Prof. Mazuri Katika Maktaba ya Prof. Mohamed Timamy, Takaungu

Prof. Mazuri Katika Maktaba ya Prof. Mohamed Timamy, Takaungu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
Prof. Ali Mazrui Katika Maktaba ya Prof. Mohamed Timamy, Takaungu

Leo ni siku yangu ya tatu niko Takaungu kijiji kiasi cha 50 km Kaskazini ya Mombasa njia ya kwenda Malindi.

Nimemtembelea rafiki na ndugu yangu Prof. Mohamed Khalil Timamy.

Naitazama maktaba ya Professor.

Sina msamiati wa kuieleza hii maktaba kwani ni kitabu juu ya kitabu na vitabu juu ya vitabu.

Vingine viko ndani ya mabox hayajafunguliwa.

Nimepigwa na butwaa sijui nianzie wapi.

Vitabu kila mahali vinaniita.
Nami ni rafiki na ndugu yao vitabu.

Nachukua funzo kutoka adabu njema ya kula chakula.

Unakula pale palipo karibu na wewe.

Jicho linaangukia "bound book'' - ''Ali A Mazrui Annual Newsletters No. 17."

Prof. Ali Mazrui ni mwalimu wangu wa masafa ya mbali, yaani "Distance Learning."

Nimeanza kumsoma Prof. Mazrui nina miaka 15.

Sasa Prof. ninae machoni na mkononi kila kitu kimesimama kwa upande wangu.

Nimepata kusoma siku za nyuma Newsletter ya Prof. Mazrui aliyokuwa akitoa kila mwaka.

Newsletter hii mikononi mwangu ni ya mwaka wa 1992.
Utaipenda na nafsi yako itaburudika.

Prof. Mazrui ni bingwa wa kucheza na maneno.

Prof. kaeleza mengi lakini mimi nitanyambua kidogo yale ambayo yamenigusa.

Anazungumza kuhusu "Departures" na "Arrivals," yaani nani kaondoka na nani kawasili.

Waliozaliwa na waliofariki.

Prof. Mazrui anaeleza msiba wa kaka yake, Sheikh Harith Al' Amin aliyekuwa akiishi hapa Takaungu.

Nakumbuka mara yangu ya kwanza kukutana na Prof. Mazrui, Kampala mwaka wa 2003 nilimfahamisha kuwa nimefika kwao na nimeuona msikiti wao wenye umri wa miaka 400 na kisima chake.

Jana niliutembelea tena msikiti huu ambao niliuona kwa mara ya kwanza mwaka wa 1995.

Bahati mbaya msikiti ulikuwa umetiwa kufuli.

Prof. Mazrui anaeleza kifo cha binamu yake Sharifa Abdulla Salim ambae ni dada yake mkubwa Sal Davis.

Sal Davis kwa wengi haitaji kutambulishwa.

Bi. Sharifa katika miaka ya mwanzoni 1960 ndiyo chanzo cha nyimbo maarufu ya Sal Davis, "Makini."

Nimekieleza kisa cha nyimbo hiyo katika kitabu changu cha maisha ya Sal Davis.

Hii Newsletter ina lukuki ya mambo.

Yatosha kabisa kukomea hapa.

1755664506516.jpeg
1755664594013.jpeg

1755664627744.jpeg

1755664666601.jpeg
 
Back
Top Bottom