magufuli, ikiwamo kuifumua bajeti ili kutenga fedha za kiwanda hicho.

Akaongeza, “Tumeibiwa sana, never, never, never again (kamwe isijirudie). Tuhakikishe fedha zetu zinarudi, wakikataa tuwashitaki,” alieleza Balozi Adadi. Kwa upande wake, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) alisema wananchi wa jimbo lake wanafahamu madhira yaliyosababishwa na kampuni za madini, ikiwamo vifo vya binadamu na mifugo.

Alisema zipo pia rasilimali nyingine zinazoibwa hata katika maeneo ya utalii kama Loliondo. Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko (CCM), alisema Taifa limeibiwa sana na sasa basi,

Chanzo: Habari leo
Kwa sisi wapinzan hakuna cha kusifia wala masilahi ya taifa sisi ni kupinga mwanzo mwisho ndo maana halisi ya opposition
 
Lissu ndio mwamba uliobaki mambo ya kuchunguza na mikataba kupelekwa bungeni yameanza tangu 2000 lakini wizi ulikuwepo tu, solution ni CCM out sio porojo za kila siku.
 
Lissu ndio mwamba uliobaki mambo ya kuchunguza na mikataba kupelekwa bungeni yameanza tangu 2000 lakini wizi ulikuwepo tu, solution ni CCM out sio porojo za kila siku.
Mkuu nyie ndio watu wenye matatizo...unahisi CDM tu ndio solution, this time Magufuli Hayupo kichama kama akili yako ipo vizuri utakua umetambua.Hata kama katokea chama kilicholeta haya madudu but haimaanishi Mwenye dhambi akigeuka akiacha dhambi(wengine wanasema kuokoka) ashindwe kuhubiri madhara ya dhambi cuz alikua mtenda dhambi...ni mpango wa Mungu kuileta Tanzania Mpya now hata kama asingekua Mh Magufuli angekuapo Rais Mwingine, Mpango wa Mungu Ni sasa. Tanzania Kwanza.
 
acha kumsingizia Mungu mambo yasiyo faa,
 
Gazet lenyewe uhuru , wataandika kinyume cha Magu?? Bahat nzuri Lowassa ameongea hadharan vinginevyo wangeandika tofauti na alivyoongea. Haya Lowassa kampongeza na kasema tupate katiba mpya kama suruhu ya mambo haya mbona hili hamwongelei????? Kwa lugha rahis Lowassa amesema ni bure kupambana na wanyinyaji kwa taratibu hizi tulizo nazo. Ambazo sheria inasema madini ni mali ya mwekezaji!! So hata sipage shida nani kaongea nini
 
ngoja wamsifie kukimbia tu apitilize mpaka kwao mr.misifa
 
Mkuu nyie ndio watu wenye matatizo...unahisi CDM tu ndio solution, this time Magufuli Hayupo kichama kama akili yako ipo vizuri utakua umetambua.Hata kama katokea chama kilicholeta haya madudu but haimaanishi Mwenye dhambi akigeuka akiacha dhambi(wengine wanasema kuokoka) ashindwe kuhubiri madhara ya dhambi cuz alikua mtenda dhambi...ni mpango wa Mungu kuileta Tanzania Mpya now hata kama asingekua Mh Magufuli angekuapo Rais Mwingine, Mpango wa Mungu Ni sasa. Tanzania Kwanza.
"Magufuli hayupo kichama" umeondoa uhalali wa post yako mkuu wangu kajipange.
 
Ameanza Lowasa kumpongeza Magufuli. Amekuja Prof Safari. Naamini ndani ya UKAWA kuna mpasuko mkubwa unakuja

Ila mpaka leo Lissu na Msigwa wanampinga. Sasa itategemea kati ya hawa pamoja na Mbowe ni nani ambaye ndio kiongozi wao kiukweli. Msimamo wa kiongozi wa kiukweli utafuatwa na wote ikiwa ni pamoja na wale wanaoonekana kutofautiana muda huu. Ni kama wanyama waleeeeee wa mwituni wote hukimbilia kumoja . Kumbuka kiongozi wa wakati ule alivyotuongoza kuupinga ufisadi kwa nguvu halafu baadaye alipobadili gia angani na kuukumbatia ufisadi kwa mahaba pia tukamuunga mkono na kumfuata kama wanyama waleeee wa mwituni.
 
Kwahiyo na Edward Lowasa naye ni msaliti na aondoke ?
Maana hata yeye amesifu jitihada za Magufuri.
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu atakataa juhudi za mheshimiwa Raisi juu ya kudhibiti raslimali za taifa.
Upinzani ni ushindani wenye maslahi kwa taifa.
Namfahamu mheshimiwa Prof, Safari.
Ni msomi makini na mzalendo halisi.
Yapo mengi mema yanafanywa na vyama vya upinzani na CCM pia.
Sera yenye maslahi kwa taifa ni lazima iungwe mkono bila kujali kama imetolewa na Tundu Lisu au Rais Magufuli.

Tundu Lisu , yeye anataka tusubili mpaka Chama chake kiingie ikulu(Mwaka 2999) ndiyo tuanze kufuatilia/kulinda Madini yetu.
 
Back
Top Bottom