Prof. Muhongo ampiga dongo Zitto Kabwe(?)

Muhongo 2015!


HAKUNA KITU HUYU NI MSOMI MTENDAJI ANAYEPENDA KUONA RESULTS. YEYE MWENYEWE NINA HAKIKA HATAKI KABISA HAYA MAMBO YA SIASA. Ningetamani Semunyu amuulize hilo swali kipindi kijacho tusikie. Sitashangaa akisema kuwa yeye si mwanasiasa. Kweli sasa tunaona umuhimu zaidi wa kutenganisha ubunge na uwaziri kwenye katiba tunayoitengeneza!!!
 
Tatizo la mzee nae ana dharau sana,ushauri asipokee kwa sababu hauna tija lakini sio kwa vile umetolewa na mtu ambae hajasoma petroleum geology

kama ana dharau,asingesema atapeleka rasimu ya sera ya gesi kwa kwa ajili ya kupata maoni kutoka kwa makundi yote ya watumiaji wa gesi bila kujali elimu yao,atapeleka pia kwa vyuo vinavyofanya tafiti,kwa wataalamu mbalimbali,miji mikubwa yote yenye viwanda dar,mwanza na arusha.

kama ana dharau,nahisi itakuwa kwa wale wanaomdhihaki...au walio kwenye payroll ya kumdhihaki...
 
Tusipojenga taifa la kuheshimu taaluma za watu tutaishia kuwapeleka Mabwepande....

Hivi Chenge si mtaalamu, ni lini mlimdharau, nipe matokeo ya kumheshimu.
kwa kuwa huwezi sema, nakwambia amewatia ....
 
Tusipojenga taifa la kuheshimu taaluma za watu tutaishia kuwapeleka Mabwepande....
Asante mkuu, Mimi ningesema tumejenga taifa lisiloheshimu taaluma ndiyo maana wengi wameishia na wataendelea kuishia Mabwepande.......
 

Pamoja na maelezo marefu naomba nikukumbushe kuwa wanaolalamika kuhusu umeme sio wabunge ni wananchi, wabunge ni vipaza sauti vya wananchi.

Pili naomba ufafanuzi hapa; kama muhongo anasema hawezi kusililiza mawazo ya wenye certificate of participation iweje tena atumbie amepeleka rasimu kwa wananchi ili watoe maoni yao kuhusu sera ya gas kabla haijawa sheria?

Anakataa ushauri wa watu wenye access na information anasubiri maoni ya watu ambao hata umeme hawana. Prove kwamba hii sio contradiction.

Prof. kaniangusha bana, ameulizwa jinsi tanesco ilivyojiandaa kupambana na hujuma akasema wao hawapigi propaganda ni vitendo zaidi, badala ya angalau kutumegea kidogo jinsi walivyojipanga, lakini baadaye akaanza kutaja njia mpya za umeme wanazojenga (kwa maelezo yake). Hili jibu nalo ni la kimkakati kama ambavyo angejibu swali la kwanza. Contradiction nyingine.

Pia amezungumzia huduma za tanesco kwa kusema eti zimekuwa bora zaidi, akatoa mfano kwamba sasa hivi kama umeme utakatika meneja wa eneo husika lazima atangazie eneo lake na kama umeme unakatika ghafla basi lazima awaombe radhi waathirika.

Acha tu prof. Apewe ushauri bana
 
Last edited by a moderator:
U-Prof...haukupewa u deserved to be and i consider u as an ASSET na mwenye utashi wa kusimamia kazi kimisingi yake, tenda kazi achana na midomo ya wapenda short-cut. Mungu akujaze nguvu na hekima.
 
Mikataba mibovu tuliyo nayo kwenye madini ndio 2tegemee mpaka kwenye gas na mafuta! hivi waziri wa nishati na madini kuna umuhimu gani wa kuchimba uranium? wakati hatuwezi kuepuka madhara yake? madini athari 2meshindwa kushughulikia? tafadhari 2naipeleka wapi nchi ye2 yenye resources za kutosha? kuwa makini waziri hiyo secta ni muhimu kwa uchumi wa tanzania!!
 
Huyu mzee anaonekana ni mchapakazi, kwanza siyo mwanasiasa na anaonekana kumtetea mtz wa kawaida!
 
waziri wetu una mpango gani au serikali yako ina mpango gani wa kupeleka umeme kwenye baadhi ya vijiji mikoani ambako hawajawahi kuona umeme unafananaje katika maisha yao? its amazing 2012 kuna watu hawajawahi kuona taa ya umeme maishani mwao
 
Prof. Muhungo amejaribu kuonyesha vision yake kuhusu umeme na gas. Tumpe muda kabla ya kumfanyia evaluation. Kumbukeni siasa zetu zilivyoiharibu TANESCO.
 

Mkuu hapa umenyoosha mambo vizuri sana. Na umenikumbusha niliwahi kumsikiliza Jenerali Ulimwengu wakati wa mjadala wa Katiba mpya, uleeee wa wanza kwanza. Alikuwa anashangaa siasa zetu zilivyo za ajabu. Aliuliza inakuwaje wanapokutana wakuu wa Wilaya ambao ni maaskari wastaafu walioteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya wanapokuwa na vikao, maana wengine ni ma-Luteni, wengine ma- Captain wastaafu sijui ma Major wakichanganyika na Raia wengine nk. Sasa heshima inakuwaje humo ndani ya Kikao? (sijamnukuu 100% lakini ndiyo hoja aliyoijenga).
Sasa Prof. Muhongo atachakaa muda si mrefu pale atakapopewa vikwazo na Mkuu mmoja wa Mkoa au Wilaya. Labda awe amewekeana special MoU na Mkuu wa nchi.
Hakuna shaka kabisa kwamba Siasa mbovu ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo. Nchi yoyote duniani ukiona wanasisa wake ndiyo wanaolipwa mishahara minono kuliko watu wa taaluma ujue hiyo nchi haiwezi kuendelea. It simply is practicing silly Politics, which will take the country nowhere! Badala yake uchumi ni lazima udidimie na maisha ya wananchi wake hayataweza kuwa mazuri hata siku moja.
Nchi ya namna hiyo utakachoona ni viongozi kutaka maendeleo ya vitu vichache vya kujiletea sifa binafsi, kujenga barabara, madaraja, majumba makubwa nk. huku wakiua vile vilivyokuwepo kabla hawajaingia madarakani. That is what I call silly politics.
 

Nimeona nikuwekee hii kitu ujipime wewe na huyo muhongo mnafiti namna gani.

“A word to the wise ain't necessary, it's the stupid ones who need the advice.” by bill cosby.
 
Ebu badili heading yako mwenzio nikaenda ITV nkakuta mziki umeniboa
Ila nashukuru kwa kunikumbusha icho kipindi maana uyu mheshimiwa huwa namkubali sana he is a professional not a politician
kuwa waziri ni sifa tosha ya kukufanya kuwa mwanasiasa maana cheo chenyewe ni cha kisiasa. i only say, within politicians are professionals.Vilevile muwe makini na huyu profesa asiyependa kushauriwa maana mafuta na gas ni mali ya watanzania na ajue watanzania si wote wamesoma na waliosoma wote hawajasoma kuhusu miamba. lakini wanao uhuru na haki kikatiba kuhoji mambo yanayoendelea. jiulize kama mwili wote ungekuwa jicho sikio lingekuwa wapi? ajue hata aliyemteua si mtaalam wa gesi je nae asihoji?watanzania lini tutaacha kuchukulia mambo kishabiki tukaanza kuhoji?
 
Profesa aelewe kwamba si kila mtu atakuwa mtaalam wa kila kitu. Lakini hali hii haimuondolei yeyote yule haki ya kutoa maoni. Professa elewa kwamba watu wanao uhuru hata chini ya katiba ya sasa ya kutoa maoni kuhusu mambo yaendavyo katika nchi yao. Hii ni "fundamental right" ya kila raia, mtaalam na asiye mtaalam. Ninachokiona kwa profesa ni "intellectual arrogance."

Prof. Muhungo elewa kwamba ni juu yako na "the so called wataalam" kutafsiri na kuweka katika lugha ya kitaalam yale ambayo raia wa kwaida anayatoa kama maoni yake.

Prof. ndio maana kuna hata kura ya maoni ambayo inawahusisha wataalam na hoi hahe kama sisi. Nchi hii na rasilimali zake ni kwa wote na sio kwa wataalam. We are not children ambao wazazi watusemee.

Kiongozi tena mwenye hadhi ya Waziri anatakiwa kuelewa mambo haya na hasa lugha anayotumia kwa umma.

Nampenda Mbunge Msigwa anaposema " Anapozungumza Profesa huoni tofauti na mtoto wa darasa la pili". Tuweke mbali ushabiki wa kisiasa na tukubali "constructive criticism". There is no one with a monopoly of ideas on how to run the national economy. Certainly it cannot be the so called experts who have put this country in a hopeless situation through dubious deals and agreements signed as related to the exploitation of our mineral wealth.

By the way professor where are the Tanzanian experts with the necessary experience in the gas sector, anyway? Book knowledge, oh come on professor, you are not serious! Aren't we sailing in the same boat?

Good luck!
 

prof amesema rasimu ya sera ya gesi wataipeleka kupata maoni kwa wananchi bila kujali elimu na kwa wataalamu pia ,vyuo mbalimbali n.k...sasa hapendi kupata ushauri katika muktadha upi? kama kupiga dongo la cheti cha mahudhurio ya wiki moja,hicho ni kijembe kwa wale wanomdhihaki...kikundi cha wanaomdhihaki(kama ukiwa kwenye nafasi yake ,hata wewe ungefanya hivyo)...na walengwa wa kijembe hicho wanajijua...wewe vipi inakuumizaje? pilipili usiyoitafuna,inakuwasha vipi? kama angesema hatatoa nafasi kwa watanzania kuchangia kuhusu rasimu, ungetakiwa ikuume na si kijembe kidogo alichotoa kwa watu wanaokesha kudhihaki kazi anazofanya kwa kuwa wao wanajiona wamebobea kwenye sekta hii ya madini na wanamwona waziri ni mtu wa kuja...tafuteni darubini muone mbali kama macho hayatoshi....
 
hapendwi kushauriwa katika lipi ?
prof amesema rasimu ya sera ya gesi wataipeleka kupata maoni kwa wananchi bila kujali elimu na kwa wataalamu pia ,vyuo mbalimbali n.k...sasa hapendi kupata ushauri katika muktadha upi?
kama kupiga dongo la cheti cha mahudhurio ya wiki moja,hicho ni kijembe kwa wale wanomdhihaki...kikundi cha wanaomdhihaki(kama ukiwa kwenye nafasi yake ,hata wewe ungefanya hivyo)...na walengwa wa kijembe hicho wanajijua...wewe vipi inakuumizaje? pilipili usiyoitafuna,inakuwasha vipi? kama angesema hatatoa nafasi kwa watanzania kuchangia kuhusu rasimu, ungetakiwa ikuume na si kijembe kidogo alichotoa kwa watu wanaokesha kudhihaki kazi anazofanya kwa kuwa wao wanajiona wamebobea kwenye sekta hii ya madini na wanamwona waziri ni mtu wa kuja...tafuteni darubini muone mbali kama macho hayatoshi....
 
Zitto tusikilize ushauri wake wa nini wakati alishauri nchi inunue haraka mitambo ya Dowans la sivyo nchi itaingia gizani wengine tulianza kumwamini... Loh: Kumbe mgao ulikuwa wa kutengeneza!

Nani alikuwa nyuma yako Zitto ukatusaliti Watanzania bila hata huruma! Shukuru sana uko Tanzania, watu wa aina yako China ungeshatiwa kitanzi.
 



Ataongea sana huyu mzee lakini udhaifu hupo palepale!
 
Muhongo huwa namkubali but sometimes nakuwa na wasi wasi naye!!! ngoja kwanza ije report ya Ngwiliz may be !!! hiz dauti nilizokuwa nazo kwake zinaweza kuisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…