Aondoke tu kwa amani asiwaharibie wenye chama chao, kama angeshinda ile nafasi aliyogombea wakati ule akashidwa vibaya kweye topten za CUF angeondoka? Nafikiri kwa kuwa Prof. Safari ni mtu mwenye heshima zake si busara kuondoka kwa kuzua lawama kwa wenzake. Vyama vyote vinakasoro zake na hicho chama cha malaika anachosubiri kitokee hapa nchini kamwe hakitatokea hivyo nafikiri aendelee na shughuli zake za kila siku badala ya kuwatuhumu wenzake. Haya ndiyo mambo yanaodhoofisha vyama vya siasa na kuruhusu chama tawala kifanye kitakavyo. Kama amegundua kasoro ndani ya CUF angewasilisha maoni yake kwa kufuata taratibu zinazoeleweka pale inaposhindikana ndiyo aangalie uwezekano mwingine bila kuwaharibia wenzake.