Prof Lipumba: Nilimkaribisha Lowassa UKAWA dhamira ikanisuta,CHADEMA walitumia UKAWA kuiua CUF

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
image.jpeg
image.jpeg

Prof Lipumba amezungumza ktk kipindi cha FUNGUKA cha Azam Two kinachoongozwa na Tido Mhando.Amehojiwa mambo mengi ikiwemo sbb ya yeye kuondoka ktk UKAWA na kukaa pembeni kwa miezi 10 baada ya kujiuzulu.

Lipumba anasema akiwa UKAWA walikubaliana kuwa mgombe wa UKAWA awe Dr Slaa,na yeye alikubali kumuachia Dr Slaa ili awe mgombea wa Urais wa UKAWA.

Lakini cha kushangaza akiwa katikati ya harakati za uchaguzi,Prof Lipumba alipata taarifa kuwa Katibu wake Maalim Seif anaendeleza maongezi na Mbowe kumkaribisha LOWASSA kuwa mgombea wa UKAWA.

Akapata nafasi ya kuonana na Lowassa na wakakubaliana na Lowassa na team yake wahamie UKAWA,na yeye Lipumba alifika mpaka kwa Lowassa kwa kupelekwa na James Mbatia.

Lipumba anamshangaaa Maalim Seif inakuaje alikubali kuzungumza na CCM walioiba kura zake Mara kadhaa na hata kuua Wanachama wa CUF 2001 lakini hataki kuzungumza na Lipumba eti kisa karudi CUF kipi kibaya zaid Kati ya yeye kurudi CUF na Wanachama wa CUF kuuawa kwa Risasi za Moto lakini a kakubali Mazungumzo ?'

Anasema Magufuli na Lowassa wote walikuwa Wagombea wa CCM na hata Mganga wao alikuwa mmoja TB Joshua na baada ya Uchaguzi alikuja kuzungumza nao

Anasema Maalim Seif Hapokei Simu yake wala ofisni hafiki Buguruni sasa angemjulishaje kuhusu Kupokewa kwa Ruzuku?

Anasema Mbatia ndie aliemjulisha Ujio wa Lowassa na hata ndie alietoa Gari yake na kuamuru Dereva ampeleke Lipumba kwa Lowassa kwny Mazungumzo.

Anasema kwny Mkutano wa Wabunge wa UKAWA kabla ya Uchaguzi uliofanyika Kijitonyama Mbowe alimshambulia hadharani Lipumba kuwa anachelewesha Mchakato wa kumtangaza Slaa kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kwa Kuwa Lipumba anasubiria Makapi ya CCM na akaapa Chadema Safari ile haitokubali kapi lolote toka CCM

Baadae dhamira yake ikamsuta,maana hata kama mzigo mzito mpe Mnyamwezi lkn mzigo huu wa kumpokea Lowassa ulikuwa mzito kwa Mnyamwezi.Anakubali kuwa yeye ndio aliitisha mkutano na kumpokea Lowassa,lkn baadae akaona hataweza kumnadi Lowassa ambaye kwa muda mrefu hata CHADEMA wenyewe walimtaja kwenye "List of Shame" pale Mwembeyanga kama "fisadi" namba moja wa nchi hii.

Baadae alikuja kugundua pia kuwa Maalim Seif ndio amekuwa akifanya mazungumzo na Mbowe jinsi ya kumkaribisha Lowassa ambaye alisema atakuja na kundi la watu.Majadiliano hayo ya Mbowe na Maalim Seif hayakuwa yakimshirikisha Prof Lipumba,hivyo aliamua kukaa pembeni.

Kitu kingine alichosema Lipumba ni kuwa aliamua kuondoka UKAWA baada ya kugundua kuwa Chadema wanataka kuizika CUF huku Tanzania bara kwa jina la UKAWA.Na ameshuhudia hilo kwa kauli ya Mbowe aliyokuwa anapita ktk mikoa na kauli ya kutaka kuifuta CUF Tanzania Bara.

Prof anasema watu wanamsakama kuwa kwa sasa analindwa na dola na kuwa karibu zaidi na serikali kuliko upinzani.Kitu ambacho siko kweli,kwani kama kuhudhuria mikutano inayoandaliwa na serikali amekuwa anahudhuria hata kabla ya kuwa na mgogoro ndani ya chama.Hata ile picha ya polisi kumpigia saluti,alikuwa ni polisi wa kata ya Buguruni ambaye alikuja kwenye usafi na alikuwa anampigia saluti diwani ambaye ndio muhusika wa kata ya Buguruni.

Prof anasema anamsihi sana Maalim Seif warudi na kukaa meza moja.Prof Lipumba anasema wametoka mbali sana na Seif,toka 2001 walipouwawa Wazanzibar na yeye kuvunjwa mkono.

Prof Lipumba anasema hana tatizo kabisa na Maalim,anamuheshimu sana na anaomba kama ikiwezekana watoe kesi mahakamani na waje wakae meza moja na kujadiliana kwani mambo yao ya siasa hayawezi kuamuliwa na mahakama.Mambo ya siasa yanahitaji majadaliano na si mahakama.

Prof Lipumba anasema aliamua kurudi baada ya wanachama wengi wa Tz bara na Znz kumsihi sana arudi,japo yeye hakuwa na mpango kabisa wa kurudi.Anasema na siku ya mkutano pale Ubungo Plaza alienda sbb vijana walinzi wa chama walimfuata nyumbani na kumwambia aende kwenye kikao ili kuwaambia wajumbe kuwa anataka kurudi,bahati mbaya Mtatiro kama mwenyekiti wa muda wa mkutano akamkatalia.

Suala la ruzuku,Prof kwa kweli kajichanganya sana.Inaonekana hapa hata yeye hana majibu ya kwanini kunatokea mgogoro wa kuchukua ruzuku,sbb kanuni na tararibu zinakiukwa.Katika suala la ruzuku amemuomba Maalim Seif wakutane,sbb ofisi yake ipo wazi,waje wajadiliane na kupata muafaka.

Prof Lipumba anasema hapendi kuona CUF inagawanyika,wala hapendi kusikia kuna CUF-Zanzibar na CUF-Bara.

Mwisho Prof anasema anamuheshimu na kumtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu wa CUF.Anapenda wakae na Maalim ili kumaliza mgogoro ambao unawaumiza wengi waliokipigania chama kwa jasho na damu kwa miaka mingi sana.Suluhu yao si Mahakamani,bali ni katika meza ya majadiliano.Ataheshimu maamuzi yatakayotolewa na mahakama lakini haamini kama mahakama inaweza kuwa suluhu kwa mgogoro huo wa kisiasa ndani ya chama.

Prof Lipumba anasisitiza "Namuomba Maalim Seif turudi ktk majadiliano,mimi na yeye tunafahamiana sana.Tumekuwa tunafahamiana toka miaka ya 1970.Mgogoro huu unataturika kama tukikaa meza moja.Namuomba aje Buguruni,ofisi ipo wazi kwa majadiliano ili kukirudisha chama ktk mstari"
 
Lipumba anamshangaaa Maalim Seif inakuaje alikubali kuzungumza na CCM walioiba kura zake Mara kadhaa na hata kuua Wanachama wa CUF 2001 lakini hataki kuzungumza na Lipumba eti kisa karudi CUF kipi kibaya zaid Kati ya yeye kurudi CUF na Wanachama wa CUF kuuawa kwa Risasi za Moto lakini a kakubali Mazungumzo na Mwisho wakafikia Makubaliano ?'

Anasema Magufuli na Lowassa wote walikuwa Wagombea wa CCM na hata Mganga wao alikuwa mmoja TB Joshua na baada ya Uchaguzi alikuja kuzungumza nao

Anasema Maalim Seif Hapokei Simu yake wala ofisni hafiki Buguruni sasa angemjulishaje kuhusu Kupokewa kwa Ruzuku?

Anasema Mbatia ndie aliemjulisha Ujio wa Lowassa na hata ndie alietoa Gari yake na kuamuru Dereva ampeleke Lipumba kwa Lowassa kwny Mazungumzo.

Anasema kwny Mkutano wa Wabunge wa UKAWA kabla ya Uchaguzi uliofanyika Kijitonyama Mbowe alimshambulia hadharani Lipumba kuwa anachelewesha Mchakato wa kumtangaza Slaa kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kwa Kuwa Lipumba anasubiria Makapi ya CCM na akaapa Chadema Safari ile haitokubali kapi lolote toka CCM
Anasema Dunia Nzima Migogoro ndani ya Vyama humalizwa kwa Mazungumzo na Seif analijua Hilo lakini Hataki Mazungumzo kwa kuwa anajua Hana uwezo wa kujibu hoja!

Anasema Kazi ya Mahakama ni kuamua Kesi sio kusuluhisha Migogoro

Anasema Seif aliamua kuwavua kina Magdalena Sakaya Uanachama ili wapoteze Ubunge akijua kabisa kwny Chaguzi ndogo ni Kazi sana kukomboa Majimbo hayo kutokana na Nguvu ya Dola ya CCM

Anamshangaa Mbowe kuitisha Press conference na kutangaza atahakikisha Lipumba harudi kuwa Mwnykt wa CUF wakati issue za CUF hazimhusu kabisa

Anasema hata Kama wahenga husema 'Mzigo Mzito mpe Mnyamwezi' lakin kwa hili Nafsi ilimsuta kusimama Jangwani na kumshika Mkono Lowassa na kuwatangazia Wafuasi wao kuwa wamewaletea Edward Lowassa ndie Muarubaini na Kamanda wa Vita dhidi ya Ufisadi wampe kura awe Rais.
 
Lipumba anamshangaaa Maalim Seif inakuaje alikubali kuzungumza na CCM walioiba kura zake Mara kadhaa na hata kuua Wanachama wa CUF 2001 lakini hataki kuzungumza na Lipumba eti kisa karudi CUF kipi kibaya zaid Kati ya yeye kurudi CUF na Wanachama wa CUF kuuawa kwa Risasi za Moto lakini a kakubali Mazungumzo ?'

Anasema Magufuli na Lowassa wote walikuwa Wagombea wa CCM na hata Mganga wao alikuwa mmoja TB Joshua na baada ya Uchaguzi alikuja kuzungumza nao

mweeeee kumbe ccm ni wauwaji mnaanza kutoa siri wenyewe

hii ina maanisha huwezi kumuua mtu bila kulilia au kuiba kisichokuwa chako mkiambiwa ccm huwa wanashindwa mara nyingi mnakataa angalia ulichoandika

kwa maana nyingine maalim anaongea na ma killer!!
 
Lipumba anamshangaaa Maalim Seif inakuaje alikubali kuzungumza na CCM walioiba kura zake Mara kadhaa na hata kuua Wanachama wa CUF 2001 lakini hataki kuzungumza na Lipumba eti kisa karudi CUF kipi kibaya zaid Kati ya yeye kurudi CUF na Wanachama wa CUF kuuawa kwa Risasi za Moto lakini a kakubali Mazungumzo ?'

Anasema Magufuli na Lowassa wote walikuwa Wagombea wa CCM na hata Mganga wao alikuwa mmoja TB Joshua na baada ya Uchaguzi alikuja kuzungumza nao

Anasema Maalim Seif Hapokei Simu yake wala ofisni hafiki Buguruni sasa angemjulishaje kuhusu Kupokewa kwa Ruzuku?

Anasema Mbatia ndie aliemjulisha Ujio wa Lowassa na hata ndie alietoa Gari yake na kuamuru Dereva ampeleke Lipumba kwa Lowassa kwny Mazungumzo.

Anasema kwny Mkutano wa Wabunge wa UKAWA kabla ya Uchaguzi uliofanyika Kijitonyama Mbowe alimshambulia hadharani Lipumba kuwa anachelewesha Mchakato wa kumtangaza Slaa kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kwa Kuwa Lipumba anasubiria Makapi ya CCM na akaapa Chadema Safari ile haitokubali kapi lolote toka CCM
Magufuli na Lowasa wanaunganishwa na "upendo wa agape" na Lipumba na maalim Seif wanatenganishwa na " kisasi" mwenye uelewa na aelewe!
 
mweeeee kumbe ccm ni wauwaji mnaanza kutoa siri wenyewe

hii ina maanisha huwezi kumuua mtu bila kulilia au kuiba kisichokuwa chako mkiambiwa ccm huwa wanashindwa mara nyingi mnakataa angalia ulichoandika

kwa maana nyingine maalim anaongea na ma killer!!

Tuliza Kichwa chako uelewe.

Hayo ni Maneno ya Mwenyekt wa Taifa na Big boss wa Chama cha Maalim Seif Sharif Hamad na Muasisi wa UKAWA Prof. Ibrahim Haruna Lipumba sio Maneno yangu!

Mie Kazi yangu ilikuwa kuwasilisha kwako msomaji hoja za Prof .lakini bahati mbaya pia hujaelewa ukakurupuka!
 
Blames must go directly to the corrupt and power monger mr Lowassa for having intentions to kill democracy in our country
 
Tuliza Kichwa chako uelewe.

Hayo ni Maneno ya Mwenyekt wa Taifa na Big boss wa Chama cha Maalim Seif Sharif Hamad na Muasisi wa UKAWA Prof. Ibrahim Haruna Lipumba sio Maneno yangu!

Mie Kazi yangu ilikuwa kuwasilisha kwako msomaji hoja za Prof .lakini bahati mbaya pia hujaelewa ukakurupuka!

lupumba kaongea hayo ya mauaji sio maalimu amekiri ccm ni ma killer na wezi kwa hiyo anaomba kuongea na maalimu aache kuongea na ma killer
 
Tuliza Kichwa chako uelewe.

Hayo ni Maneno ya Mwenyekt wa Taifa na Big boss wa Chama cha Maalim Seif Sharif Hamad na Muasisi wa UKAWA Prof. Ibrahim Haruna Lipumba sio Maneno yangu!

Mie Kazi yangu ilikuwa kuwasilisha kwako msomaji hoja za Prof .lakini bahati mbaya pia hujaelewa ukakurupuka!
Hata wewe ndio haohao wanaomshangilia na kumpa ulinzi, VIBALI kufanya mikutano na ruzuku Propesa ili auwe UKAWA.
 
Back
Top Bottom