Prof Mwandosya - Afya yangu ipo fiti

Prof Mwandosya - Afya yangu ipo fiti

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,474
Reaction score
45,048
AZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, amewaeleza Watanzania kuwa baada ya kuugua kwa muda mrefu hivi sasa afya yake imeimarika kwa kiasi kikubwa na anasonga mbele kuwatumikia wananchi kwa ujumla.

Mwandosya aliyasema hayo jana Mbeya wakati akitoa salamu kwa wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Viwanja vya Bustani ya Jiji mkoani hapa, baada ya kumalizika kwa matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho.
Maandamano hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

"Si mmeniona jamani afya yangu imeimarika hivyo kilichobaki ni kuchapa kazi na kusonga mbele katika kuwatumikia Watanzania," alisema Mwandosya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki.

Kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya na sasa afya yake imerudi katika hali ya kawaida na kuwapa moyo wapigakura wake, ambao kwa muda walikuwa na wasiwasi kutokana na kuugua kwake.

Mbali na Mwandosya pia viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Taifa Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Godfrey Zambi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Mbeya, Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe na viongozi wengine walishiriki matembezi hayo.

Matembezi hayo yaliyoanzia Soweto saa 1.30 na kumalizika saa 2.15 asubuhi, wananchi walijitokeza kwa wingi na wengine wakisimama kandokando ya barabara huku wakionesha kushiriki pamoja na viongozi na wanachama, wakereketwa wa CCM.

Awali, wananchi waliopata fursa ya kuzungumza na gazeti hili kuhusiana na hali ya kisiasa mjini hapa walisema kuwa kwa mara ya kwaza haijawahi kutokea wananchi hao kujitokeza kwa wingi katika sherehe za Chama hicho, kutokana na upinzani wa kisiasa uliokuwepo.

Source: majira.co.tz
 
Naona dalili za ccm nyingine kuzaliwa hapa'
 
Ila tunakushauri uendelee kupumzika, usije ukaanza mchuano na kina EL.
 
"Si mmeniona jamani afya yangu imeimarika hivyo kilichobaki ni kuchapa kazi na kusonga mbele katika kuwatumikia Watanzania,"

Maneno haya yananikumbusha maneno aliyosema Sokoine huko nyuma baada ya kupumzishwa Uwaziri Mkuu kutokana na matatizo ya kiafya. Baada ya hapo Nyerere alimrudisha tena kwenye uwaziri mkuu, hadi kifo kilipomkuta.

Katika Chadema, wapo watu ninaowaheshimu sana kutokana na mapenzi yao kwa nchi yetu Tanzania, na huko CCM mmojawapo wa watu ninaowaheshimu sana ni Prof. Mwandosya.

Kama kuna mtu amewahi kumsikia Prof. Mwandosya akitoa kauli za kitoto kuhusu vyama vya upinzani, kama ambazo nimezisikia toka kwa watu kama Mwigulu, Wasira na hata Mkapa, tafadhali anifahamishe.
 
Huyu hata vijana wa LUMUMBA hawamjui ufanisi wake. Ukiwapambanisha Prof. Mwandosya na Capt. Komba, lazima watampa kura Capt. Komba.
 
Asije akaanza tena kampeni za ubunge!!!! Kweli demokrasia inaruhusu ila hakika pumzika mjomba. Kula pensheni yako taratibu. Mshukuru Mungu kwa uzima hadi leo but dot overwork yourself. Na mbaya zaidi achaneni na makundi ya kisiasa, hayawasaidiii tena kwa sasa umri na ugonjwa vinagoma.
 
Huyu hata vijana wa LUMUMBA hawamjui ufanisi wake. Ukiwapambanisha Prof. Mwandosya na Capt. Komba, lazima watampa kura Capt. Komba.
Mimi nikiona jina lako tu nakumbuka mambo ya ajabu sana.
 
Waliomwekea sumu yeye na Mwakyembe wapo humohumo CCM na inawezekana kabisa mwenyekiti wao anawajua lakini cha ajabu bado wanashabikia chama ambacho wauaji wao wapo humo.
 
Maneno haya yananikumbusha maneno aliyosema Sokoine huko nyuma baada ya kupumzishwa Uwaziri Mkuu kutokana na matatizo ya kiafya. Baada ya hapo Nyerere alimrudisha tena kwenye uwaziri mkuu, hadi kifo kilipomkuta.

Katika Chadema, wapo watu ninaowaheshimu sana kutokana na mapenzi yao kwa nchi yetu Tanzania, na huko CCM mmojawapo wa watu ninaowaheshimu sana ni Prof. Mwandosya.

Kama kuna mtu amewahi kumsikia Prof. Mwandosya akitoa kauli za kitoto kuhusu vyama vya upinzani, kama ambazo nimezisikia toka kwa watu kama Mwigulu, Wasira na hata Mkapa, tafadhali anifahamishe.

Prof. Mwandosysa ni mtu mwema sana ni Mtanzania kwelikweli.
 
waziri asiyekuwa na wizara maalumu! anakula tu kodi za watanganyika bila kazi yoyote! hovyooo.
 
Back
Top Bottom