Prof Mbarawa fuatilia kodi za kampuni za ndege za nje tunadai mabilioni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Vigumu kuamini!

Mhe. Waziri nenda pale TRA ofisi zao karibu na jengo la ushirika ulizia kampuni za ndege wanadaiwa shilingi ngapi.

Mbaya una uhakika wa malipo na kampuni za hapa kwetu unakuta kampuni moja ya nje inadaiwa dola laki 2 hadi 3.

Mhe. Waziri hizi pesa sio kwamba wanatoa wao. Hizi pesa ni abiria wanalipa. Wanachofanya ni wanatumika kama YONO A.M., kukusanya kodi zetu na kuturudishia.

Unapokata tiketi kodi zetu zipo ndani kisheria, kila mwezi wanatakiwa wawe wanalipa pesa zetu walizokusanya. Kukaa na pesa zetu zaidi ya dola laki moja+ Mh. waziri. Katibu Chamuriho huu ni wizi mweupe. Wanazifanyia nini muda wote?

Mhe. Waziri, saa ya kukusanya hadi shi tano. Nendeni TCAA mkapate records zote za ndege zao na abiria wao tudai pesa zetu.

Tusibanane kwenye viduka vidogo wakati ndege za nje nyingi tunadai kodi zetu. Kamuulizeni tule tubabu cha TRA pale Ushirika.

Pamoja tunaweza! Tunahitaji ndege mbili za ATCL. Hizo pesa tunapata wapi kama sio kubana hawa kodi zetu walipe?
 
nafikiri wakati umefika jamii forum wawaalike ama waziri wa fedha au kamishina wa kodi tuwaeleze jinsi gani kodi zinakwepa serikali ina uwezo wa kukusanya zaidi ya hapo
 
Back
Top Bottom