Prof. Muhongo: TANESCO haiwezi kulipa madeni kwa kupandisha bei ya umeme

Gazeti LA serikali
 
Hivi kwanini tusifanye kama South Korea.Kwanini hawa walugaluga wanatuchukulia sie maboya?.Wakati yule mama wa NIMR anatangaza ishu ya zika waziri wa afya alikuwapo lakini baadae akamkana mwenzio kama yuda eskarioti alivyomkana yesu.Leo huyu profesa ndumilakuwili naye anajifanya eti hajui mchakato mzima wa EWURA.sasa hawa mawaziri kazi zao nini haswa kama hata swala coordination na mashirika yaliyo chini yao wanashindwa.hopeless kabisa
 
Anaandika Dr Onesmo Mhadhiri Kitivo cha sheria UDSM.

Swala la bei ya umeme ni siasa uchwara. Kuna wakati wanasiasa wanakuwa kama watoto, eti wanasema bei ya umeme haitapanda ili tuone kuwa serikali inawatetea wananchi kitu ambacho si kweli. Utaratibu wa kupandisha umeme upo hivi. TANESCO inaandika mapendekezo na sababu za kutaka kupandisha umeme. Mapendekezo hayo yanapelekwa EWURA. Ewura inafanya inquiry kwa kushirikisha wadau wote wakiwemo serikali, vyama vya walaji, wafanyabiashara nk. Baada ya hapo inatumia wataalam wao kuangalia kama kuna sababu za kukubali ombi la kupandisha bei kama lilivyo au wanaweza kukubali kiasi fulani au wakakataa. Baada ya kutoa maamuzi kama kuna mtu hajaridhika ikiwemo serikali inatakiwa kukata rufaa Fair Competition Tribunal. Na wangeweza kuomba temporary injunction kuzuia kutumika bei mpya. Kwa hiyo si kweli kwamba serikali haijaona hiyo writing ya sababu za kupandisha umeme na Waziri hana mamlaka ya kuzuia maamuzi ya EWURA. Mimi kama mwananchi ninafurahia umeme kutopanda lakini tusipofuata utaratibu wa sheria tunazidumaza taasisi zilizopewa mamlaka ya kutoa maamuzi. Utawala wa sheria ni muhimu sana katika ustawi wa nchi. Ni maoni yangu tu. Happy new year.
 
Kama Waziri asingeweza kuchukua hatua kwa taarifa za kusikia, alisubiri aletewe taarifa rasmi ofisini lakini mkurugenzi hakufanya hivyo,
 
Mkuu hivi umeelewa mantiki ya mtoa mada au unatoa tu povu?

Mtoa mada anamshangaa waziri anaposema wanachi hawatalipa madeni ya Tanesco, wakati huo huo anasema serikali itakopa kulipa madeni ya Tanesco, huo mkopo utalipwa na nani kama sio wanachi kupitia kodi?

Wewe unadaiwa, unasema huwezi kulipa deni kwa hela ulizonazo benki ila utalipa kutoka kwenye hela uliyotunza nyumbani,hapo unakua na unafuu gani katika kulipa hilo deni au anakua amelipa mtu mwingine tofauti na wewe?

Uwe unaelewa kwanza mantiki(Logic) kabla hujatokwa na mapovu.
 
Waziri hapewi taarifa ya tanesco kupandisha bei kwa magazeti.
 
Bora uende kazini maana umezidi uongo na unafiki, swala na bonus lilishasemwa siku nyingi na prof.
 
Nimesoma mahala...kuhusu utaratibu.

Tanesco hupeleka maombi EWURA, kisha EWURA hutisha vikao vya kukusanya maoni ya wadau, kisha maoni hayo hupitiwa na EWURA kisha UWURA huitaarifi Wizara, kisha Wizara (Serikali) huidhinisha, kisha UWURA huutangazia umma.

Huu
ndio utaratibu unaopaswa kufuatwa.

Kilichofanyika.......

Tanesco walipeleka maombi EWURA ya kupandisha tarriff, kisha EWURA wakaitisha vikao vya kukusanya maoni ya wananchi (wadau), EWURA haikupeleka ripoti ya mchanganuo wa maoni ya wananchi kuhusu gharama hizo Wizarani, EWURA ikapanga ongezeko na kuutangazia umma.

Waziri kwa kuona utaratibu umekiukwa akaiandikia EWURA juzi kupinga maamuzi yao na kusimamisha upandishaji huo.

Nionavyo Mimi;

Makosa hapo sio ya Tanesco bali ya EWURA. Tanesco hawana mamlaka Ndio maana jana nilipoiona ya kupandisha bei.

Nilipoisoma ile barua jana nikasema kama umeandikiwa barua halafu cc zikapelekwa kwa watu hao waliopelekewa itabidi ukeshe ukiomba kikombe hicho kikuepuke.

Nilijua tu wangeosulubiwa hapo ni Uongozi wa EWURA. Hasa nikirejea kilichotokea majuzi sakata la Zika (same like utaratibu tu ndio haukufuatwa). Bahati mbaya jumba bovu limemuangukia Mhandisi Mramba.

In short; Mkurugenzi wa EWURA ni usajili mpya wa Mkuu, ila mhandisi wa Tanesco ni usajili wa Baba Riz 1, labda kigezo kilichozongatiwa ni hicho.

By Robert Mugabe
 
Kila mtu ni mnafiki, mnafiki!
Hata sisi yaani wananchi ni wanafiki walipotangaza bei ya umeme itapanda tulilia waziri aingilie kati tanesco wasipandishe. Leo ameingilia kati tunasema waziri mnafiki.
Watanzania nadhani ndio watu wanaongoza kwa unafiki duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…