King'amzi changu cha Azam kimeisha na nikajikuta naangalia TBC.Jambo la kwanza walioalikwa mostly ni pro government,Lipumba,Hamadi Rashidi,Lecturer wa Udom na huo Mhalu(?).
Jambo la pili muongazaji alionekana wazi anataka majibu ya namna gani,Mwalimu Rioba hata body language ilikuwa inamsuta.kabla ya kuruhusu majibu alitoa maelezo marefu mno na kuna wakati alikuwa anakatiza.
Nilivutiwa mno na Hamadi Rashidi alikuwa anatumia lugha ya busara lakini "when you read between the lines" unamuona mtu anayetaka mabadiliko.
Mwalimu Rioba achukue muda kuangalia clips za "Hamza Kasongo hour" au Jenerali on Monday" kutoka channel ten.Atapata mawili matatu ya kujifunza.