Midas Touch
Senior Member
- Jan 23, 2008
- 187
- 200
- Kwanza nakupongeza sana Prof. wangu pale UDSM miaka ya 90s kwa kuteuliwa kati ya wengi kuiongoza Wizara ya Elimu. Pia nampongeza Dr. Magufuli kwa kukuteua.
- Nimesoma gazeti la Daily News la January 1, 2016 ukurasa wa kwanza na kuendelea uk. wa tatu kuhusu agizo lako ukiitaka TAASISI YA ELIMU TANZANIA vitabu VILIVYOIDHINISHWA vifikishwe mashuleni kabla ya tarehe 13/1/2016. Hili ni agizo zuri sana kuendana na kasi Mh. Rais Magufuli kuelekea ELIMU BORA na ya bure kwa maana hiyo. Peruzi kiambatanisho hapo chini,
- Kama Waziri wa Elimu, Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) hawajakupa habari kamili na za uhakika ili utoe maamuzi sahihi kuhusu hali ya vitabu na usambazaji wake.
- TIE hawana vitabu. Hata vile vya KKK darasa la I-II hawajakamilisha utayari wake ili vitumike mashuleni.
- Private Publishers/Wachapishaji binafsi ndio wenye vitabu vilivyoidhinishwa kuanzia chekechea hadi sekondari na vyuo vya elimu.
- Usambazaji vitabu mashuleni unafuata sheria ya manunuzi kupitia Government Procurement Services Agency (GPSA) kupitia wasambazaji walioidhinishwa (Authorized Booksellers/Distributors) na GPSA.
- Authorized Booksellers/Distributors wana mikataba hai na halali kati yao na GPSA (Hadi 2017) kuhusu usambazaji wa vitabu vilivyoidhinishwa vya Publishers/Wachapishaji katika shule na vyuo za/vya serikali. Kila mzabuni (Authorized Bookseller/Distributor) anayo orodha na bei ambatanishi kuhusu vitabu vilivyoidhinishwa vya Publishers/Wachapishaji vitakavyopelekwa mashuleni.
- TAMISEMI kitengo cha Elimu ndio kinachohusika na mpango mzima wa kusambaza vitabu mashuleni na vyuoni kwa mujibu wa sheria kupitia GPSA.
- TAMISEMI (Elimu) wanawasiliana na Private Publishers/Wachapishaji binafsi kupanga mkakati wa ununuzi wa vitabu na kisha usambazaji wake kupitia Authorized Booksellers/Distributors walioenea kila wilaya nchini. Unaweza kupata orodha ya Authorized Booksellers/Distributors kutoka GPSA. Mpangilio huu unaendana na sheria ya "Public Private Partnership (PPP) iliyopitishwa na Bunge letu hivi karibuni.
- Ni kweli kuwa TIE wanatakiwa kuandika vitabu vya shule, lakini itachukuwa muda mrefu sana kukamilisha shughuli hiyo kwa shule za chekechea, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. Hii ni kuzingatia ukweli kuwa kwa sasa TIE wako katika mchakato wa kuandaa Mtaala mpya, na itachukua muda mrefu mtaala kukamilika ndio uandishi wa vitabu vipya uanze na kukamilia hadi mika kama saba ijayo. Mtaala wa sasa ni ule uliorekebishwa mwaka 2005. Kila baada ya miaka 7, kitaalamu kunafanyika "Curiculum review", sasa ni miaka 10 imepita...!
- Kwa sasa, vitabu vya Private Publishers vilivyoidhinishwa ndivyo vitaendelea kutumika hadi huo mtaala mpya utakapokuwa tayari, ndipo vitabu vipya vianze kuandikwa na ku-phase out kila kitabu kilichoko shuleni kwa kasi ya kitabu kimoja kwa kila darasa kwa mwaka mmoja. Kwa shule za msingi itachukua miaka 7 na kwa sekondari itachukua miaka 6..! THINK BIG PLEASE.
- Hata kama TIE itaandika vitabu vya shule na vyuo vya ualimu ili kuwa na mtizamo wa universal single textbook hapa Tanzania, kimantiki TIE itabaki kuwa Author tu kwani kazi iliyobaki itafanywa na Private Publishers (To publish), Printers (To print) na Distributors (To distribute). Ndivyo biashara ya vitabu inavyoendeshwa duniani kote. Hii inaendana na sheria ya PPP kawa nilivyoeleza hapo juu.
- Wahusika wanatakiwa wakupe mtiririko sahihi kuhusu hali ya vitabu nchini ili utoe uamuzi sahihi. Haiwezekani agizo litolewe tarehe 1/1/2016 hadi 13/1/2016 vitabu viwe vimefika mashuleni. Leo ni tarehe 17/1/2016. TIE hawana vitabu hivyo . Wakisema wanavyo, itakuwa miujiza..!
- Wewe ni Prof. tunakutakia kila la kheri katika Wizara ya Elimu na hatutasita kukupatia habari sahihi zaidi ili kufanikisha kazi yako kwa faida ya wote.
- Kaimu Mkurugenzi wa TIE Bw. Fentu anatakiwa akueleze ukweli. Siku chache zilizopita kaimu huyo alidai kuwa makontena 9 ya vitabu yamekwama bandarini, hakutoa sababu. Eti printers wa vitabu hivyo walivi-print India wakati kampuni hizo ziko Pugu Road! Kampuni hizo ni Jamana Printers na Tanzania Printing Services (TPS).
- Wabane hao NECTA urudishe division zetu 1,2,3,4 na 0. Huyo Mkurugenzi wa NECTA kama alipata maelekezo kutoka JUU akabadilisha mfumo wa division kuwa GPA, ajue kuwa "He diluted his professional standard! HE MUST GO.