Prof. Makame Mbarawa: Daraja la Kigamboni litaanza kutumika 16/4/16, Utaratibu watolewa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,502
3,483
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka, amewata Wananchi wote kuanza kulitumia Daraja la Kigamboni pindi litakapoanza kutumika. Makame Mbarawa, amesema, "Ninapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la kigamboni litaanza kutumika 16/4/16 saa 12:00 asubuhi".

Kuanza kutumika kwa Daraja hili Linalounganisha Kurasini na Kigamboni Jijini Dar es Salaam, utapunguza adha ya foleni Jijini Dar es Salaam na kukuza sekta ya uchumi inayotarajiwa kukuwa kwa kasi hasa kwa Wakazi wa Kigamboni ambao walikua wanapata adha ya kuvuka kwa foleni kwenye Pantoni au Kuzunguka Kongowe kwa wale waliokuwa wakitokea Mjini.

====================

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi.

Katika siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia.

Aidha, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni. Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.

Magari yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela, Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji.

Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.

Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-

1) Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu miundombinu ya daraja

2) Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.

3) Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo hicho.

4) Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.

5) Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.

Aidha, Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.

Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga

Katibu Mkuu (Ujenzi)

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

14 Aprili, 2016
20160218072309(3).jpg
20160218072309(1).jpg
20160218072312.jpg
20160218072309(6).jpg
 
1-1.png

View attachment 338493 View attachment 338494 View attachment 338495 View attachment 338496
Kwa kulifunguwa Siku ya Jumamosi Hili daraja halina Mwisho mwema ninatabiri hivyo mimi MziziMkavu.
 
Je daraja la mto Wami tunaweza tengeneza kama hili la Kigamboni katika kipindi hikihiki cha Mheshimiwa wetu?
 
Kazi ya Alhaj Dr.Ramadhan Kitwana Dau, Mwenyezimungu akulipe kwa kutekeleza wajibu wako ipasavyo!
 
Back
Top Bottom