Prof. Ndalichako: Ni ipi nafasi ya elimu ndani ya taasisi za elimu?.

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,008
2,000
Salam!
Wadau nimekuwa nikipata taabu sana ,hasa nikijiuliza hivi Elimu inapaswa kusimamiwa kwa hekima,umri,uzoefu ama kisayansi,kisera na kisheria.

Kumekuwa na Sera nyingi mfano Sera ya Elimu ya mwaka 2014/15.Ambayo sidhani kama wadau Wa Elimu wanaijua vizuri hasa walimu. Sasa sjui kwanini tuliandaa kama nchi?

Pia Kumekuwa na tatizo lingine mtu alichosomea hakifanyii kazi? Mfano mtu kasoma Early childhood education, ila anafundisha secondary au mtu kasomea Education in psychology anafundisha civics na kwa njaa yake anakubali.

Sasa unajiuliza hivi hawa wataalam kwanini tunawahamisha kwenye fani zao mama,ambazo sjui hazhtajk tena au la ?na kuwachepushia maeneo mengine,mfano ninae jamaa yangu alimaliza uhasibu japo alkuwa in service , alirudi kazini kwake anaendelea kufundisha Geography na mathematics, hata uhasibu wa shule kapewa mtu asiye na Elimu ya uhasibu. Ni mwaka wa nne tangu ahitimu hiyo degree yake, hajawahi fanya kazi za kihasibu katika taasisi yake.

Lingine la Viwango vya Elimu ,katika kusimamiana, mfano prof anasimamiwa na PhD hii ieleweke ni katika mktadha wa Elimu ya profession moja. (professional wise)

Haya nenda huko chini ndo utacheka kabisa , mkuu wa shule ana diploma anawasimamia wenye degree ,Sasa hapa unafkr nini kitatokea,kama sio kusimamia lesson plan bla kukagua kilchoandkwa ndani kwa hofu ya mgogoro wa kiuelewa?

Kubwa zaidi ni hawa waratibu Elimu ,wengi ni form four ,wanaopaswa kuwasimamiwa waalimu wenye diploma na degree mpaka masters katika kata zao , wengi wa waratibu hawa hata vikao wamekuwa hawezi kuita hofu ni likiibuka jambo linalohitaji utaalamu,linaweza kuwaletea fedheha kubwa ,wanaona ni bora wasiitishe vikao hivyo.Yaani hakuna vikao vya kitaaluma,

Swali hivi ni ipi nafasi ya Elimu ktk taasisi za Elimu, maana sidhani kama Nesi wa kawaida anaweza kumsimamia mganga mfawizi,iweje kwenye Elimu iwezekane.?. Na miongozo ipo kipi kinawawea kigumu kutekeleza ?

Au tuazime mifumo jeshini,ili upande cheo Latima kuwe kuna juhudi umefanya,sio kuwepo jeshini tu. Kwa mtazamo wangu Elimu yetu ndo eneo liloachwa lichezewe vya kutosha.

Samahani kama kuna yeyote nmemkwaza!

Nawasilisha kwa heshima!
 

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,242
2,000
Nadhani kuna haja ya kupitia upya sera na kanuni au taratibu zilizowekwa katika sekta hii ya elimu na mambo ya ajira ama vyeo vya ualimu.

Ila binafsi,katika masuala ya kiutawala sidhani kama kuna tatizo mkuu wa shule kuwa na diploma then kusimamia au kuongoza wenye degree.utendaji wa kazi na uzoefu ndo vitu muhimu sabu hiko ni cheo cha kiutawala tu na si taaluma sana.kazi ni mkuu wa shule kusimamia shughuli au kuongoza taasisi na kuiwakilisha vema.
 

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,008
2,000
Nadhani kuna haja ya kupitia upya sera na kanuni au taratibu zilizowekwa katika sekta hii ya elimu na mambo ya ajira ama vyeo vya ualimu.
Ila binafsi,katika masuala ya kiutawala sidhani kama kuna tatizo mkuu wa shule kuwa na diploma then kusimamia au kuongoza wenye degree.utendaji wa kazi na uzoefu ndo vitu muhimu sabu hiko ni cheo cha kiutawala tu na si taaluma sana.kazi ni mkuu wa shule kusimamia shughuli au kuongoza taasisi na kuiwakilisha vema.
Uhalali wa kusimamia au msingi wa hicho cheo ni nini?,vp unaweza kuwa na mkuu wa shule asie na Elimu?
 

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,242
2,000
Uhalali wa kusimamia au msingi wa hicho cheo ni nini?,vp unaweza kuwa na mkuu wa shule asie na Elimu?
Sifa ya kuwa mkuu,wa shule ni lazima uwe mwalimu so kwa kuwa unakuwa na elimu bhas n dhahiri ni lazima uwe nayo.
 

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,008
2,000
Sifa ya kuwa mkuu,wa shule ni lazima uwe mwalimu so kwa kuwa unakuwa na elimu bhas n dhahiri ni lazima uwe nayo.

Kaka kuwa mkuu wa shule ,ni lazima uwe umesomea ualimu, ila kuna ka -inferiority complex unakokuwa nako.

Ni kusaidie au nkukumbushe tu ,miongoni mwa kazi za mkuu wa shule ni pamoja na kuangalia namna mwalimu au walimu wanafundisha kimbinu, ki zana ,nukuu za somo na usahihi wa kinachofundishwa kwa niaba ya serikali,

Hivyo ujue hawa vijana waliohitimu vyuo wako bookish zaidi ,ukitoa wazo uwe na source ya uhakika.Hapo ndo wakuu huhis wanadharauliwa ,hatimae huamua kuwa passive ile siku ziende tu.
 

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,242
2,000
Kaka kuwa mkuu wa shule ,ni lazima uwe umesomea ualimu, ila kuna ka -inferiority complex unakokuwa nako . Ni kusaidie au nkukumbushe tu ,miongoni mwa kazi za mkuu wa shule ni pamoja na kuangalia namna mwalimu au walimu wanafundisha kimbinu, ki zana ,nukuu za somo na usahihi wa kinachofundishwa kwa niaba ya serikali, Hivyo ujue hawa vijana waliohitimu vyuo wako bookish zaidi ,ukitoa wazo uwe na source ya uhakika.Hapo ndo wakuu huhis wanadharauliwa ,hatimae huamua kuwa passive ile siku ziende tu.
Point ni hyohyo kwamb,vigezo awe mwalimu na uwezo wa kuongoza ndio maana hupatikana miongoni mwa walimu hao hao bila kujali level ya elimu.so miongoni kuna wanaofaa na wasiofaa kuwa wakuu,kingne lipo kwenye masuala ya madaraja yao walimu jinsi wanavyotofautiana.
 

Brightfame

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,159
2,000
Haina tofauti na mbunge aliyeingia bungeni kwa sifa ya Kujua kusoma na kuandika halafu anakuwa na last say kwenye jopo la wasomi.
 

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,008
2,000
Kwa sasa sifa za kuwa mkuu wa shule ni degree holder (secondary) kwa mwalim wa primary ni kuanzia diploma, mratibu Elimu kata ni kuanzia degree
Hili ndo nlkuwa nazlngumzia hapo juu lipo kwenye Sera ya Elimu na miongozo mbalimbali ya Elimu,lkn je wakuu wa idara wanaljua hilo?, au waziri analkumbuka hilo?
 

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,008
2,000
Tafadhali moderator ,msiundoe kwenye trending mpaka wadau wa Elimu wachangie Mawazo yao . Nchi hii inamambo mengi sio siasa tu kila wakati
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom