Prof Muhongo ni MUONGO au ANATANIA!!


LAPROFESERI JAMANI TULIENI NDIYO TANZANIA HII 1+1=11 NOT 2 :yell:
 

Mkuu, hakika ukipenda chongo utaita kengeza!

Kweli kwa profesa wa sayansi ya miamba, ambaye vipimo vya urefu ndiyo lugha yake asijue sentimeta ni kitu gani hadi akichukulie kama kipimo cha ukuaji wa uchumi halafu useme eti ulimi umetereza bila kutilia shaka???!!! Hakika TZ haiishi vituko.

Kweli inawezekana msomi kama daktari wa tiba, aseme joto la mgonjwa huyu ni juu sana kiasi cha kufikia kilogramu 45!!!, halafu aseme ulimi ulitereza, nawe kama zuzu ukubali bila kutilia mashaka? Mhh, hapo kazi ipo.

Nakumbuka tukiwa wadogo tunasoma shule za msingi na upili, tulipata kudokezwa kwamba ukiona mwalimu wenu ni mkali sana na au ana mbwembwe sana akiwa darasani, basi ujue huyo mwalimu ni mtupu kichwani, na anaficha kasoro zake kwa stahili hiyo.
 
Elimu yake haikumsaidia sana, mbwembwe zake zinakera na tayari ameshalewa madaraka! ..nashangaa bunge limekuwa siasa, anabaki anaweweseka na ccm, kuna kipindi pia ilisema "hoja za upinzani na hoja za ccm"? ...sipati picha na sielewi maana yake!
Unaweza kuwa msomi lakini uwezo wako wa kutafakari nakuukubali ukweli ukawa duni!!!!!!!!!
Hawa wamezoea taarabu na mipasho, ...a lunguage which a gentleman cannot speak very well! ....taarabu? ...mipasho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…