Prof. Lipumba: Maalim Seif hajahama Chama, amefukuzwa

ndio agenda ya mkutano au ilikuwa by way. maana huwezi kila mara umamzungumzia loose.
 
Hahahah. Huyu mzee naona anaweweseka sasa. Nimeona clip moja znz watu wakishusha bendera za cuf na kupandisha za act ni noma aisee. Huyu lipumba na wengine hawakutegemea kama seif atahama cuf. Pole prof umeachiwa chama chako kiongoze sasa.

Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahi Lipumba amewataka Wanachama wa chama hicho wanaotaka kukihama chama na kuhamia ACT Wazalendo kuungana na katibu mkuu wa Zamani Maalim Seif Shariff Hamadi, kuchanganya akili zao na kutokurupuka kwani wanaweza kujulikuta wamekuwa bendera fuata upepo pasipo kujua upepo una uelekeo gani.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Dar es Salaam, Prof. Lipumba amesema kuwa kwanza kabla ya Maalim Seif kukihama chama hicho tayari alikuwa amefukuzwa.

"Mimi na sisi kama Chama cha Wananchi CUF tunachokijua Maalim Seif alifukuzwa kuwa mwanachama wa chama chetu kwenye mkutano mkuu uliopita, baada ya kubaini hana nia njema ya chama na anataka kukidhoofisha sio kwamba amehama chama bali amefukuzwa," amesema Prof. Lipumba.

Utakumbuka hapo jana Marchi 18, 2018 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif alitangaza kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo. Hiyo ni baada ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kutimua kiongozi hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaotaka kuhama wajiatafakari.

Hii inamaanisha anajua wazi kua CUF haina wanachama. Imebaki kwenye makaratasi.

Ila pia ACT wana mzigo wa Kumuabudu Maalim as ikitokea kahama basi wanachama wataondoka naye.
 
Awe amefukuzwa au kuhama, la msingi ni kwamba hayupo CUF na hahusiki chochote na CUF.. Lipumba ameachiwa CUF aendelee na CUF yake, swali adui yake ni ACT na MAALIM au CCM?
 
Prop Lipumba amebaki kuwa White Elephant project ya CCM, alichotarajia na walichotarajia sicho kilichotokea sasa kifuatacho ni Lipumba kutelekezwa huku watu wakitafuta plan B, Mzee uza tu jengo la buguruni ujilipe kiinua mgongo chako maana huwezi tena kufanya kazi hauna credibility tena, matendo yako yamekuvua uprofesa..
 
Hivi lipumba si ndio alianzisha CUF mpaka kesho ni mwenyekiti huko CUF hawanaga uchaguzi?
 
Mbona Lipumba analialia sana atulie anabembeleza wanachama wasifuate upepo anaona ndo mwisho wake,anahofia ruzuku ileee inaondoka
 
Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahi Lipumba amewataka Wanachama wa chama hicho wanaotaka kukihama chama na kuhamia ACT Wazalendo kuungana na katibu mkuu wa Zamani Maalim Seif Shariff Hamadi, kuchanganya akili zao na kutokurupuka kwani wanaweza kujulikuta wamekuwa bendera fuata upepo pasipo kujua upepo una uelekeo gani.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Dar es Salaam, Prof. Lipumba amesema kuwa kwanza kabla ya Maalim Seif kukihama chama hicho tayari alikuwa amefukuzwa.

"Mimi na sisi kama Chama cha Wananchi CUF tunachokijua Maalim Seif alifukuzwa kuwa mwanachama wa chama chetu kwenye mkutano mkuu uliopita, baada ya kubaini hana nia njema ya chama na anataka kukidhoofisha sio kwamba amehama chama bali amefukuzwa," amesema Prof. Lipumba.

Utakumbuka hapo jana Marchi 18, 2018 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif alitangaza kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo. Hiyo ni baada ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kutimua kiongozi hiyo.
Ujumbe huu una wafaa Hata kwa watakao baki maana Viongozi wenu wa Kitaifa wa CUF hawatunzi kauli zao mara nyingi viongozi wenye uchu wa Madaraka hawana uwezo wa kuimarisha chama. Chama imara hakina migogoro
 
Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahi Lipumba amewataka Wanachama wa chama hicho wanaotaka kukihama chama na kuhamia ACT Wazalendo kuungana na katibu mkuu wa Zamani Maalim Seif Shariff Hamadi, kuchanganya akili zao na kutokurupuka kwani wanaweza kujulikuta wamekuwa bendera fuata upepo pasipo kujua upepo una uelekeo gani.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Dar es Salaam, Prof. Lipumba amesema kuwa kwanza kabla ya Maalim Seif kukihama chama hicho tayari alikuwa amefukuzwa.

"Mimi na sisi kama Chama cha Wananchi CUF tunachokijua Maalim Seif alifukuzwa kuwa mwanachama wa chama chetu kwenye mkutano mkuu uliopita, baada ya kubaini hana nia njema ya chama na anataka kukidhoofisha sio kwamba amehama chama bali amefukuzwa," amesema Prof. Lipumba.

Utakumbuka hapo jana Marchi 18, 2018 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif alitangaza kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo. Hiyo ni baada ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kutimua kiongozi hiyo.
Ni kweli wanatakiwa kuchanganya akili zao...kubaki CUF isiyo CUF waliyoijua au kwenda ACT wasiyoijua kwa sasa ya Maalimu Seif wanayemjua! Ni kazi ngumu.
 
Viongozi wenye uchu wa madaraka hawana uwezo wa kuondoa migogoro kwenye chama wala kuimarisha chama
 
😁😁😁Tatizo lipumba hajui mchezo wa mpira 🤗 ukipiga chenga nyingi Sana mwishowe huwa Kuna kujifunga😎😎😎 kwa sasa Naona Dk za nyongeza Lipumba Anajifunga Goli mwenyewe, Akidhani kuwa yupo Golini kwa Wapinzani 😋kumbe ndio Kwanza kapewa pass chonganishi na kipa(Mahakama) 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Natamani mh Spika awaulize hao wabunge wa CUF kuwa wapo pamoja na m/kiti wao au?? Kama hawapo naye inamaana majimbo hayo yako wazi. Uitishwe uchaguzi haraka tujaze nafasi hizo. Hapo ndio itakuwa kipimo cha CUF huko Zenj na CCM pia endapo watanyakua hata kiti kimoja tutafurahi
 
Back
Top Bottom