Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Status
Not open for further replies.
Si jambo la ajabu sana kwenda huko maana wote kiitikadi (Zitto na Lipumba) ni sawa. Sale outs. Hakuna jipya. Kwa wasiolewa watashangalia lakini hii ni political strategy ya CCM kucheza na akili za watu. Ni dhahiri kuwa ACT ni CCM B na kipindi cha uchaguzi kina Slaa walipokuwa wanakaa Serena kwa siri na Lipumba kwenda vacation Rwanda halafu States sasa ni wakati wa kutumikia ruzuku waliozokula. Hamjiulizi Lipumba alikuwa wapi siku zote toka alipojiuzulu asidai ueneyekiti wake tena mpaka juzi na baada ya kuja tu CUF imesambaratika. Alikuwa kwenye mission kaitimiza.

Dhamira hapa ni kudhoofisha upinzani. Kitakochofuata Slaa nae atajiunga ACT na wale wachumia tumbo wa upinzani wote watakwenda huko pia kujifanya wanapigania nchi.

CUF tayari kuna mtafuruku ambao Lipumba ana mkono wake, CHADEMA napo hakukaliki kina Lema na Lissu kutwa wapo lupango, mwenyekiti anadhoofishwa kiuchumi, muda si mrefu watakuwa chali. Hapo sasa ACT wataonekana ndio tegemezi la wanyonge while in reality ni decoy tu.

Come 2020 aidha Lipumba ama Slaa atasimama kugombea urais ambapo in reality itakuwa ni CCM A versus CCM B na mshindi mnajua atakuwa nani. Na hii ndio Tanzania yetu ya kidemokrasia na amani tele............................

Tatzo liko wapi? Kama Lowassa yule, yule aliyeitwa majina yote mabaya na CDM alihamia CDM na ndani ya siku chache akateuliwa kupeperusha Bendera ya CDM kuna ubaya gani Prof. Kuhama CUF kama hajaridhika na maamuzi kama ilivyokuwa kwa Lowassa.
Anyway, hw sure are you that Lowassa's move to CDM wasn't a decoy? Au unaongea tu baada ya kura maharage cjui ya wapi!
 
Wadau,

Katika kile kinachoonekana kwa mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Wananchi (CUF) kuipenda nafasi hiyo ambayo huenda alikula kiapo kwamba hadi allah atakapomuita basi aondoke akiwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti, haijalishi ni wapi ila awe mwenyekiti tu! Yaani iwe kwenye siasa, vyama vya kijamii (kufa na kuzikana) au kwenye vigodoro lazima awe mwenyekiti tu!

Leo ameibukia hukooo kwa kiongozi mkuu wa chama, Hukooo! kwenye chama cha wazalendo ACT kwa lemgo la kuungana na akina M1, M2, sijui na nani mwingine vile. Vyanzo vya karibu vinatonya kuwa huko nako anataka uenyekiti. Sasa najiuliza Iron Lady aliyepeperusha bendera kwa nafasi ya Urais na kuweka historia ya kuwa mwanamke pekee Tanzania aliyegombea nafasi hiyo katika uchaguzi uliopita wa Rais, Wabunge na Madiwani. Je atakubali kumpisha Mzee wa Intarahamwe ili ashike usukani???????.....

Move ndo kwanza inaanza!!!!

Tusubiri Babu na yeye sijui atakuja na song la kutaka ukatibu!!!!!!!!
Kumbu kumbu zinaonesha uenyekiti wa milele ni wa Mbowe mkwepa kodi.

BTW mbona hata nyie mlimchukua Lowassa baada ya kumpa matusi yote mabaya.
 
Mkuu Molemo, asante kwa Taarifa, Prof. Lipumba kisiasa ni spent force, Zitto anamkaribisha tuu ili kumtumia kama mtaji kwa kuwavuta wale wafuasi wake bendera fuata upepo ili aipasue CUF na kuiimarisha ACT kwa kupanua wigo wa membership base tuu lakini kiukweli Lipumba hana lolote jipya atakalofanya CUF kwa sababu Uenyekiti wa ACT, ni uenyekiti kilemba cha ukoka tuu, all the powers lies with ZZK, Lipumba kwa vile ni power monger, can't stand kufanywa boya hivyo he will demand real powers na hapo ndipo itakapoibuka vita na mwenye chama chake! .

Hivi Prof. Lipumba ni lazima tuu awe Mwenyekiti? . Hawezi kuwa mwanachama tuu wa kawaida?!.

Pasco

Bro nani hapendi madaraka!
Nijibu swali hili, Lowassa alipohamia CDM ilikuwa lazima yeye ndo agombee urais kupitia CDM? Kwa nini hakukubali kuwa mwanachama wa kawaida? Kuna tofauti gani ya hiki unachokiponda hapa na alichokifanya Lowassa?
Au kwa vile Lowassa baba yako, bila yeye mkono hauingii kunako!
 
Kwa usajili huu Act watachukua ubingwa wa Epl msimu huu hakuna cha morinho wala man u
 
Mimi nilijua hivi karibuni atatangaza kujiunga ccm, hata hivyo ACT panamfaa kabisa. Dhambi ya usaliti ni mbaya sana.
 
Hahahaaa...kweli Act wazalendo kimekuwa chama rasmi cha wasaliti teh teh teh ..2020 lazima mmoja atokee ubavuni
 
Mkuu Molemo, asante kwa Taarifa, Prof. Lipumba kisiasa ni spent force, Zitto anamkaribisha tuu ili kumtumia kama mtaji kwa kuwavuta wale wafuasi wake bendera fuata upepo ili aipasue CUF na kuiimarisha ACT kwa kupanua wigo wa membership base tuu lakini kiukweli Lipumba hana lolote jipya atakalofanya CUF kwa sababu Uenyekiti wa ACT, ni uenyekiti kilemba cha ukoka tuu, all the powers lies with ZZK, Lipumba kwa vile ni power monger, can't stand kufanywa boya hivyo he will demand real powers na hapo ndipo itakapoibuka vita na mwenye chama chake! .

Hivi Prof. Lipumba ni lazima tuu awe Mwenyekiti? . Hawezi kuwa mwanachama tuu wa kawaida?!.

Pasco

Ndio Prof Lipumba lazima afie kwenye kiti,lazima agombee uRais hilo liko wazi jamaa yuko kimaslahi zaidi.

Zitto yuko kimkakati zaidi,yeye ni Kiongozi mkuu nguvu zote za chama ziko chini yake nafasi ya mwenyekiti ACT ni sawa na katibu mwenezi unapiga parapanda weeee mwisho wa siku Kiongozi Mkuu ndio mwenye kauli ya mwisho.

Prof Lipumba na Zitto lazima wataparangana kwasababu kila mmoja atapenda kugombea urais,kila mmoja atapenda ukuu wa chama na kuwa na kauli ya mwisho katika masuala yote ya chama.

Kwanini Zitto kakubali kumpokea Prof Lipumba,Mosi anajua ACT ipo Kigoma tu haina anafsi ya kufurukuta katika siasa za Tanganyika.Prof ana uzoefu wa fitna za siasa ana weza kuleta base kubwa ya wanachama wasiofikiri hasa wale wanywa ghahawa washinda vibarazani.Anafahamu kanda ya kusini hasa pwani CUF ilikuwa na base kubwa sana ya wanachama yamkini Prof anaweza kuondoka nayo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom