Prof.Muhongo Ulipwaji fidia kwa wakazi wa nyamongo utekelezwe

mkurya org.

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
1,571
1,694
Wanajamii na watanzania kwa ujumla huu utakuwa ni mwendelezo wa uzi utakaokuwa unazungumzia ulipwaji fidia kwa wakazi wa Nyamongo na naomba wahusika wasiufute au kuuhamisha,

Yapata sasa Ni karibia miezi mitatu tangia Waziri wa nishati na madini prof. Muhongo kuja huku nyamongo kwa ajili ya kushughulikia kero mbalimbali zikiwemo ulipwaji wa fidia kwa wakazi wa mji wa Nyamongo wanaozunguka mgodi wa Acacia uliopo Mkoa wa mara wilaya ya Tarime,

Hiyo ni baada ya waziri kuja huku akiambatana na Mbunge wetu John Heche kuja kusikiliza kero mbalimbali zinazotuhusu,

Kwa hiyo alikuja na akaelezwa kero zetu zote na kaamua kuunda tume ya kushughulikia hayo matatizo ,

Na baada ya tume kuundwa na ripoti ya tume kutoka mpaka saivi Mh.yupo kimya sana na hatujui nini kinaendelea na hamna hatua zozote hata moja zilizochukuliwa na viongozi wa serikali au wizara husika ikiongozwa na Mh Prof.

Kuhusiana na hii kero ya muda mrefu inayotutatiza wakazi wa Nyamongo wananchi wameanza kutomwamini mh.mhongo na serikali kwa ujumla kwa ahadi alizozitoa wakati alipokuja huku ,

Na ilifikia hadi kipindi Gazeti la mwananchi likaandika Wananchi wa Nyamongo kunufaika na fidia zao mwezi wa nne tarehe 11 na hiyo ni baada ya ripoti ya tume ya kushugulikia matatizo kukamilisha ripoti ,

Lakini tangia siku hiyo hatujawahi kusikia chochote kikitamkwa Na uongozi wa Wizara na serikali husika mpaka saivi,


TUNAMUOMBA SANA MH.MUHONGO WIZARA YAKO NA SERIKALI KWA UJUMLA KUSHUGHULIKIA HILI TATIZO MAPEMA KWANI WANANCHI WAMEANZA KUTOKUWA NA IMANI NA SERIKALI YAO ,,

I MEAN TUMECHOKA SANA NA UONGOZI ULIOPO NA TUNAOMBA UTEKELEZAJI NA SIO MANENO MATUPU.
 
Back
Top Bottom