Prof. Muhongo vs mh. Mp pinda+ dr. Jm kikwete

Prof. Muhongo vs mh. Mp pinda+ dr. Jm kikwete

tangaraha

Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
51
Reaction score
9
Waziri anayehusika na madini prof. s muhongo kapotoka sana, anashambulia makundi ya watz bila hata chembe ya busara. Alianza kule mlimani city dhidi ya wadau wa madini/nishati, akaja kulishambulia 'shirikisho' la sekta binafsi nchini na karibuni hapa kawashambulia viongozi wa dini.
Natoa wito (kama inawezekana) afundwe tena kuhusu uongozi wa umma, asipojirekebisha ataingia kwenye daftari la mawaziri wa hovyo kabisa aliyejikitika kulopoka hovyo waliowahi tokea Tanzania. Kapewa uwaziri sababu ya kaka yake wa damu..................................................................................
Kauli yake kwamba mikataba ya nishati na madini ipo wazi inapingana na kauli ya waziri mkuu pinda aliyowahi itoa bungeni kwamba mikataba ni 'siri',
Kama mishipa ilivyomtoka wakati anawashambulia wale viongozi wa dini zote kwamba mikataba ipo wazi basi namuomba atoe hata hints za mikataba ya karibuni kati kikwete na serikali ya china ili watz wajue.
Mwisho kabisa nitoe wito kwa waajiriwa wa kuitetea serikali hapa jf kwamba wapunguze unazi, kauli za prof. muhongo ni tatizo. Katika hali ya kawaida huwezi anzisha mgogoro usio na tija na viongozi wa dini, hata mtu aliyehudhuria kozi ya wiki moja ya political science anajua kwa nchi kama tz taasisi za kiislam na kikristo zinanguvu sana kisiasa. Sitegemei prof, waziri anaweza warushia makombora yasiyo na tija viongozi wa dini. Msaidieni mlio karibu nae.
 
Back
Top Bottom