Prof. Lipumba: Uhaba wa sukari umesababishwa na Rais Magufuli

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
Akihojiwa na Mtangazaji Yvonne Kamuntu kwenye Azam News, Mchumi mbobezi hapa nchini Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa nchini umesababishwa na Rais John Magufuli mwenyewe kwa kuzuia sukari ya nje kutoingizwa Nchini, ilhali viwanda vyetu havikidhi idadi inayohitajika katika uzalishaji wake.

Pia Prof. Lipumba amesema hakuna sheria inayoruhusu Serikali au Bodi ya Sukari kupanga bei ya sukari nchini hivyo ametaka siasa kuacha kutumika katika mambo serious na wafanyabiasahara wasitishwe.
 
Nani amesema Rais amezuia sukari kuagizwa kutoka nje ya nchi?

Ukweli ni kwamba, Rais amezuia sukari kuagizwa holela kutoka nje ya nchi.

Kwa nini baadhi ya watu wanapotosha?

Kuna baadhi ya watu wanakuja na hoja za demand and supply kwenye product lakini wanashindwa kuelewa kuwa Rais Magufuli ana hoja ya demand and supply kwenye sugar manufacture industries.
 
Sijawahi kukuelewa na sidhani kama nitakuja kukuelewa..Sasa hapo umeandika nini?
 
Akihojiwa na Ivona Kamuntu hivi punde kwenye Azam News, Mchumi mbobezi hapa nchini Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa Nchini umesababishwa na Rais John Magufuli mwenyewe kwa kuzuia sukari ya nje kutoingizwa Nchini, ilhali viwanda vyetu havikidhi idadi inayohitajika katika uzalishaji wake.

Pia Prof. Lipumba amesema hakuna sheria inayoruhusu Serikali au Bodi ya Sukari kupanga bei ya sukari nchini hivyo ametaka siasa kuacha kutumika katika mambo serious na wafanyabiasahara wasitishwe.
huyu nae katoka wapi? Na yule Mwingine sijui katokomea wapi?

Wamwache Mkuu wa kazi Apige Kazi. Usaliti utawatafuna yeye na mwenzake.
 
Prof Lipumba ana matatizo ya uelewa, yaani ni kichwa maji ukija kwenye utendaji na siasa, yaani hajitambui.

Rais alisema kuwa wafanya biashara wasiokuwa waaminifu walitumia muanya huo wa kuagiza sukari toka nje wa kuingiza sukari zilizo isha muda wake, serikali pamoja na kulinda viwanda vya ndani pia ilifanya hivyo kulinda afya za watumiaji.

Sasa huyu na u prof wake hamna kitu, na pia nadhani siasa huyu mzee haziwezi.
 
Back
Top Bottom