CCM wanatuletea maigizo matupu kwenye hili suala! Rushwa imeshamiri kila kona ya nchi, halafu bado wanathubutu kudai kwamba wanapambana nayo.
Swali la msingi ni:
wanapambana kivipi, au wanatuzuga tu?
=============
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi Kimekuwa kikipinga rushwa na kupiga vita Rushwa hivyo anayesema CCM haizungumzi kuhusu Rushwa haijui vizuri CCM na hio imekuwa ni ajenda ya Mgombea Urais wa CCM.
Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Rushwa inapigwa Vita.