Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Awali ya yote, Lusako, alishukuru uongozi wa gazeti la The Citizen, alimshukuru sana mwandishi wa makala hii ndugu, Khalfa Said na wahariri wake, haswa kwa kufanya utafiti wa kina kujua undani wa sakata hili ambalo limekuwa gumzo sasa nchini. “Shukrani yangu kuu ni moja tu, mumepaza sauti ya mnyonge ambayo huenda isinge sikika tena katika historia ya taifa hili. Watawala hutumia nguvu ya Vyombo vya habari kuzika ndoto za wanyonge kinyume na ninyi mlioamua kuchimba undani wa sakata hili na kupaza sauti” alisema Lusako.
Lusako: pamoja na baadhi ya taarifa chache sana za Ukweli alizozitoa Prof. Rwekaza Mkandala, nimesikitishwa sana na upotoshwaji wa taarifa uliofanywa na Prof. ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Saam(UDSM), lakini vilevile Dr. Kokuberwa Mollel, Mkurugenzi wa Udahili katika Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU). Nachotaka niseme ni kwamba; naomba karne za Upotoswaji zifike mwisho. Mnachokifanya kwangu mnanionea na sijui mnamaslahi gani na uonezi huu.
Prof. Rwekaza Mkandala anapotosha umma waziwazi kwamba kosa kuu la Lusako ni kurudi kusoma shahada ile ile kinyume na sheria ambayo inataka mtu aliyefukuzwa asisome shahada ile ile mpaka baada ya miaka minne(4). Maneno haya hayajasemwa na Prof. Rwekaza Mkandala peke yake, yameungwa mkono pia na Mkurugenzi wa Udahili Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Dr. Kokuberwa Mollel ambaye pia kapotosha umma kupitia gazeti hili kwamba, kosa lake ni kurudi kusoma kozi ileile ambayo alikuwa nasoma mwanzo na pili anadai kwamba kisheria Lusako haruhusiwa kusoma kozi ileile baada ya miaka minne.
Ukweli ni kwamba, Lusako hajawahi kurudi kusoma kozi ile ile ya mwanzo. Kwa mujibu wa Nyaraka zake nilizojiridhisha wakati wa mahojiano naye. Lusako Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa Masomo 2009/2010 akisomea shahada ya Uhasibu (B.com Accounting) na sasa aliomba kusoma shahada ya Sheria na Uchumi kozi ambazo hajawahi kusoma hapo awali, Lusako akachaguliwa kusoma Shahada ya Uchumi, kwa kuwa dhumuni la Lusako lilikuwa Kusoma Sheria, aliomba kuhamia kitivo cha Sheria(UDSoL) na akakubaliwa kwa sababu ya kukidhi vigezo. “Hata ningerudi kusoma Shahada ya Uhasibu kwa mujibu wa hoja yao(Prof. Rwekaza na Dr. Mollel) bado ningekuwa na sifa kwani nimekaa mtaani kwa takribani miaka mitano(5) inaelekea sita(6) sasa. Nasikitika kwamba hata TCU ambao ndio waliokuwa msaada kwangu wameungana na dhambi ya upotoshwaji anayoifanya Prof. Rwekaza Mkandala” alisema Lusako.
Sababu anazozitoa Prof. Rwekaza Mkandala juu ya kufukuzwa kwangu katika gazeti la The Citezen ni tofauti kabisa na sababu walizoziandika katika barua yangu niliyokabidhiwa. Nashtushwa na hili. Nimekabidhiwa barua kwamba Nasimamishiwa Udahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa sababu nimedahiliwa kimakosa na nipo kinyume na Sheria ya Udahili ndani ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam(Reg.12) inayoeleza kwamba mwanafunzi mwenyesifa ya kurudi Chuo ni Yule pekee aliyedisko kwa sababu ya kuvunja taratibu za mitihani. Sheria hii ipo kinyume na Sheria mama Universities Regulation 43 (1) GN. 226 inayotuba haki ya kusoma baada ya miaka miwili kama sababu ya kufukuzwa ilikuwa makosa ya kinidhamu.
Mkurugenzi wa Udahili TCU amekili kwamba Lusako hakudahiliwa Kimakosa na kusisitiza kwamba anasifa ya kuwa Mwanafunzi wa UDSM ila kosa lake ni kurudi kusoma kozi ilele ile. Hivyo ndivyo Prof. Rwekaza Mkandala na Dr. Kokubelwa Mollel walivyoamua kupotosha taarifa kwa malengo yao binafsi. Nazani Mtanzania Utajiuliza kwa nini Prof. anapambana sana kuzika ndoto za Lusako Kielimu?, Prof. ana maslahi gani na Kutosoma kwa ndugu yetu Lusako mpaka kufikia hatua ya kutoa taarifa potofu waziwazi na tena kwa makusudi?. Binafsi ninamengi ya kujifunza katika sakata hili nitawajia tena nitapopata undani wake baada ya tafiti za kina.
Lusako anasema; Prof . Mkandala amepotosha umma kwamba, yeye aliitwa kuhojiwa katika kamati za nidhamu ndani ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Huu ni upotoshwaji mkubwa kwa umma kupitia gazeti hili. Lusako amefanya jitihada za kidiploasia hata kuandika barua rasmi takribani mbili ya kuomba kurejewa kwa maamuzi ya kufukuzwa kwake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kuishauri Tume ya Vyuo Vikuu kutomdahili tena katika Vyuo vya umma. “Niliona napokwa haki yangu ya kusoma mchana kweupe, niliona watawala wakitumia mabavu ya madaraka yao na mtandao walionao katika wizara ya Elimu kuhakikisha sipati haki yangu ya kusoma. Namuomba Prof. Rwekaza arejee barua mbili walizonijibu. Tar. 27.04.2012, nilijibiwa barua hii yenye kumbukumbu no. 2009-04-00256, yenye kichwa cha habari “ NOTICE OF COUNCIL DECISION” ikisisitiza kwamba Baraza la Chuo limeshathibitisha kwamba umefukuzwa Chuo.” Alisema Lusako katika Mahojiano naye.
Lusako anasema; Niliendelea kufanya diplomasia ili viongozi wengine wanisaidie, kwa ushauri wao waliniomba niandike tena maombi ya kuomba kurejewa kwa adhabu. Naomba nimkumbushe Mkandala, Tar 28.12.2011 nilijibiwa barua yenye kumbukumbu No. 2009-04-00256 yenye kichwa cha Habari “NOTICE OF INTENTION TO APPEAL” Ikisisitiza kutotuma tena barua katika Baraza la Chuo kwa hoja kwamba Baraza la Chuo (UDSM) ndilo lenye maamuzi ya mwisho “The Council of University of Dar es Salaam are final and conclusive and therefore not subject to appeal within University Procedure. Barua zote hizi anazo. Sasa hoja ya ndugu, Prof. Rwekaza Mkandala kwamba nilisikilizwa katika kamati ya nidhamu imetoka wapi?.
Prof. anatoa hoja kwamba Sikuandika barua ya kuomba Msamaha na anasisitiza niombe msamaha katika makala hii. Ninaomba niliweke wazi juu ya hili. Sioni kosa langu wala dhambi kubwa niliyoitenda ndani ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2011. Ninaona thamani kubwa kwa kusimamia haki za wanafunzi wanyonge ndani ya taifa hili waliotaka kupoteza haki zao za kusoma kwa sababu ya uhuni wa mikopo hewa. Siwezi kushusha utu wangu eti kwa sababu watawala wanataka nifanye hivyo. Nimelinda utu wangu kwa takribani miaka sita(6) sasa pamoja na changamoto nyingi ninazo zipitia. Prof atambue kwamba, Binafsi sihitaji huruma kutoka kwake au Baraza la Chuo bali nahitaji nipatiwe haki yangu ya kikatiba ya kupata elimu katika Udongo wa nchi hii.
Namuomba Prof. Rwekaza Mkandala atambue kwamba mimi bado ni kijana na bado napambania ndoto ninayoiota ya kusoma Shahada ya Sheria, bado ninandoto kubwa na taifa langu, aniache nisome nije kulisaidia taifa. Namuomba pia asitishe Chuki, visasi na misimamo isiyojenga taswira njema yakwake na Chuo (UDSM) kwa Ujumla wake. Namsisitiza kutawala Chuo Kikuu UDSM kwa Mujibu wa Sheria za nchi hii na si kwa Chuki, visasi na utashi wake binafsi. Narudia kusema kwamba Chuo kikuu cha Dar es Salaam ni Chuo Kikuu cha Umma, ni Chuo Kilichojengwa na kodi za Watanzania. Hivyo kila Mtanzania mwenye sifa ana haki ya kusoama chuo hiki bila kubaguliwa.
Naamini wakati Utafika nitasoma na kutimiza ndoto zangu kielimu alisema Lusako.