Prof. Lipumba na Lissu wakosoa uteuzi wa Prof. Muhongo

Prof. Lipumba na Lissu wakosoa uteuzi wa Prof. Muhongo

pakaywatek

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
4,710
Reaction score
6,372
Saa chache baada ya rais Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alikuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini.

Profesa Lipumba amekosoa uteuzi wa profesa Muhongo kwa madai kuwa uteuzi wake umelitia doa baraza hilo.

"Kwa kitendo kama hiki, Rais Magufuli amejiwekea dosari kutokana na uteuzi huu. Maana yake ni kuwa katika kashfa ile Profesa Muhongo hakuwa na hatia," Profesa Lipumba aliliambia gazeti la Mwananchi.

Profesa Lipumba aliongeza kuwa wananchi watapata ugumu kumuelewa Rais kutokana na ahadi zake kuwa atapambana na rushwa na ufisadi.


Naye Tundu Lissu aliliambia gazeti hilo kuwa uteuzi wa Dk. Harison Mwakyembe hakuwa sahihi kwa kuwa ndiye aliyekuwa waziri wa Uchukuzi na punde baada ya rais Magufuli kuingia ikulu, Mamlaka ya Bandari ikabainika kukumbwa na kashfa ya upotevu wa makontena.

"Juzi Rais Magufuli aliufumua uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa, miongoni mwa waziri waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk. Harrison Mwakyembe, eti leo amemrudisha kundini?" Lissu ananukuliwa.

Lissu aliongeza kuwa Muhongo pia hakufaa kuwa miongoni mwa mawaziri kwa kuwa alifukuzwa na Bunge kutokana na sakata la Escrow.

Hata hivyo, Profesa Lipumba alimpongeza rais kwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda baraza dogo kwa lengo la kubana matumizi.



============

MSIKILIZE PROF. LIPUMBA: View attachment HAPA.mp3 : HAPA
 
Lipumba naye atulie alee wajukuu, Muhongo hakujiuzuru kwasababu ya ufisadi maana hakuna sehemu ripoti ya CAG ilimtaja kuhusika moja kwa moja na suala la ESCROW, Muhongo alijiuzuru kwa manufaa ya taifa.

Hiyo wizara bado inamfaa na hakuna mbadala.

Msiyemtaka kaja.
 
Huyo naye ni pumba kweli. Kama kuna mawaziri vichwa ni Muhongo na Mwijage. Ni wasomi waliobobea. Muhongo taifisha IPTL haraka na kamata yule kalasinga aliyekutapeli.
Hizo pesa za Escrow zilitolewa wakati Muhongo akiwa anaongoza hiyo wizara!!
 
Huyu mzee anaanza kupotea kisiasa na atapotea kama Lowasa
 
prof Muhongo yule aliyewatafutia watoto wa wanyonge watanzania scholarship za kusomea utaalam wa gesi na mafuta kule China.????
huyu ndio SI unit ya kutupeleka kwenye uchumi wa kati makanda.
wafanyabiashara wakubwa hawampeeeendi nahisi walivyosikia jina lake wali paralize. walipata kiharusi hapohapo.
Bigup! Magufuli
 
Nilivyoifuatilia issue ya Tegeta Escrow mhe Muhongo hakustahiri kufanyiwa yale aliofanyiwa, ile issue ina mwenyewe na mwenyewe anajulikana; kama kuna mawaziri ambao nimeponheza uteuzi wao basi profesa Muhongo na Lukuvi. Hao wengine hata wasipokiwepo sawa tu.
 
Amedai kumteua Muhongo kwenye baraza jipya la mawaziri wakati alijiuzulu baraza lililopita kwa kashfa ya ufisadi ni kwenda kinyume na maadili ya uongozi.

Chanzo: DW

.
Ameagizwa na chama amkomoe Mengi. Na bado kuna fununu za kumleta Dialo ndani ya baraza katika wizara zilizo wazi bado. ccm ni ile ile!!!
.
 
prof Muhongo yule aliyewatafutia watoto wa wanyonge watanzania scholarship za kusomea utaalam wa gesi na mafuta kule China.????
huyu ndio SI unit ya kutupeleka kwenye uchumi wa kati makanda.
wafanyabiashara wakubwa hawampeeeendi nahisi walivyosikia jina lake wali paralize. walipata kiharusi hapohapo.
Bigup! Magufuli

Mnashangilia mtu anayewakatisha tamaa wawekezaji wa ndani? Mnapenda uchumi ushikwe na wawekezaji wa nje pekee yao. Nadhani pamoja na umahiri wake katika sekta hii lakini katika hili hayuko sahihi.
 
Lipumba mwenyewe ni mnafiki, Mpuuzi sana huyu Profesa feki!
 
Amedai kumteua Muhongo kwenye baraza jipya la mawaziri wakati alijiuzulu baraza lililopita kwa kashfa ya ufisadi ni kwenda kinyume na maadili ya uongozi.

Chanzo: DW
prof atakuwa kasemewa kwani kila mtanzania anajua nguvu ya mafisadi kwa kipindi kilichopita ililazimu tu muhongo apishe ukizingatia wabunge wenyewe walinunuliwa na wakatusaliti watanzania
 
Back
Top Bottom