Prof. Lipumba: Tanzania kwanza vyama baadaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Lipumba: Tanzania kwanza vyama baadaye

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kadogoo, Sep 23, 2010.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  WA TZ WENZANGU KWANZA NAWASALIMU NYOTE HABARINI NA NATUMAI HAMJAMBO POPOTE MULIPO KWANI HII NI MARA YANGU YA KWANZA KUJIUNGA NA MTANDAO HUU AMBAO NADHANI NI MTANDAO ULIO HURU NA UNAOKARIBISHA MAWAZO TOFAUTI TOFAUTI AU SIJUI NIMEKOSEA?

  BAADA YA KUSEMA HAYO LEO NIMESOMA POST MOJA KTK GAZETI LA RAIA MWEMA NA KWA KWELI NIMEVUTIWA SANA NA MGOMBEA URAIS WA CUF PROFESA LIPUMBA NA NAWAOMBA NA NYINYI HEMBU SOMENI SERA ZA CHAMA HICHI CHA CUF HALAFU TUJADILI TUONE KAMA KUNA CHAMA KINGINE CHENYE SERA BORA ZAIDI YA HIKI ASANTENI:


  Prof. Lipumba: Tanzania kwanza vyama baadaye

  Felix Mwakyembe
  Septemba 22, 2010

  [​IMG]
  Amshukia Kikwete na mkewe kwa matumizi mabaya
  [​IMG]
  Mikutano yake yajaa hoja za kisomi, si burudani
  [​IMG]
  Asisitiza kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

  KUNA tofauti kubwa kati ya mikutano ya kampeni za mgombea nafasi ya urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete na mgombea wa nafasi hiyo kupitia Civic United Front (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba.

  Wakati ile ya mgombea wa CCM huchukua sura ya tamasha la muziki wa kizazi kipya (maarufu kama
  fiesta) kutokana na muda mwingi kutumika kwa burudani za wasanii mbalimbali maarufu kwa wakati huu hapa nchini, ile ya CUF inachukua sura ya mihadhara ya kisomi zaidi, ikiwa imejaa hoja nzito za kitaifa kuliko burudani.

  Kutokana na sura hizo mbili tofauti za mikutano ya kampeni za wagombea hao, baadhi ya wafuatiliaji wa kampeni jijini Mbeya wanaamini kuwa ndiyo sababu vile vile ya tofauti ya idadi ya wasikiliza katika mikutano ya wagombea hao ambapo Kikwete alionekana kukusanya umati mkubwa wakati alipofanya kampeni zake mkoani Mbeya kuanzia mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa Septemba tofauti na aliopata Prof. Lipumba aliyekuwepo jijini humo siku ya Jumamosi na Jumapili.


  Wananchi waliohudhuria mikutano ya Prof. Lipumba walikuwa wachache lakini kila aliyepata hiyo bahati alionekana wazi kushiba hoja za mchumi huyo aliyebobea hapa nchini, na kama uwezo wa mgombea ndio kingekuwa kigezo kikuu cha wapiga kura, hapana shaka katika wagombea hao wawili waliopita jijini hapo hadi sasa, basi wa CUF angeibuka kidedea mkoani Mbeya .


  "Kama kuzungumza, Prof. Lipumba anajenga hoja nzito sana. Sijui tu mtazamo wa wananchi na hicho chama, lakini kwa kweli hoja zake ni nzito sana," anasema mkazi mmoja wa Jiji la Mbeya.


  Miongoni mwa hoja zilizowakuna zaidi waliohudhuria mikutano ya Prof. Lipumba, ni pamoja na ile ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ambapo msimamo wake wa kuwaingiza kwenye serikali yake Watanzania wenye uwezo na waadilifu pasipo kujali itikadi za vyama ulipokelewa vizuri na wakazi wa mkoa huo.


  Katika hoja hiyo Prof. Lipumba anasema: "Nitaunda serikali ya umoja wa kitaifa. Nitatumia watu waadilifu walioko kwenye vyama mbalimbali vya siasa. Sio kwamba walioko CCM wote ni mafisadi, wapo Watanzania wazuri tu kule, na wengine hawana vyama lakini wanashindwa kuingia kwenye uongozi kutokana na sheria zetu zilizopo."


  Anasema umasikini unaowakabili Watanzania unatokana na viongozi waliopo madarakani kukosa uadilifu ambapo katika hilo anabainisha akisema: "Ikiwa mtu anakataa serikali ya umoja wa kitaifa, basi, huyo ni ajuza; hajui analolifanya au ana nia mbaya na Tanzania."


  Imani ya Prof. Lipumba kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa inaenda sambamba na kaulimbiu ya chama hicho isemayo "Tanzania Kwanza Vyama Baadaye" ambayo nayo inaoana na ile ya "Mbeya Kwanza Vyama Baadaye," na anasisitiza akisema iwapo Zanzibar wameweza kwa nini Tanzania Bara wasiweze?


  Mgombea huyo wa CUF anaenda mbali zaidi ambapo anasema kukosekana kwa uadilifu katika serikali ya CCM ndiko kulikozaa sera mbili kuu za chama hicho anazozitaja kuwa ni ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma.


  "CCM inatekeleza sera mbili, ufisadi na matumizi mabaya ya mali ya umma. Kikwete anaongoza kwa matumizi mabaya. Ni kiguu na njia, hatulii. Ile ndege ya kifahari ya serikali anayotumia inatumia dola za Kimarekani elfu sita kwa saa kila inaporuka, posho yake, Mama Salma, na wapambe.

  Mama Salma naye ana safari zake utadhani ni Makamo wa Rais," anachambua mchumi huyo na kubainisha madhara zaidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma akisema:

  "Asilimia 30 ya fedha za serikali huibwa na wajanja wachache. Ukiwa na mapapa ya ufisadi yanamzunguka Rais, naye anaogelea nayo, huwezi kuwaletea maendeleo wananchi."


  Katika wizi huo wa fedha za serikali, Prof. Lipumba anafichua kwamba Shilingi trilioni 11.8 zimeibiwa ndani ya miaka mitano ya utawala wa Kikwete, fedha anazosema zingetosha kujenga shule bora za kata zenye maabara, maktaba na walimu; hivyo kutoa elimu bora kwa watoto wa masikini.


  Pamoja na kuunda serikali ya umoja, Prof Lipumba anaahidi kuondoa sheria zote kandamizaji, lengo likiwa kuhakikisha utoaji haki sawa kwa kila raia.


  Analitaja tatizo jingine la uongozi wa taifa kuwa ni viongozi wa CCM kutanguliza maslahi ya kisiasa zaidi kuliko ya taifa ambapo anatoa mfano wa Uwanja wa Ndege wa Songwe unaoendelea kujengwa kwamba unasuasua kutokana na dhamira ya baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho kuua nguvu ya kisiasa ya Prof Mark Mwandosya mkoani Mbeya.


  "Uwanja wa Ndege wa Mbeya haukamiliki kwa sababu ya njama za kumkomoa Prof. Mwandosya kwa sababu ndiye aliyeanzisha ujenzi wake. Wametanguliza maslahi ya kisiasa kuliko ya taifa," anasema Prof Lipumba.

  Sera ya CUF kuhusu elimu ilikoga nyonyo za wasikilizaji waliohudhuria kampeni hizo za mgombea wao urais, hususani pale Prof. Lipumba anapotamka kwamba serikali yake itatoa elimu bure kwa watoto wote nchini, kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu.

  Anaiponda sera ya elimu ya CCM; hususan kuhusu shule za sekondari za kata akisema zinajenga matabaka nchini na kuyataja kuwa ni lile la watoto wa matajiri na viongozi ambao watoto wao husoma kwenye shule za
  English Medium, au nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda na Ulaya.

  Mgombea huyo analitaja tabaka la pili kuwa ni lile la Watanzania masikini ambao watoto wao ndio hao wenye kusoma kwenye shule hizo za sekondari za kata.


  "Sekondari hizi za kata haziwezi kutuvusha. Ni sekondari za watoto wa masikini - hazina maabara, walimu wala maktaba. Leo watoto wa masikini hawapati fursa ya kusoma katika shule zenye walimu bora, maabara na maktaba," anasema Prof. Lipumba huku akiwashangaa viongozi wa CCM kudai haiwezekani wakati wao, pamoja na wazazi wao wakati ule kuwa masikini lakini walisomeshwa bure hadi chuo kikuu na hata kupelekwa nje ya nchi kwa elimu ya juu zaidi.


  Pamoja na kutoa elimu bure kwa watoto wote nchini, katika ilani yake wanayoita "Dira ya Mabadiliko au
  Vision for Change," CUF wanakusudia vile vile kutoa matibabu bure kwa wananchi wote, kuboresha afya ya mama wajawazito ili kupunguza vifo vyao vinavyozidi kuongezeka nchini kiasi cha kutoyafikia malengo ya milenia.

  Prof. Lipumba alikuwa mgombea wa kwanza hadi sasa aliyezungumzia hifadhi ya jamii kwa wazee nchi ambapo alibainisha kuwa itawahusu wazee wote pasipo kujali kama aliwahi kuwa mwajiriwa au la.


  Hoja kuhusu umasikini wa Watanzania ilionekana kuvuta hisia kali zaidi za wasikilizaji wake; hususan vijana kutokana na chama hicho kutumia vigezo vinavyojibainisha zaidi katika maisha yao ya kila siku.


  Miongoni mwa vigezo vilivyotumika kwenye mikutano ya kampeni za mgombea huyo ni pamoja na makazi na chakula duni, barabara mbovu, elimu duni na kuongezeka kwa ujinga, ambapo viongozi hao wa CUF wanabainisha kuwa inajidhihirisha kwa wananchi kugubikwa na imani potofu zinazojidhihirisha hivi sasa kwa wengi wao kukimbilia kwa waganga kwa ajili ya kupata utajiri, ajira, uongozi na tiba.


  "Maisha bora yaliyoahidiwa na CCM yako wapi? Wakati Kikwete anaingia madarakani 2005, bei ya sukari ilikuwa Shilingi 600, leo hii mnanunua shilingi ngapi?", aliuhoji umati uliomsikiliza ambao nao ulijibu kwa sauti: "Elfu mbili..!"

  kisha naye huwachoma zaidi akisema,

  Prof Lipumba aliwagusa zaidi aliposema: "Bakora za maisha magumu za CCM hazibagui, zinatuchapa wote, CCM na wasio CCM".

  Gwiji huyo wa uchumi anaichambua CCM kati kigezo cha umasikini akisema: "Ukitumia kuanzia shilingi 570 kwa siku, wewe sio masikini. Hiki ndio kigezo cha Serikali ya CCM, lakini pamoja na kigezo chao hicho cha chini bado masikini wameongezeka kwa milioni 1.5."

  Hata hivyo, ni kwa jinsi gani basi serikali ya Prof. Lipumba itaweza kuwaondoa Watanzania kutoka kwenye umasikini huo uliokithiri, kutoa elimu na afya bure, anasema:


  "Tatizo la CCM ni kwamba serikali haikusanyi kodi sawa sawa. Kwa mfano kutoka kwenye wawekezaji wakubwa wakiwemo makampuni ya madini na mafuta, tutaondoa misamaha ya kodi ikiwemo kwenye madini. Hivi sasa serikali inakusanya asilimia 15 tu ya pato la taifa, CUF imelenga kukusanya asilimia 22 hadi 25 ya pato la taifa. Katika madini tunataka serikali ichukue angalau Shilingi 300 katika kila Shilingi 1,000 na sio mrahaba wa asilimia tatu tu kama ilivyo sasa."

  Prof. Lipumba hakubaliani na kigezo cha machinga kujumuishwa kwenye ongezeko la ajira kama walivyofanya CCM. Kwamba ajira 1,300 zilizozalishwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita zimo kwenye sekta binafsi ambayo ni pamoja nawauza karanga, maji na mama lishe.

  "Serikali ya CUF itahakikisha tunazalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbali mbali vilivyopo ikiwemo makaa ya mawe ya Kiwira. Tanzania haina umeme wa uhakika, inazalisha Kilowati 770 tu. Tatizo viongozi hutumia mwanya wa matatizo ya umeme nchini kujitajirisha. Ni lazima tuwe na umeme wa uhakika ili kukuza sekta ya viwanda," anasema Prof Lipumba na kutumia mfano wa kiwanda kilichokufa cha Zana za Kilimo Mbeya akisema:


  "Kiwanda cha Zana za Kilimo cha Mbeya kikifufuliwa, kinaweza kuajiri wafanyakazi 400 ambao watalipwa mshahara wa shilingi laki tatu kila mwezi, kwa mfano. Hii ina maana kuwa Shilingi milioni 120 zitaingia kwenye mzunguko wa Jiji la Mbeya, hapa mafundi seremala watauza fanicha, mafundi nguo watashona nguo mpya sio kuweka viraka nguo zilizochakaa, mama lishe watapata wateja, kwa hiyo zaidi ya watu 2,000 watanufaika," kisha anatoa takwimu za kitaifa akisema


  "Leo hii viwanda nchini vimeajiri wafanyakazi wasiozidi 92,000 tu. Huwezi kukuza uchumi katika mazingira haya."


  Pamoja na kaulimbiu ya CUF ‘Tanzania kwanza vyama baadaye' kuwavutia wengi mkoani Mbeya, bado wananchi wanashindwa kuwaelewa viongozi wa vyama vya upinzani nchini kwa kushindwa kuelewana na kuwa na mkakati mmoja, hawawaelewi pale wanapopingana na kukashifiana, hatua wanayoibainisha kuwa inawadhoofisha na kuimarisha CCM zaidi
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  karibu sana jamvini.naomba nikuulize swali moja tu. Unamjua DR .Slaa?
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Vigezo vya usomi Tanzania haviangaliwi kwakuwa Lipumba anagombea....!!!
   
 4. Wun

  Wun JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 353
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  anamjua ndiyo maana akaandika hoja ya kisomi hata kama amecopy somewhere but inapay.
   
 5. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Huyu bwana hajawahi na wala hana calibre ya uwanasiasa,,Kipaji chake ni cha kufundisha,,ni zuruku tu ya TENDWA ndio inamfanya mpaka leo awe anasikika lasivyo angakuwa ashasahaulika. Ntawashangaa saana watakao haribu kura zao kwa kumpigia LIPUMBA
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Taratibu mkuu, hata mimi Lipumba namkubali na nampongeza kwa yote aliyofanya. Chadema waliunga mkono CUF mwaka 2000 kwa sababu hii (miongoni mwa mengine). Je ni kuomba mengi kama CUF nao wangeunga mkono CHADEMA mwaka huu?
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Sep 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama miaka yote hii tangu 1995, 2000 na 2005 watanzania hawajamwelewa Prof Lipumba, iweje leo wamwelewe na kumwamini na hatimaye kumpa kura za kutosha? Au usomi wake umeanza mwaka huu?
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu Mwafrika, ww unaelewa usitake kulitia ugumu suala la kuungana mkono, sitaki kurudia hadithi ya Tarime, miliposema ushirikiano wa vyama vya upinzani umekufa kule. Ukumbuke kuwa Prof. Lipumba alitangaza kugombea urais mapema, akachukuwa fomu na kupitishwa na chama, mda wote huo chadema haijatangaza mgombea wake urais. Hata Dr. Slaa, alishatangaza kuwa hana nia ya kugombea urais na alitangaza hadharani kutetea kiti chake cha ubunge Karatu, na fomu alishachukuwa. From nowhere as breaking news to all of us, kusikia anapendekezwa kugombea urais!

  Kilichonishangaza, kama chadema hawakuwa na mgombea urais mpaka dakika za mwisho kwanini wasimuunge mkomo Prof. Lipumba, kama walivyomuunga Mkono Maalim Seif Zanzibar?
  Au linapokuja suala la wapinzani kushirikiana, mnataka chadema mfuatwe nyinyi tu, kuwafuata wenzenu hamtaki?

  Lakini Mkuu, hilo si tatizo langu, tatizo langu ni uongozi wa juu wa chadema. Nawaambia ukweli mkitaka kataeni kuwa soon chadema ikipata Mwenyekiti asiyekuwa Freeman Mbowe, ambaye si mwanasiasa, basi chama kitafika mbali na kitapiga hatua kubwa za kimkakati na ushindi kuliko ilivyo sasa.

  Chadema katika uhai wake wote wa kisiasa tokea ianzishwe[ukiondowa waasisi wake] imekuwa na wanasiasa wawili tu wenye mtazamo wa kuona mbali kimageuzi, Mh. Zitto Zuberi Kabwe na marehemu Chacha Wangwe...kama chama hiki kingebahatika kuongozwa na mmoja kati ya wawili hawa basi leo hii JK asingelianguka jukwaani tu bali tungekwisha mzika zamaani kwa presha.
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0


  Lakini mbunge wa Tarime aliyekuwepo alikuwa ni wa chadema. Baraza la madiwani Tarime linaongozwa na chadema - je tukiwa fair, nani alitakiwa kumwachia nani Tarime? Ulitaka Chadema wamwachie CUF Tarime (ingawa wao ndio wamekamata halmashauri)?  Slaa alitangaza kutogombea, lakini chadema hawakusema kuwa hawatasimamisha mtu.  Una hakika kuwa chadema hawakuwa na mtu - kulikuwa na kina Baregu wamekaa wanasubiri tu mkuu.  Nadhani hapa unadaganya, mwaka 2000 chadema walimuunga Lipumba kwenye uraisi na Seif kule Zanzibar. Kwa nini mwaka huu CUF wasingefanya the same?  Lakini mkuu, mafanikio mengi ya chadema, yametokea chini ya uenyekiti wa Mbowe. Kwa nini unataka mtu ambaye so far anafanya vizuri atolewe?

  Wewe kina Bob Makani, Mtei na wenzake wote hujawaona tu?
  Unasema Zitto na Wangwe ukijua kabisa kuwa Wangwe ni marehemu.
  Ina maana chadema yote ile ya kina Baregu na wenzake, ni Zitto pekee anafaa kuwa kiongozi? What about Slaa kuwa mwenyekiti, umefikiria hilo pia?
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mwafrika,
  Unamwingiza Baregu wakati Dr. Slaa hakuwa na mpinzani wakati anateuliwa, au nimekosea?
  Unataka kusema kuwa CUF ingewasubiri nyinyi mutowe mgombea at the eleventh hour, ili iwaunge mkono wakati hamkuwa na yeyote aliyetangaza nia?

  Chadema imefika hapa ilipo kwa mawazo na fikra za waasisi wake (nimetangulia kusema hivyo). Najuwa Wangwe hayupo ila wakati wake angelitumika vizuri chama kingekuwa mbali. Kumbuka ni karibuni tu Zitto alitaka kuchukuwa nafasi ya Mbowe nini kilitokea unajuwa.

  Siyabezi mafanikio ya Mbowe, kifedha kweli chama kinapata ushirikiano wake. Ila kiuongozi wa siasa hafawi, yeye si mwanasiasa ni mfanyabiashara vitu hivi na siasa ni tofauti...maamuzi mengi ya kukurupuka sababu ni yeye Mbowe nani hajuwi hili?
   
 11. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watu huwa hawaeleweshwi ghafla bin zuu kwa kukurupuka brother!!, bali huchukuwa muda na pia ni muhimu kumsoma mtu kwa muda mrefu ili ujue kama kweli huyu mtu ni muadilifu? na kama tukimpa Urais anaweza kutuletea maendeleo? sasa nadhani wakati umefika wa kumpa kura Profesa Lipumba kwani ameonesha kweli ni muadilifu kwani tangu aingie CUF hajawahi kugombea ruzuku, hajawahi kukwaruzana na viongozi wenzake, huyu Profesa ni tofauti kabisa ukilinganisha na akina Dr. Slaa, Mbowe, Lyatonga Mrema, Mabere Marando, James Mbatia na wengine ktk upinzani! kwa mfano: Slaa alishakwaruzana na Zito Kabwe kwa kugombea madaraka ya uwenyekiti wakati Mbowe anagombea na Slaa akawa upande wa Mbowe, na musisahau kashfa mbaya ya kupora mke wa watu dhidi ya Slaa! ambae anakashfa nyingi tu!

  CUF ni chama madhubuti kilichopitia misukosuko mingi tangu kianzishwe lakini bado kiko ngangari! kwanza kiliitwa chama cha Wa Pemba, baadae kikaitwa cha Wa Zenji, halafu kikaitwa cha Waislamu na cha kusikitisha wafuasi wa CHADEMA ndio wako mstari wa mbele kupigia debe kauli mbiu hiyo! lakini wao wakiambiwa chama chao ni cha wachaga hawakubali!!!

  Kwa ajili hiyo tunawaomba ndugu zetu wa CHADEMA mutuunge mkono ili CUF kiunde Serikali ya umoja wa kitaifa si Zanzibar pekee bali na bara pia na kwa kauli ya Profesa amesema CUF ikichaguliwa itaunda serikali ya umoja wa kitaifa na bila shaka huwenda Waziri Mkuu akawa DR. Slaa na wanamageuzi wengine kuingia ktk serikali hiyo ya CUF! vinginevyo itabidi upinzani tugawane kura na CCM kuibuka ushindi!!! kwani CUF kina wafuasi wengi zaidi ktk mikoa yote ya ukanda wa Pwani, Zanzibar na mikoa ya kusini!! na bila shaka CHADEMA kina wafuasi wengi ktk mikoa ya Kaskazini na mikoa iliyobaki CCM wana wafuasi wengi zaidi ya vyama vingine!!

  Musidanganywe na kura ya maoni yanayotolewa na mitandao kuonesha ati SLAA anaongoza!! ni lini mitandao hiyo iliwafikia wananchi wa vijijini na kuchukua maoni yao? au inamaana maoni hayo ya wa TZ wengi wako nje ya nchi ndio inawakilisha maoni ya wananchi wote wa Tanzania? tusidanganyane kama vitoto vidogo!!!!!
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Bravo Lipumba!

  Tatizp watu mshaanza kujadili nje ya hoja na nadhani mnataka kuichakachua hii topic lol, tutajitahidi iendelee tu vizuri. Jadilini kilichomo kwenye ujumbe achana na issues za kuvuruga makusudi bana
   
 13. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0


  Kulikuwa hakuna yeyote aliyetangaza kugombea siku Slaa anaombwa kugombea.... unakumbuka hili?

  Mkuu, hii ilikuwa wazi wa lini kikao cha kamati kuu ya CHADEMA kitakaa, kila chama kina ratiba yake. Kama vile ilivyokuwa katika kuzindua kampeni, kila chama kilikuwa na ratiba yake ya kampeni. Ilitokea tu kuwa CUF walikaa kikao chao kabla ya kikao cha kamati kuu ya CHADEMA haijakaa, hii haina maana kuwa CHADEMA ilikuwa haina mgombea.

  Hoja yako ni dhaifu na hata wewe unajua hili.

  Lakini pia umesema kuwa toka CHADEMA imeanza, watu wanaofaa kuongoza ni Zitto na Wangwe (huku ukijua kuwa Wangwe ni marehemu) tu.

  Zitto aliombwa kujitoa na akakubali, kuna makosa katika hilo?

  Hapa unadanganya,
  Chadema imeongeza madiwani na wabunge wakati wa uongozi wa Mbowe. Unabisha?
   
 14. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wanaccm wanaoleta unafiki kuwa ni wapinzani huwa wanachekesha sana

  So what?

  CHADEMA iliunga mkono CUF mwaka 2000, hiyo haitoshi?

  Bwa ha ha ha
   
 15. C

  Chuma JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tangu lini Uchaguzi ulikuwa wa Haki na Usawa?...Hadi hapo uchaguzi utakapokuwa hurua na Haki ndipo unaweza walaumu watanzania....
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mwafrika,
  Nilichosema ni kuwa "watu wenye kuona mbali kimageuzi" ni Zitto na Chacha Wangwe. Kuongoza kila mtua anaweza..vipo vyama vinaongozwa na wagonjwa wa akili humu! Nimemtaja Wangwe nikikumbuka wakati wake akiwa na dhamira ya kukipeleka chama kwa wapiga kura halisi vijijini, wazo ambalo ana share na Zitto Kabwe.

  Zitto aliombwa kujitoa...Dr. Slaa aliombwa kugombea...kwa hiyo unakubalina na mimi kuwa Mbowe si mwanasiasa kwa mfano huu tu. Maana yake ni kuwa kwa chadema na akili za Mbowe, asiyetaka atake (Dr. Slaa) na anayetaka hatakiwi (Zitto)!

  Naona sasa unajigeuza geuza, ulisema akina Baregu walitaka kugombea (CUF wangesubiri tu)...saivi unasema hakuna aliyetangaza kugombea...hukumbuki vizuri Mkuu!!

  Mkuu, again unazidi kukubaliana na mimi kuwa Mbowe angefaa kwa nafasi nyingine ya chama na si Uenyekiti (pengine mtu wa mipango na fedha angefaa zaidi), kwa kuwa, mathalani, biashara ya kuata faida milioni 30, wewe unapata milioni 10, bado unaita faida? Nakubali chama kimeongeza madiwani wakati kilikuwa na uwezo wa kuongeza wabunge zaidi ya kumi majimboni.
   
 17. C

  Chuma JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni Very Low argurment kufikiri Prof Lip anaishi kwa kutegemea Ruzuku....!!! Tafuta wengine kaka
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  kwani uongo?

  BTW - ule mchongo aliopewa na ccm kule UN (kama sikosei) umeishia wapi? Talk about kununuliwa na ccm hadharani, kuna thread ilikuwa hapa JF miezi kibao iliyopita, ngoja niitafute.
   
 19. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu nakubalina na wewe 100%, ila nimegunduwa kuna watu wanakuwa na nongwa wakiona wagombea wengine wanajadiliwa, hebu angalia jukwaa la siasa lina thread ngapi anajadiliwa Dr. Slaa, tokea ugombea wake mpaka mambo yake ya siri. Leo katokea mtu, tena mgeni wa jukwaa, kwa mtazamo wake anaona Prof. Lipumba anafaa kuwa rais kwa jinsi alivyomsoma sera zake (raia mwema), watu hawataki, hii ndiyo inaniudhi binafsi na siipendi kuona hapa JF. Kama mtu lazima anataka ajadiliwe Dr. Slaa tu si thread zake zipo tele na asome tu lazima aje hapa kuharibu thread za watu?
   
 20. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0


  Haya ni maoni yako tu mkuu. Chama sio mtu mmoja, chama ni mkusanyiko wa watu. Wangwe peke yake asingeweza kuibadilisha CHADEMA. Wanachadema wote walitakiwa (wanatakiwa kushirikiana) kwenye hili.

  Wewe Zitto unamuona kiongozi bora, mimi nikimuona Zitto nakumbuka mambo ambayo sitayataja hapa kwa sasa hivi. Maoni yako peke yako sio biblia au korani. Chama ni watu, wanashirikiana kufanya mambo pamoja.

  Chadema ilikuja vijijini kabla ya Wangwe. Hivi unajua kuwa Wangwe alikuwa NCCR Mageuzi kabla ya kuhamia chadema? Unajua kuwa muda wote huo Chadema ilikuwepo Tarime. Je ni Wangwe ndiye aliyeipeleka CHADEMA vijijini kule Tarime. Au je, Ni Zitto ndiye aliyeipeleka CHADEMA kigoma?


  Sijaona point yako hapa

  Kutaka kugombea na kutangaza kugombea ni vitu viwili tofauti .. unajua hili?

  Wewe inaonekana una ugomvi binafsi na Mbowe. Mimi naona Chadema wanafanya vizuri tu chini ya Mbowe na sina tatizo na mwenyekiti wa chama. Hayo mengine ni mtizamo wako binafsi.
   
Loading...