Prof.Ndalichako:Mitaala ya elimu hii iko sawa?

Prof.Ndalichako:Mitaala ya elimu hii iko sawa?

Mbekenga

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2010
Posts
3,257
Reaction score
8,178
Wana JF naomba kutoa hoja yangu na michango yenu iifikie Wizara ya Elimu. Nimepokea wanafunzi na wahitimu ili wafanye mazoezi ya vitendo na nikagundua kuwa mitaala ya elimu haitajenga nchi. Nikafikiria kwamba ningekuwa kiongozi kama Prof.Ndalichako ningebadili mitaala ya elimu ikawa na sura ifuatayo:
  • Shule za misingi zituondolee ujiga tujue kusoma, kuandika, kuhesabu, kujua jiografia ya nchi, mila, desturi, rasilimali za nchi n.k
  • Shule za Sekondari, vyuo na vyuo vikuu vijenge wanafunzi kama rasilimali watu kwa matumizi ya kurithisha shughuli za kujenga nchi.
Mfano:
-Shule/Chuo kihakikishe kuwa kila mwanafunzi awe na shamba, duka, genge, hospitali, karakana, mahakama, kiwanda, mitambo, misitu, mto, ziwa, mnyama, mgodi, (ambacho ni mali ya chuo au ashikishwe kwa mtu mwenye taasisi binafsi mtaani) ambapo atahudhuria kipindi chote cha masomo. Mwanafunzi afundishwe sheria na Sera za taaluma hiyo. Hapa mitaala ingeruhusu mijadala ya makosa yaliyokwisha fanyika kwenye sheria, mikataba na sera za taaluma hiyo kusababishia hasara kwa mtu binafsi au nchi ili yaepukwe.

Mtu anasoma miaka 7 msingi, miaka 4 sec, miaka 2 chuo au 6 sec na 3 chuo lakini akifika ofisini ni stori tu. Naona tunahitaji mageuzi ya elimu si lazima tukae na mitaala ya kikoloni, mambo yanabadilika. Nimeandika kwa ufupi ili wana jukwaa tuongezee kadri ya jinsi mnavyoona vijana wanakuja ofisini kuanza kazi.
 
Naunga hoja mkono.

Ngoja nisubiri maoni ya wadau
 
Back
Top Bottom