Prof. Ndalichako amvaa Makonda

KWAKO KATIBU MKUU, WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA UFUNDI, NIELEZE JE, UMERUHUSU NYONGEZA YA ADA KWA SHULE BINAFSI? TAYARI ADA IMEPANDISHWA MWAKA UJAO. KA SHULE KA MSINGI PALE MLIMBA KAMETANGAZA ADA KUWA NI 1,800,000.00 KWA MWAKA KUTOKA 1,600,000. TOA MAJIBU HARAKA
 
Kwanini msiwahamishe? Kwani lazima shule hiyo? Biashara huria siku hizi.
Running from the from does not mean that you are solving.Ukisema wawahamishe wattoto wao huo ni ubinafsi maana watoto wengine watakuja kuzulika na hayo mafundisho kama wazazi wangekaa kimya
 
Nimesoma haya maelezo yaani inaonekana kuna jambo..yote sio kweli hata kidogo kwa sababu zifuatazo.
  • hakuna penalty inayotozwa kwa kuchelewa kulipa .mie watoto wangu wpo hapo na sijawahi kulipishw afaini hio japo kuchelewa kulipa.
  • hii ni shule ya Kishia, na inafundisha madhehebu yao . kama shule za kasabato zitafundisha kisabato na shule zs kisuni zitafundisha kisuni. huo ni ukweli haupingiki. hapa ni fitna zinapangwa
  • mbali ya somo la dini kwa wanafunzi ambao sio waislam hawasomi somo la dini bali kwa wanaotaka wanasoma moral study
  • hili la almuntazir lilianzia na Wabunge wa CHADEMA Bungeni wakati wa kujadili fees za shule za binafsi wao ndio walizua Uwongo kwa chuki zao za waislam . na serikali wakalichukua kama issue kumbe wanataiwa mtegoni.
  • wazazi wanao lalamika ni feki , hawapo ila kuna kikundi maalum kimepangwa kwa lengo la kuziua hizo shule., wizara itoe ushahidi wa barua za wazazi hao kama kweli waliwahi kutozwa faini
  • Shule hizi zipo chini ya Shia Ithna asheri Trustees na shule zina Bodi zinazo julikana kama Central Education Board na ndio inayo simamia masuala ya shule
  • Azim Dewji sio Mkuu wa shule wala mjumbe wa bodi ya shule . Azim ni Rais wa Jumuiya ya Mashia Tanzania..
  • ada za shule hizi bado zipo chini ukinganisha na ada nyengine za shule zenye hadhi kama Almuntazir, shule nyingi aina hii zinatoza zaidi Million 7 kwa mwaka
  • nina imani kubwa huu mgogoro umepangwa na baadhi ya watu njee ya shule ambao wana chuki na Shule za kiislam ili kuona shule hii inapigwa vita na kuimaliza .
  • hawa sio wazazi nakataa kabisa kabisa kwani kwa mwaka kuna utaratibu wa mikutano kati ya Uongozi na Managemnet na hakuna wakati wowote kwa mzee kulalamika , au kutoa rai ya fees. wengi wanaridhia kwani shule hizi wanajitahidi katika kutoa elimu na wanaridhika na vifaa vinavotolewa shuleni. hivyo ni dhahiri hawa ni wazee feki na tunaiomba hawa wazee wachunguzwe vizuri na kuangalia suala hili lilifika vipi kwa Wabunge wa Chadema na kulitilia fitna bungeni. Kuna siasa na udini wa chadema pia.
  • haiwezekani kwa wabunge wa chadema waje na hili huku wakijua shule zao kule Arusha na Moshi ni ghali mnoo lakini kwa sababu wansoma watoto na wanapata elimu nzuri basi hawataki wenzao wapate
 
Running from the from does not mean that you are solving.Ukisema wawahamishe wattoto wao huo ni ubinafsi maana watoto wengine watakuja kuzulika na hayo mafundisho kama wazazi wangekaa kimya
Nothing involves running over there. We tend to create unnecessary story. The school has been existing for over forty years with so many children and now parents who went to the same school sending there. It is now normal in our society to fabricate stories and accusations. Never heard of the religion that teaches sodomy.
Wazazi si wajinga kiasi kile. Watu hupenda kuzua. By the way, there are so many schools that perform better than Al-Muntazir.
 
Leo Makonda kampiga marufuku waziri,kama mh Magufuli ataendelea kumpongeza bila kumkemea kwa baadhi ya mambo mabaya anayoyafanya mwisho na yeye atapigwa marufuku na Makonda.
...sasa kama maconder kesha sema kabisa kuwa aliposimama yeye ni Mungu ndo kasimama we huoni tayari keshajipaisha juu zaidi ya magu..
 
Choko choko zilanza hapa kutoka hotuba ya chadema bungeni. Ilijaa chuki kwani Tatizo la ADA Chadema waliliona kwa shule hii ya Kiislam tu. Kule Moshi na Arusha zipo shule zinatoza mpaka 20 million na kila mwaka wanaongeza lakini Chadema waka single out AlMuntazir schools.
Naamini hii shule ingekua ya Mangi hii wasingesema..


Serikali na Waziri kuweni Macho mnagombanishwa na waislam . Hao wazee inawezekana ni wazee wa Chadema…



Hii ni sehemu ya hotuba kwa ufupi

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI MHESHIMIWA SUSAN ANSELIM JEROME LYIMO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17.

UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kuchukua fursa hii, kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sote uhai na kutuwezesha kuliona Bunge la 11 tukiwa salama. Pili napenda kumshukuru kwa dhati kabisa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (Mb) kwa imani kubwa aliyo nayo kwangu kwa kuendelea kuniteua kuwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa vipindi vitatu mfululizo. Ninaahidi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, na kwa hakika sitaiangusha Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika wajibu huu niliopewa wa kuisimamia Serikali katika sekta ya Elimu nchini.

Mheshimiwa Spika, naishukuru familia yangu ikiongozwa na mume wangu Boniventure Ngowi na wanangu wote. Kipekee namshukuru sana Naibu Waziri wangu Dr. Suleiman Ally Yussuf kwa ushauri wake. Vilevile nawashukuru sana BAWACHA Mkoa wa kichama wa Kinondoni kwa kunichagua kuwawakilisha hapa kama kawaida sitawaangusha.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napenda kuwapongeza viongozi wote wakuu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kwa kazi kubwa na nzuri walioyoifanya ya kuwaongoza watanzania kuchagua mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakemea kwa nguvu zote na inaitaka Serikali kuacha mara moja tabia hii ya kuingilia shughuli za kikanuni za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa kutumia mgongo wa Bunge.
ELIMU YETU NA HATMA YA TANZANIA
Mheshimiwa Spika, dhambi kubwa na mbaya kuliko zote kuwahi kufanywa na Serikali hii ya CCM ni kuwanyima Watanzania elimu bora; kupandikiza elimu nyepesi, potofu na tegemezi kwa vizazi vingi vya taifa hili; dhambi ya kuwachanganya na kuwavuruga watoto wa Taifa hili kwa sera dhaifu, mitaala isiyo na dira na vitabu visivyokuwa na tija kwa maendeleo yao na ya Taifa lao.

Mheshimiwa Spika, Nchi yetu ipo hivi ilivyo kwa sababu ya elimu duni. Umaskini, ujinga na maradhi vinavyotesa Taifa hili ni matokeo ya elimu mbovu iliyotolewa na Serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 55 tangu tupate uhuru. Taifa linalotoa elimu bora halifanani hata kidogo na jinsi Tanzania yetu ilivyo.

Mheshimiwa Spika, hizi ni zama za kuelezana ukweli, hata mkitufungia humu Bungeni wananchi wasituone Live bado Ukweli utaendelea kupasua kuta za Bunge hili na kuwafikia Watanzania. Mwanafasihi mashuhuri wa nchi yetu, Afrika ya Mashariki na Barani Afrika, Hayati Shaaban Robert, katika kitabu chake cha KUSADIKIKA aliandika hivi, Msema kweli hukimbiwa na Rafiki zake, nikipatwa na Ajali kama hiyo sitawaonea Wivu wale wanaodumu na marafiki zao siku zote. Siwezi kuikana Kweli kwa kuhofia Upweke wa kitambo na kujinyima Furaha ya milele inayokaribia kutokea baada ya kushindwa kwa Uongo mwisho wa kunukuu. Maneno haya ndio msimamo wangu na wa Kambi kwa ujumla wake, kwani siku zote wabunge wa Upinzani tumeonekana kama maadui na kunyanyapaliwa na Serikali hii ya CCM kwa sababu kusema ukweli kuhusu madhaifu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, nchi zilizoendelea zinafanya mambo mengi ya kimaendeleo kwa kuwatumia wataalam wao wa elimu ya juu University graduates. Wataalam wa vyuo vikuu wanatengenezwa kwa kutegemea pia elimu bora ya msingi na sekondari. Tanzania nayo ina vyuo vikuu. Lakini leo ipo haja ya Bunge hili kujiuliza nini hasa maana ya Chuo kikuu A University is an institution of higher learning where people's minds are trained for clear thinking, for independent thinking, for analysis and for problem solving at the highest level, is the centre for advancing the frontiers of knowledge". Kwamba: Chuo Kikuu ni taasisi ya elimu ya juu inayoandaa watu kuwa na fikra pevu, fikra huru kwaajili ya kuwa na uwezo mkubwa wa kiuchambuzi na kwaajili ya kutatua matatizo kwa kiwango cha hali ya juu, ni kituo cha kuendeleza maarifa.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa na Mawaziri wengi tu waliopita vyuo vikuu, lakini bado wameliingiza Taifa hili kwenye hasara kubwa kwa maamuzi mabovu, kwa kuingia mikataba isiyojali maslahi ya taifa na kwa utendaji usio na ufanisi. Hivi hawa wana-fit kweli kwenye definition hii ya Chuo Kikuu? Ukweli ni kuwa hata Serikali yenyewe haiwaamini wataalam wake wanaozalishwa na vyuo vikuu hasa kwenye Sekta ya Sayansi na Teknolojia. Na hili lipo wazi; leo Tanzania ina madini, gesi na mafuta, lakini watafiti, wachimbaji na wavunaji wakubwa wa raslimali hizi, wenye mashine kubwa na za kisasa, na zenye kutumia teknolojia ya hali ya juu si Watanzania.

Ajira mpya ziingizwe kwenye payroll mapema ili kuondoa kero ya kucheleweshwa kwa maslahi ya walimu kutokana na majina yao kutokuwepo kwenye payroll.

UKIUKAJI WA KATAZO LA SERIKALI LA KUONGEZA ADA KWA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI KWA MWAKA WA MASOMO 2016
Mheshimiwa Spika; Pamoja na mkanganyiko uliopo kuhusu ada elekezi na katazo la Serikali la kuongeza ada kwa shule zisizo za Serikali kwa mwaka wa masomo 2016, zipo baadhi ya shule zisizo za Serikali zimeendelea kuongeza ada kwa mwaka huu wa masomo 2016 na kwenda mbali zaidi kuwatoza wazazi faini ya hadi shilingi laki moja kwa kuchelewa kulipa ongezeko hilo ndani ya siku saba.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo taarifa kwamba shule ya awali ya AL MUNTAZIR UNION NUSERY SCHOOL ya Dar es Salaam imeongeza ada kutoka shilingi 1,580,000/= mwaka 2015 hadi kufikia shilingi 1,980,000/= mwaka 2016 sawa na ongezeko la shilingi 400,000/=. Aidha, shule ya msingi ya AL MUNTAZIR BOYS PRIMARY SCHOOL ya Dar es Salaam imeongeza ada kutoka shilingi 1,820,000/= mwaka 2015 hadi shilingi 2,480,000/= mwaka 2016 sawa na ongezeko la shilingi 460,000/=
Mheshimiwa Spika, pamoja na barua mbalimbali zilizoandikwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar na Kamishna mwenyewe ambayo kopi yake tunayo bado shule hii imeendelea kukaidi. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kujua, hii shule ya AL MUNTAZIR inapata wapi nguvu ya kukaidi maagizo ya Serikali waziwazi? sambamba na hilo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa msimamo wake kuhusu katazo lake la ongezeko la ada kwa shule zisizo za Serikali, na namna inavyolisimamia utekelezaji wa agizo hilo.

UPANGAJI WA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na changamoto ya muda mrefu ya upangaji wa matumizi katika sekta ya elimu. Mara zote upangaji wa bajeti ya sekta umeshindwa kuzingatia uwiano unaokubalika kati ya matumizi ya kawaida na yale ya maendeleo. Uchambuzi wa bajeti ya wizara unaonesha kuwa kati ya shilingi bilioni 897.6 za bajeti ya Wizara zilopangwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo, shilingi bilioni 427.5 ambazo ni sawa na asilimia 47.6% zimepangwa kwa ajili ya kugharamia mikopo ya elimu ya juu.
Mheshimiwa Spika, athari ya kupanga fedha za mikopo katika bajeti ya maendeleo ili bajeti ya maendeleo inaonekane kuwa kubwa lakini kimsingi fedha inayokwenda kutekeleza miradi halisi ya maendeleo ni kidogo sana na hivyo kutokidhi mahitaji.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inahoji, kama mkopo wa mafunzo ni uwekezaji kwa nini bajeti za mafunzo ya maofisa wa Wizara (Training domestic na Training outside) yako kwenye bajeti ya Matumizi ya Kawaida? Mafunzo kwa ajili ya walimu 7000 wa sayansi na lugha katika kasima 4001 ya SEDP yako katika bajeti ya matumizi ya kawaida. Kwa nini bajeti ya mafunzo ya Program 20 kasima ndogo 2001 ambayo ni shilingi bilioni 3.9 na Program 70 kasima ndogo 7001 yako kwenye bajeti ya matumizi ya kawaida? Upangaji huu wa bajeti ni kushindwa kuwa na msimamo unaowiana na hii husababisha miradi mingi ya maendeleo katika sekta ya elimu kutotekelezwa.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuwa na vigezo vya bajeti ya maendeleo katika wizara hii tofauti na ilivyo sasa ambapo fedha zinazoonekana dhahiri kuwa ni za matumizi ya kawaida zinawekwa kwenye bajeti ya maendeleo ili bajeti iungwe mkono wakati ki-uhalisia hakuna maendeleo yenye tija yatakayofanyika kutokana na upungufu mkubwa wa fedha za maendeleo.
Mheshimiwa Spika, kama Serikali inadai kwamba mikopo ya elimu ya juu ni fedha za maendeleo kwa kigezo kwamba huo ni uwekezaji kwenye maendeleo ya rasilimali watu; basi

Mheshimiwa Spika, napenda kumalizia hotuba yangu kwa kusema kwamba, sera ya elimu bure ilianzishwa na CHADEMA. Ipo katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA chini ya mwavuli wa UKAWA tangu mwaka 2005, 2010 na hatimaye 2015. Lengo lilikuwa ni kutoa huduma ya elimu bure kwa ukamilifu wake kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu. Maigizo ya ilani ya CHADEMA yaliyofanywa na CCM, yameishia kuondoa ada tu na michango midogomidogo ya uendeshaji wa shule hadi kidato cha nne tu, huku kukiwa na sintofahamu kubwa juu ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika shule hizo. Hali hii inapelekea kuporomoka zaidi kwa elimu.
Mheshimiwa Spika, kuna msemo usemao, ‘If education is expensive try ignorance’, tafsiri yake ni kwamba; kama elimu/ kuelimika ni gharama basi jaribu ujinga. Tanzania tumeamua kujaribu ujinga, kwa kutowekeza vya kutosha katika elimu na ndio maana elimu yetu imeporomoka na kufikia hapa ilipo.
Mheshimiwa Spika, Waziri wa Elimu katika awamu ya kwanza Marehemu Jackson Makwetta alisema kwamba: Tanzania ni kama mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungia zimefika lakini hajifungui, hivyo Tanzania inahitaji mabadiliko vinginevyo itaendelea kudidimia kielimu na kiuchumi. Kwa sababu hiyo; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuutazama upya mfumo wa elimu sasa kwa kuunda tume maalum ya kuupitia upya na kutoa mapendekezo ili Taifa liweze kuwa na mfumo bora wa elimu unaokidhi viwango vya kimataifa.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha.

Susan Anselm Jerome Lyimo (Mb)
WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUDI

26 Mei, 2016
 
Yaani shule inafundisha watoto "ikiwa mkeo yuko kwenye hedhi basi unaruhusiwa kumwingilia kinyume na maumbile" 😡

Shenzi kabisa.
toba, Mungu wangu tutasalimika hiv kwel.....
 
Ndiyo maana IS ni watuhumiwa wa urafiki na Saudia Arabia (Sunni) na Saud Arabia ni rafiki wa chanda na Pete wa US, na US mshabiki mkubwa wa makundi yasiyochukia dhambi ya kinyume na maumbile!!!chain ya hatari hii!!
 
nimesoma al muntazir sijawah sikia hicho kitu, shame on ur stupid thinking
Kwa nini unam attack afrodenzi ? kwani yeye ndiyo hao wazazi walioenda kulalamika kwenye gazeti la Jamhuri?
Watu kama ninyi ndiyo wale mlisoma hapo lakini mliokua hamuelewei hata kinachofundishwa, na hata mwalimu wako wa darasa labda ulikua haumfahamu.
Kingine ni kwamba hata sisi wakati tunasoma kuna mengi tlikua hatujawahi kuyasikia lakini watoto wa kike walifundishwa na kati yao wengine hawakuwahi kuyaelewa.
 
Kama Mzazi Unaona Ada ni kubwa hamisha mwanao mambo ya kulaumu kwamba ada imepanda acheni
 
Jibu la huyu ndugu la "Utafuatilia mangapi na magazeti yanaandika kila siku?" Pia "Serikali huwa tunawasiliana nao kwa barua siyo magazeti" lina maana sana.
 

Kama kuna mwenye reference ya hiko kitu hapo naomba anipe.
 
Nimesoma habari yote nimegotea hapa " Hawa wamiliki wa shule za Al-Muntazir tulilalamika kwa waziri kuwa wanafundisha watoto wetu katika mtaala kuwa ikiwa mkewe yupo kwenye HEDHI basi dini yao inaruhusu mume kumwingilia mkewe KINYUME NA MAUMBILE "

eeh wajameni naombeni mnisaidie hapo kwa kweli sijaelewa
 
Yaani shule inafundisha watoto "ikiwa mkeo yuko kwenye hedhi basi unaruhusiwa kumwingilia kinyume na maumbile" 😡

Shenzi kabisa.
Whaaaat hrbu nifafanulie vizuri tafadhali
 
Sasa nimeelewa ni kwa mini wanawake wa kule wanapenda sana kutatuliwa marinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…