Prof. Safari ajiondoa CUF; Atafakari pa kwenda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Safari ajiondoa CUF; Atafakari pa kwenda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jan 18, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mwanachama mwanazuoni wa CUF aliyewahi kupambana na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CUF na kuambulia kuzomewa, Profesa Abdallah Safari, amejivua uanachama wa chama hicho na inasemekana yuko mbioni kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mhhhh ni habari njema! Ila asije leta vurugu
   
 3. czar

  czar JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Cool man, the guy is goood. Ataleta changamoto nzuri kwenye chama.
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Source please
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,057
  Trophy Points: 280
  Lipumba ni mgombea urais na mwenyekiti wa CUF 4LiFe.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,775
  Trophy Points: 280
  mkuu ngoja nijaribu kuamini hii kitu..
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Namfahamu vema Ndugu Abdalla Safari.

  Ni miongoni mwao watoto halisi wa baba wa taifa na wenye uchungu wa kweli na uduni wa maisha yetu huku taifa letu likiporwa na majambazi kupitia lango kuu na kwa msaada wa watu tuliowapa dhamana kulinda mali ya pamoja.

  Huyu Prof Mwenye ofisi zake pale barabara ya Samora, ni kifaa, ni mzalendo anayeumwa na taifa lake kubakwa, ni mwanasheria mwenye uwezo wa kuona jambo na kulitolea msimamo BILA KUMEZWA NA UKUNGU WA IMANI YA DINI YAKE, na ni mtu jasiri siku nyingi na hata pale alipokua chuo cha diplomasia kurasini.

  Naunga mkono hatua anayofikiria kuuchukua, si kwa ajili ya kutafuta vyeo wala pesa, bali ni katika kuumwa kule na ufukara wetu na jinsi wasomi walio wengi wanavyoonekana wabinafsi wakubwa kwa KWA KULA NJAMA NA MAFISADI NA SERIKALI DHALIMU NA YA MAUAJI YA CCM na jinsi kinavyotutenda Watanzania ambao hata siku moja hatukujua kitu kubaguana wala kula jasho la wenzetu.

  Karibu Prof Safari katika hii safu pana na huru zaidi kutafuta kutuokoa sisi Vijana wa taifa hili nasi tupate kuwa watu mbele ya waungwana. Karibuni na wasomi wengine wengi wenye kupenda kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa letu.

  Utaifa mbele kama tai na vijana sote tuko tayari kuwapeni kura zetu kwa muda mwafaka.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,775
  Trophy Points: 280
  utaifa mbele kama tai sio? Nimeipenda hii
  na nawaomba cdm kuwa huyu jamaa akishajiunga tu apewe cheo ..ni itasaidia sana katika ukombozi coz many knows that chadema ni ya kidini
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,057
  Trophy Points: 280
  Kuna watu humu wataanza kumponda kwa vile tu anajiunga CDM ngoja niwape muda, and this could be a substitute for Zitto.
   
 10. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  it is good for diversity within Chadema
   
 11. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Karibu Prof. kwa wapiganaji wenzako.
   
 12. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Karibu Prof. Vijana tupo tayari, walete na wenzio
   
 13. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Profesa Safari ang'atuka CUF

  Sadick Mtulya

  ALIYEWAHI kupambana na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CUF, Profesa Abdallah Safari, amejivua uanachama wa chama hicho.

  Taarifa ambazo zilipatikana jana na baadaye kuthibitishwa na Profesa Safari, hazikubainisha sababu za kujitoa kwake kwenye chama hicho na kwamba, anapanga kuanika hadharani keshokutwa.


  "Pamoja na kwamba zipo sababu za mimi kufikia uamuzi huu, lakini kwa leo (jana) siwezi kueleza chochote zaidi ya kutangaza nimejiondoa CUF,'' alisema Profesa Safari na kuongeza: "Kesho kutwa (Alhamisi) nitatangaza rasmi azma yangu ya kujivua uanachama wa CUF.''

  Profesa Safari ambaye ni mwanazuoni aliyebobea kwenye taaluma ya sheria, alijiunga CUF mwaka 2005 na Februari 2009, aliwania uenyekiti na Profesa Lipumba akaambulia ushindi kura sita.


  Alisema amefikia uamuzi wake huo kwa utashi wake, bila kushinikizwa na mtu. "Napenda wananchi waelewe kuwa uamuzi huu, nimeufikia bila shinikizo lolote,'' alisema Profesa Safari.


  Hata hivyo, Profesa Safari alieleza kuwa pamoja na kung'atuka kwake CUF, ataendelea kuwa mwanasiasa bila kueleza atashabikia chama atakachoshabikia. Uamuzi huo ameufikia ikiwa ni takriban mwaka mmoja na nusu baada ya kuangushwa vibaya kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CUF na Profesa Lipumba aliyepata kura 646.


  Kufuatia matokeo hayo, Profesa Safari aliwashtumu wajumbe wa mkutano mkuu kuwa, walimdhalilisha na angeandaa kitabu kueleza udhalilishaji huo. Februari 23, 2009 wakati Profesa Safari akijieleza katika mkutano mkuu wa kuchagua mwenyekiti wa CUF, wajumbe walikuwa wakimzomea na baadaye kumrushia maswali yaliyomtingisha, ikiwamo kumtaka kutaja jina la katibu wa tawi lake. "Nimedhalilishwa; nimezomewa; nimeulizwa maswali ya kipuuzi.


  Ule ni uhuni hakuna kitu pale," alisema Profesa Safari na kuongeza: "Wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wamepotosha na kuharibu maana ya demokrasia ndani ya CUF na kutumia vibaya nafasi hiyo ya kuchagua viongozi." Alipobanwa kueleza iwapo anafikiria kuwania tena nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho, Profesa Safari alisema hawezi na hana nia ya kuwania uongozi wa chama hicho.


  Hata hivyo, taarifa ambazo zilikuwa zikisikika ni kwamba, Profesa Safari alikuwa haelewani na uongozi wa CUF hasa baada ya kuhoji taratibu zilizotumika kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kusaini mkataba wa siri kuunda ya umoja.
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,057
  Trophy Points: 280
  Kama Chadema watafanikiwa kumpata huyu jamaa watakuwa wameua ndege wawili kwa jiwe moja.
   
 15. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Hataanzisha ugomvi na Marando?
   
 16. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bad timing! Kila mmoja atajua kuwa amenunuliwa na KANISA ili ku-balance mambo kwenye CDM. Atadharauliwa hata na nzi! Asubiri upepo wa udini upungue CDM
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,057
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu mtakuja wapenda udini ina maana alipokuwa CUF alikuwa amenunuliwa na msikiti gani acha ujinga.
   
 18. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Some people are 100% predictable
   
 19. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watu wengine ovyoooooooo, hata uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, sana, Yaani Profesa Safari ANUNULIWE na kanisa ili iweje, ?, kiufupi Kama profesa safari atahamia CDM, litakuwa pigo kubwa sana kwa CUF, watake wasitake.
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Nakusikitkia sana kwamba Prof Abdalla Safari humjui hata kidogo. Wa kununuliwaa Ndg Abdalla Safari?? Hebu kaulize wenzio kwamba huyu professor ni mtu wa aina gani.

  Kuhusu swala la udini ambao mara nyingi humfanya Prof Lipumba kugeuka BUBU HATA KWA MASWALA MAZITO KITAIFA AMBAYO YANAHITAJI BUSARA ZA HALI YA JUU BILA KUEGEMEA UPANDE, kwake Prof Safari wala hili halimpi taabu hata kido

  Walau japo hata kidogo tu, ukitaka kujua Ndg Safari ni nani katika nchi hii basi nakushauri upitie mchango namba 7 hapo juu. Wala sikubaliani na wewe kwamba kuna majira maalum katika mwaka ambapo ndio mtu anaweza kuhamia chama nyingine.

  Chukua darasa zaidi JF.
   
Loading...